Sunday, May 19, 2013

majadiliano ya ushirikiano kwa manufaa ya wote yamalizika Visiwani Zanzibar


Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (tnbc) Bw. Raymond Mbilinyi, akizungumza na washiriki mbalimbali mjini Unguja Visiwani Zanzibar wakati wa kuhitimisha majadiliano ya ushirikiano kwa manufaa ya wote (smart partnership dialogue) katika ngazi ya kanda ikiwa ni hatua ya kuelekea katika ngazi ya kitaifa, (katikati) ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dk. Idrisa Hija na mwisho (Kulia) nia Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Zanzibar Bw. Ali Vuai.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (tnbc) Bw. Raymond Mbilinyi, (kushoto) akifurahia jambo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Zanzibar Bw. Ali Vuai, wakati wa kuhitimisha majadiliano ya ushirikiano kwa manufaa ya wote (smart partnership dialogue) katika ngazi ya kanda ikiwa ni hatua ya kuelekea katika ngazi ya kitaifa. Majadiliano hayo yalifanyika huko Unguja Visiwani Zanzibar.

Na Mwandishi Wetu,Unguja-Zanzibar

Baaada ya kufungwa rasmi kwa majadiliano ya ushirikiano kwa wote katika ngazi ya kanda kwa mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar, Baraza la Taifa la Biashara limesema mafanikio makubwa yamejitokeza katika ushiriki wa watu katika kutoa mawazo yao.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (tnbc) Bw. Raymond Mbilinyi, aliyasema hayo Visiwani Zanzibara wakati wa kuhitimisha majadiliano hayo katika ngazi ya kanda visiwani humo.

“Kwa kweli sisi kama tnbc tumefarijika sana na majadiliano haya yaliyomalizika katika kanda ya Zanzibar, tathmini inaonyesha watu wamekuwa na mwamko mkubwa wa kuelezea mambo mbalimbali katika mada zilizokuwa zinatolewa”, alisema Mbilinyi.

Aliongeza kuwa katika kanda zote kumi na moja walizofanya majadiliano haya wameweza kupata wale watu ambao walikuwa wanawatarajia kushiriki na kimsingi wameweza kufika na kutoa mawazo yao katika kuchangia mada na hata katika kuuliza kile ambacho kilikuwa kinawatatiza hapo awali kulingana na mada husika iliyotolewa na wawwezeshaji.

“Kwa mikutano yote iliyofanyika hadi sasa ushiriki umekuwa ni wa hali ya juu, na watu wamefurahia mada kuu ya majadiliano ambayo ni jinsi gani teknolojia inaweza kutumika katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii”, aliongeza.

Alisisitiza kuwa baada ya kumaliza majadiliano katika ngazi ya kanda jambo kubwa lililo mbele yao ni maandalizi kuelekea katika majadiliano ya kitaifa, ambayo yanatarajiwa kufanyika kuanzia juni 1 – 2 mwaka huu.

“ Katika majadiliano haya ya kitaifa kutakuwa na uwakilishi katika mikoa na ngazi ya taifa na nimategemeo yangu kuwa watu wataweza kuweka mawazo yao kwa ufasaha zaidi hasa ukizingati tayari wameshapata ufahamu wa kutosha kutokana na majadiliano katika ngazi ya kanda” alisisitiza.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Zanzibar Bw. Ali Haji Vua alisema mapokeo kwa upande wa kanda ya Zanzibara yalikuwa ni mapokeo chanya kutokana na watu kutoa mawazo yao kwa uwazi na jinsi walivyo changia mada zilizowasilishwa.

“Watu wamezungumza kwa uwazi, wameonyesha changamoto na njia gani ya kuzitatua ambapo naamini zikitumiwa vizuri zitaweza kuleta mabadiliko kwa Zanzibara na Tanzania kwa ujumla”, alisema Vuai.

Aliongeza kuwa baada ya majadiliano ya Zanzibara kumalizika wataandaa ripoti na kuipeleka katika ngazi ya kitaifa iambayo itawasilishwa katika mkutano huo ikiwa ni pamoja na kuchagua watu watakao wakilisha Zanzibar katika majadiliano ya kitaifa.

Zanzibara inategemea kuwa na washiriki 45, ambapo kila kundi litatoa watu watano, katika makundi ya vijana , wasanii, wanahabari, wnataaluma , watu wa usalama, kwa hiyo kazi kubwa tunayo ni kuwaandaa ili waweze kwenda kutoa michango mizuriitakayokuwa na manufaa kwa Tanzania”, alisisitiza.

Majadiliano ya ushirikiano kwa manufaa ya wote yamemalizika katika awamu ya kwanza, ambapo yalikuwa yakijadiliwa katika ngazi ya kanda kabla ya kuelekea katika ngazi ya kitaifa juni 1 – 2 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment