Monday, May 27, 2013

HATIMAE MSHINDI WA PROMOSHENI YA VODACOM MAHELA AKABIDHIWA KITITA CHAKE KINONO KWEUPEEE

Mwanafunzi wa Chuo Cha Ualimu Kasulu, mkoani kigoma Valerian Nickodemus Kamugisha akinyannyua kwa Furaha sehemu ya fedha Sh 100 Milioni alizoshinda katika droo kuu ya Promosheni ya Vodacom Mehala iliyomalizika hivi karibuni. Kamugisha amekabidhiwa fedha zake hizo leo jijini Dar es salaam na kuamua kuzifungulia akaunti katika benki ya NMB. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB Bw.Abdulmajid Nsekela na Mkuu wa Chapa Vodacom na Mawasiliano Kelvin Twissa.
Mkuu wa Chapa Vodacom na Mawasiliano Kelvin Twissa akimtambulisha kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) mshindi wa Promosheni kuu ya Mahela iliyomalizika hivi karibuni Valerian Nickodemus Kamugisha (kushoto) wakati wa hafla ya kumkabidhi kitita chake cha zawadi ya sh. 100 Milioni iliyofanyika makao makuu ya NMB. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB Bw.Abdulmajid Nsekela.
Valerian Nickodemus Kamugisha (katikati) akipokea kitita cha sh. 100 Milioni kutoka kwa Mkuu wa Chapa Vodacom na Mawasiliano Kelvin Twissa alizoshinda katika droo kuu ya Promosheni ya Vodacom MAHELA. Hafla ya makabidhiano imefanyika makao makuu ya benki ya NMB ambako mshindi huyo amechagua kufungua akaunti kuhifadhi fedha hizo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB Bw.Abdulmajid Nsekela.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa benki ya NMB Abdulmajid Nsekela akimkabidhi kadi ya ATM Mshindi wa promosheni ya Vodacom MAHELA Valerian Nickodemas Kamugisha (22) punde baada ya kukabidhiwa fedha hizo na kampuni ya Vodacom Tanzania, anayeshuhudia ni Mkuu wa Chapa Vodacom na Mawasiliano Kelvin Twissa.


Siku chache baada ya Mwanafunzi wa chuo cha ualimu Kasulu mkoani Kigoma, Valerian Nickodemus (22) kuibuka kidedea na kujishindia kitita cha Shilingi milioni 100 katika promosheni ya MAHELA iliyoendeshwa kwa mafanikio makubwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, sasa ni zamu ya Watanzania wengine kujumuika na kucheka nae baada ya kuzinduliwa tena kwa Promosheni nyingine ya Cheka Nao.

Promosheni hiyo ambayo imezinduliwa hivi karibuni itaendelea kuleta faraja na mafanikio kwa wateja wa kampuni hiyo kwa kuweza kujinasua katika hali duni ya maisha. Baada ya zaidi ya Watanzania 300 kunufaika kwa kujishindia fedha taslimu katika Promosheni ya MAHELA iliyomahitimishwa Aprili 24 mwaka huu, sasa zaidi ya wateja 6000 wa Vodacom watajishindia Zawadi mbali mbali kwa kipindi cha siku 60.

Akizungumza wakati akikabidhiwa fedha zake za Ushindi, mshindi wa Shilingi Milioni 100 wa Promosheni ya MAHELA, Valerian Nickodemus amewaomba Watanzania kutambua mchango mkubwa unaofanywa na Kampuni ya Vodacom nchini katika kujenga na kuimarisha maisha ya Watanzania.

"Nimefuatilia Promosheni ya Mahela watu wengi walio jishindia fedha hizo ni wajasiriamali wadogo wadogo kama vile; wamachinga, mama ntilie, na wazee wastaafu ambapo kwa kiasi kikubwa tunajua watu wa aina hii wanahitaji msaada ili kujiendeleza kiuchumi. Kwa fedha ambazo wamezipata wengi zimewasaidia kujikwamua na kujiendeleza kimaisha," alisema Nickodemus.

Aliongeza kuwa kwa upande wake kuwa ni mfano dhahiri wa Watanzania waliokuwa wakihitaji msaada tangu zamani. "Sasa nimepata mwanga katika maisha yangu baada ya kujishindia fedha hizi kwa sababu sijapewa masharti wala utaratibu wowote wa matumizi ya fedha hizi, unafahamu maisha ya walimu wengi yalivyo duni lakini sasa nina uhakika wa maisha yangu na familia yangu kupitia ushiriki wangu katika Promosheni hii ya Vodacom MAHELA," alisema.

Amesema ataendelea kujaribu bahati yake katika promosheni hii mpya ya Cheka Nao, na amewataka Watanzania ambao ni wateja wa Vodacom kutumia fursa hii kujaribu bahati zao katika promosheni hii mpya na nyingine zote kutoka Vodacom kwani yaweza kuwa ndio njia yao kujikwamua kimaisha na kubadilisha kabisa mfumo wao wa maisha.

Hivyo, Nickodemus amewashauri Watanzania kujiunga na kuutumia Mtandao wa Vodacom hususan huduma ya Cheka Nao ambayo inawaruhusu wateja wa mtandao wa Vodacom kupiga simu kwenda mitandao mingine kwa gharama nafuu zaidi na pia waweze kujishindia zawadi mbalimbali za fedha taslim zaidi ya kiasi cha shilingi milioni 100.

"Unajua ni jambo la kushangaza sana kwanza tumewezeshwa kupiga simu kwa bei nafuu kwenda mitandao mingine na kisha tunapata fursa ya kujishindia fedha, hii ni zaidi ya kuwasiliana hivyo basi ninawasihi Watanzania wenzangu kujiunga na mtandao wa Vodacom na kutumia huduma ya Cheka Nao ili waweze kujishindia fedha na kuboresha maisha yao, nami nitaendelea kushiriki tena na tena," alihitimisha huku akitabasamu.

Pamoja na mambo mengine benki ya NMB imejitolea kutoa mafunzo ya ujasiriamali na matumizi sahihi ya fedha kwa Mshindi huyo ili kumuwezesha kuwa na matumizi yenye tija.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika makao makuu ya benki ya NMB, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Abdulmajid Nsekela, amesema kuwa benki yake imekuwa na ushirikiano mzuri wa kibiashara na kampuni ya Vodacom hasa kupitia huduma yake ya M - pesa.

"Tumekuwa na uhusiano mzuri na kampuni ya Vodacom, Hivyo tumeona ni vyema kutumiaa fursa hii kutoa elimu kwa mshindi wa promosheni hii ili kumuwezesha awe na matumizi sahihi ya fedha yatakayo leta tija katika maisha yake, wataalamu wetu watampatia elimu ya ujasiriamali ili aweze kujiendeleza kutokana na fedha hizo, alisema Nsekela.

Promosheni ya Cheka Nao inatoa fursa kwa Wateja wa mtandao wa Vodacom kujiunga na huduma ya Cheka Nao kwa kupiga *149*01# ambapo mteja atapata dakika 20 za kupiga kwenda mitandao yote zinazotozwa kwa sekunde, SMS 150 na MB 60 zinazotumika kwa masaa 24 na kupata nafasi ya kujishindia fedha taslim ambapo zaidi ya shilingi Milioni 200 zimetengwa kwa ajili ya zawadi kwa washindi.

Washindi 10 watajishindia shilingi 50,000/- kwa siku, washindi wengine 100 watajishindia shilingi 10,000/- kwa siku na washindi watano watajishindia shilingi 2m/- kwa mwezi.

No comments:

Post a Comment