Friday, March 8, 2013

WASHIRIKI WA FAINALI ZA TAIFA MISS UTALII TANZANIA 2012/13 WAPIGWA MSASA



Juu na chini ni Kaimu mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi hiyo Ndugu Devotha Mdachi akifungua Semina hiyo Maalum kwa Warembo wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 .
Mtoa Mada Mkuu wa Semina hiyo ya Mafunzo ya Kitalii Ndugu Deogratias Malogo ambaye ni Meneja wa Utafiti na Maendeleo wa Bodi ya Utalii Tanzania , akiwafundisha Warembo wa Miss Utalii Tanzania Taifa 2012/13 pamoja na kujibu maswali yao mbalimbali wakati wa mafunzo hayo
Raisi wa Miss Utalii Tanzania Organisation Ndugu Erasto G. Chipungahelo Akiishukuru Bodi ya Utalii Tanzania kwa Kubari kwao kufanya semina hiyo ya Mafunzo ya utalii kwa Warembo wa Miss Utalii Tanzania Taifa 2012/13.
Kwa picha na maelezo zaidi bofya read more
Washiriki wa Miss Utalii Tanzania Taifa 2012/13 wakipitia kwa umakini majarida yanayo elezea Utalii Tanzania
Washiriki wa Miss Utalii Tanzania Taifa 2012/13 wakiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya viongozi pamoja na wafanyakazi wa Bodi ya Utalii Tanzania.
Washiriki wa Miss Utalii Taifa 2012/13 wakiwa katika picha ya pamoja Mara baada ya Semina Maalum ya Mafunzo kwisha.

Serikali kupitia Bodi ya Taifa ya Utalii,imeendesha semina ya washiriki wa Fainali za Taifa Miss Utalii Tanzania 2012/13 iliyo fanyika leo Katika ukumbi wa mikutano uliopo Makao makuu ya Bodi ya utalii Tanzania.
Semina hiyo ambayo ilifunguliwa na Kaimu mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi hiyo Ndugu Devotha Mdachi, imeandaliwa na Bodi ya Utalii kwa lengo la Kuwapiga msasa washiriki hao kabla ya fainali ya Taifa itakayo fanyika 17.03.2013 katika ukumbi wa Dar Live.

Akifungua Semina hiyo Ndugu Devotha mdachi pamoja na kuwakaribisha washiriki wote makao makuu ya Bodi ya Utalii Tanzania aliwaasa washiriki hao kujifunza na kuvielewa kwa kina vivutio vya utalii Tanzania ili wale watakao shinda na kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia waweze kuitangaza vema Utalii wa Tanzania na nchi kwa Ujumla. Aliwakumbusha pia wao kama warembo wa utalii wanalo jukumu la kuunda mkono juhudi za Serikali kuhamasisha utalii wa Ndani lakini pia jukumu la kutangaza vivutio vya utalii wa Tanzania kimataifa na Kimataifa. Aliendelea kuwaasa pia wao kama warembo wa utalii wanapaswa kujivunia utanzania na Maliasili zake huku wakidumisha Mila na Utamaduni wa Tanzania na kwamba siku zote wanatakiwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu na mfano wa kuigwa katika jamii kwa maana warembo wa utalii ni alama ya Urithi wa Taifa na kielelezo cha Mwanamke wa Kitanzania. Aliwakumbusha wale watakao shinda kwenda kutetea Mataji ya Dunia ambayo Miss Utalii Tanzania wanashikiria .

Nae mtoa mada Mkuu katika semina hiyo Ndugu Deogratias Malogo ambaye ni Meneja wa Utafiti na Maendeleo wa Bodi ya Utalii Tanzania aliwafahimisha warembo wa Miss Utalii Tanzania wa Fainali za Taifa 2012/13 kuwa secta ya utalii ni secta muhimu katika Uchumi na kuchangia pato la Taifa kila mwaka. Alisema Secta ya utalii inachangia zaidi ya asilimia 20 ya pato la Taifa kila mwaka na zaidi ya asilimia 25 ya pato la taifa la fedha za kigeni kila Mwaka. Alisema Kidunia secta ya utalii inachangia zaidi ya asilimia 12 ya ajira zote Duniani.

Warembo hao walifundishwa Historia ya utalii Tanzania . Walifundishwa vivutio vya utalii Tanzania, Mbinu za kutangaza utalii wa Tanzania Kitaifa na Kimataifa, lakini aliwaelezea pia jitihada ambazo serikali kupitia bodi ya taifa ya utalii na Mamlaka nyengine za utalii nchini imekuwa ikifanya katika kukuza secta ya utalii na kutangaza vivutio vya utalii kitaifa na Kimataifa. Ndugu Malogo aliwaelezea juu ya umuhimu wa utalii wa ndani katika kukuza na kuchangia pato la utalii la Taifa na kwamba wao kama warembo wa utalii ni sehemu muhimu katika kukuza na kuendeleza secta ya Utalii Tanzania kwani wao ni kioo cha jamii na mfano wa kuigwa kitabia Mwenendo Muonekano na Hulka. Aliwatakia kila laheri wale watakao shinda katika fainali hizo za Taifa kwenda kuwa mabarozi bora wa Tanzania katika mashindano ya Dunia watakayo kwenda Kushiriki.

Nae Rais wa Miss Utalii Tanzania alitoa shukurani na Pongezi kwa Bodi ya Utalii Tanzania kwa juhudi kubwa wanazo fanya ya kuinua na kuendeleza secta ya utalii nchini. Alipongeza na kushukuru pia hatua ya bodi ya utalii, kwa kuendesha Semina Maalum kwa washiriki wa fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania 2012/13 na kusema kwamba semina hii itakuwa ni Dira na ufunguo kwa Miss Utalii Tanzania wa kutwaa mataji zaidi ya Dunia katika mashindano yote watakayo shiriki na pia katika kutangaza na kuhamasisha utalii wa ndani Kitaifa na Kimataifa.

Asanteni,
Fredy Tony Njeje
Marketing and Public Relation Miss Utalii Tanzania.

No comments:

Post a Comment