Saturday, March 16, 2013

Ujumbe wa CCM waendelea na ziara yao nchini China


KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akimpa zawadi ya kinyago cha 'Ujamaa', Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Kamati Kuu jimbo la Sichuan, Zhang Ning, baada ya mazungumzo yao, Machi 15, 2013, katika hoteli ya Jinjiang, mjini Chendu, China. Kinana yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo.
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Kamati Kuu jimbo la Sichuan, Zhang Ning, baada , Machi 15, 2013, katika hoteli ya Jinjiang, mjini Chendu, China. Kinana yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo.
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akipewa zawadi ya picha na Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Kamati Kuu jimbo la Sichuan, Zhang Ning, baada ya mazungumzo yao, Machi 15, 2013, katika hoteli ya Jinjiang, mjini Chendu, China.
Baadhi ya viongozi wa CCM waliopo katika ujumbe wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakiwa ukumbini wakati wa mazungumzo ya Kinana alipokuwa akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Kamati Kuu jimbo la Sichuan, Zhang Ning, baada , Machi 14, 2013, katika hoteli ya Jinjiang, mjini Chendu, China. Kinana yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo.
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akitoka ukumbini na Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Kamati Kuu jimbo la Sichuan, Zhang Ning, baada ya mazungumzo yao, Machi 15, 2013, katika hoteli ya Jinjiang, mjini Chendu, China. Kinana yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na baadhi wa wajumbe walioko katika msafara wake, wakitazama baadhi ya bidhaa zinazouzwa, kwenye eneo la mji wa Kihistoria ya zaidi ya miaka 100 wa Jin Sha, mjini Chengdu, Machi 15, 2013. Kinana yupo nchini China na ujumbe huo kwa ajili ya ziara ya mafunzo.
Katibu wa Jumuia ya Wanawake Tanzania (UWT) Amina Makilagi (kulia) akicheza muziki na mmoja wa wasanii wa kundi linalotumbuiza kwa kupewa fedha yoyote na anayevutiwa, kwenye eneo la Mji wa Kihitoria ya zaidi ya miaka 100 wa Jin Sha, jijini Chengdu, China.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (aliyefunfa mikono kifuani), na baadhi ya wajumbe katika msafara wake, wakimtazama kwa makini kijana, Hu Qingzhong, aliyekuwa akichora katuni kwenye kompyuta kwa ajili ya kuwekwa kwenye simu za mkononi. Kinana na ujumbe wake walipotembelea kituo cha Wajasriamali wasomi cha Chengdu-High-Tech zone, jijini Chengdu, China, Machi 15, 2013. Kinana yupo nchini China na ujumbe huo kwa ajili ya ziara ya mafunzo.
Hu Qingzhong akichora katuni kwa ajili ya kuingizw kwenye simu ya mkononi, katika Kituo Cha Vijana wajasriamali wasomi cha Chengdu, Machi 15, 2013.(Picha na Bashir Nkoromo).

No comments:

Post a Comment