Mhe.
Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa akisaini kitabu cha wageni jana katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
wa Mbeya, wakati akiwa katika ziara ya siku mbili Mkoani humo.
Mhe.
Waziri Membe akifafanua kuhusu mgogoro wa Mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya
Tanzania na Malawi mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama chini ya
Uenyekiti wa Mhe. Abbas Kandoro, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoani Mbeya wakimsikiliza kwa makini Mhe. Waziri Membe (hayupo pichani).
Wilayani Kyela, Mbeya
Mkuu
wa Wilaya ya Kyela, Mhe. M. Malenga akimkaribisha Mhe. Waziri Membe (wa
pili kulia), wakati alipotembelea Ofisi yake jana Wilayani Kyela. Mhe.
Membe yupo Mkoani Mbeya kwenye ziara ya kikazi ya siku mbili, ambapo
anatarajiwa kutembelea maeneo ya ufukwe wa Ziwa Nyasa.
Wajumbe mbalimbali waliohudhuria Mkutano wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kyela (hayupo pichani).
Balozi
Irene Kasyanju (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria
katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Balozi Dkt.
Mohamed Maundi (kushoto), Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia - Kurasini
wakisikiliza maelezo ya Mhe. Malenga kuhusu Wilaya ya Kyela.
Safari ya kuelekea kwenye mpaka wa Mto Songwe
Mkuu
wa Wilaya ya Kyela akiuongoza msafara wa Waziri Membe kuelekea kwenye
mpaka wa Mto Songwe uliopo kati ya Tanzania na Malawi.
Mhe. Waziri Membe na msafara wake wakiwa wamesimama kwenye mpaka wa Mto Songwe.
Waziri
Membe akiangalia Mto Songwe, huku akitafakari mpaka kwa vile hapo
aliposimama kwa ufupi ni nchini Malawi ambapo wananchi wa pande zote
wanapishana kuendelea na shughuli zao za kawaida (angalia alama ya tundu
lililoko chini ya fensi - kulia).
Mhe.
Waziri Membe akiongea na Wajumbe wa msafara wake akiwemo Mkuu wa Mkoa
wa Mbeya, Mhe. Abbas Kandoro (mwenye shati jeupe mbele ya Waziri),
Balozi Irene Kasyanju (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Kitengo cha
Sheria kwenye Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na
Balozi Dkt. Mohamed Maundi (kushoto), Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia -
Kurasini. (Picha hii na Mbaraka Islam)
Makazi
ya wananchi wa Malawi kando ya Mto Songwe ambapo mmoja wa wananchi
anaonekana akifua nguo (pichani - upande wa kushoto; ng'ando ya mpaka
kwa upande wa Malawi) wakati wengine (kulia) wanaonekana wakiendelea na
shughuli zao za kawaida huku wakiwa tayari wamevuka ng'ando ya mpaka kwa
upande wa Tanzania. Picha, maelezo na Tagie Daisy Mwakawago
No comments:
Post a Comment