Wednesday, October 10, 2012

UZINDUZI RASMI WA ULAZAJI WA WAYA WA UMEME ZANZIBAR LEO


Na Ali Issa Maelezo Zanzibar   10/10/2012

Rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Zanzibar DR Ali Muhamed Sheni amesema kukamilika kwa  jitihada zakulaza waya mpya wa  umeme kutoka Fumba hadi Rasi kilomoni Darslamu wazanzibari wataondokana na tatizo la umeme wa mgao linalo endelea hivisasa.

Hayo ameyasema leo huko Fumba wakati wauzinduzi wa laini mpya ya umeme unao tarajiwa kumalizika disemba mwakahuu na kutoa huduma kwa wananchi wa Zanzibar ambao kwa muda mrefu wanatumia  nishati hiyo ya umeme wa mgao  .

Amesema  hali hiyo  itamalizika muda mfupi tu kwani umeme umnao lazwa waya wake  una megawati 100 ambao utatoshelza mahitaji ya wazanzibari bila ya wasiwasi wowote.

Amesema hali hiyo ni ya kufurahisha  kwa wazanzibari kwani itaifanya zanzibar kuendeleza shughuli zake za kimaendeleo na kuinua uchumi zaidi bila upungufu wa huduma hiyo .

“Waya uliopo una megawati 45 ambayo hii ni ndogo kwamatumizi ya  wananchi lakini kukamilika kwa waya huu mpya uta tosheleza mahitaji  ya watu na katika mazingira ya kawaida sirahisi umeme kukosekana ”ali sema DRsheni .

DR sheni ali wasihi wana nchi kuku bali kuupokea na kuitunza huduma hiyo kwa mashirikiano kuazia ngazi ya shehia Wilaya Mikoa na  Taifa kwa kuepuka kujenga ,kuchota mchanga na kadhalika karibú na nguzo za umeme .

Aidha Raisi huyo alishukuru serikali ya marekani kupitia shirikalake la changa moto za milenia (MCA compact) ,seriaki ya japan kampuni ya VISCAS kwamengenezo ya waya huo na kuulaza baharini.     

Waya huwo umegharimu zaidi ya milioni ishirini 28 za kimarekani wenyeurefu wa kilomita 36.5 una njia za mawasiliano 24 kupitia mshipi teknohama (febre optic),una uwezo wa kuishi miaka 40 ,utalazwa kwa gharama zaidi ya milioni 72 za kimarekani na serikali ya Mapindunzi ya Zanzíbar imechangia 1,465,625.00 za marekani kufidia mali za wananchi zilizo athiriwa katika eneo la utekelezaji .

No comments:

Post a Comment