Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisalimiana na mratibu wa mahusiano baina
ya Global Fund na Mabunge Duniani Ndg. Svend Robinson, walipokutana
kabla ya kuanza kwa mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU)
unaofanyika Mjini Quebec, Canada.
Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimtambulisha Mbunge wa Bunge la Afrika
Mashariki kutoka Tanzania Mhe. Dr. Perpetua Nderakindo Kessy kwa Balozi
wa Tanzania Chini Canada Mhe. Alex Massinda kabla ya kuanza kwa mkutano
wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika Mjini Quebec,
Canada.
Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda akifuatilia taarifa mbalimbali na maazimio
ya Mkutano wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) wakati wa ufunguzi wa
Mkutano wa 127 wa IPU Mjin Quebec, Canada. Kushoto kwake ni Balozi wa
Tanzania Chini Canada Mhe. Alex Massinda na Mhe. Hamad Rashid Mohamed.
Mkurugenzi
wa Maktaba na Utafiti wa Bunge Ndg. Kileo Nyambele anaye muwakilisha
katibu wa Bunge Dkt. Thomas kashilila akishiliki kikao cha makatibu wa
Mabunge yote wanachama wa Mabunge ya Dunia (IPU) katika Mkutano wa 127
wa chama hicho mjini Quebec, Canada. Kulia kwake ni Afisa dawati la IPU
kutoka Tanzania Ndg. James Warbarg.
Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiongoza ujumbe wa Tanzania kupiga kura
kuingiza agenda mojawapo kati ya agenda 5 za dharura zilizowasilishwa
kwa udharura katika mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU)
ili zijadiliwe pia. Tanzania iliungana na nchi za Afrika kupigia kura
agenda ya kujadili hali ya usalama katika nchi ya Mali pamoja na agenda
iliyowasilishwa na Uingereza kujadili kwa udharura swala la hatma ya
Usalama na Misaada wa Kibinadamu Nchini Syria na nchi Jirani. Kushoto
kwake ni Balozi wa Tanzania Chini Canada Mhe. Alex C. Massinda na Mhe.
Hamad Rashid Mohamed.
Spika
wa Bunge akitoka katika ukumbi wa Mikutano mara baada ya kumalizika kwa
kikao cha kwanza katika Mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani
(IPU) mjini Quebec, Canada. Kushoto kwake ni Mhe. David Kafulila
anayehudhuria Mkutano huo pia.
Mhe.
Anne Makinda akitoka katika Mkutano na Spika wa Bunge la Morocco Mhe.
Karim Ghellab kwa lengo la kufanya nae mazungumzo ya faragha kuimarisha
uhusiano baina ya mabunge ya Tanzania na Morroco.
Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisisitiza jambo wakati alipokutana na
Spika wa Bunge la Morocco Mhe Karim Ghellab kujadili namna bora ya
kuimarisha mahusiano baina ya mabunge ya nchi zao. Tanzania ilipeleka
ujumbe wa Wabunge kutoka kamati ya Mambo ya Nje, ulinzi na Usalama
kutembelea Bunge la Morocco Aprili mwaka huu ikiwa ni sehemu ya
kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizi mbili.
Spika wa Bunge la Morocco Mhe Karim Ghellab akimkabidhi Mhe. Spika zawadi mara baada ya kufanya nae Mazungumzo.
Ujumbe
kutoka Bunge la Tanzania katika Mkutano wa 127 wa IPU Mhe. Hamad Rashid
na Mhe. Suzan Lyimo wakifuatilia kwa makini mada kuhusu
“Multilateralism and the role of parliament in parliamentary diplomacy”
wakati wa mkutano huo Mjini Quebec, Canada.
Kazi nzuri Mwandumbya! Dropped you an email! Please check it inboxes!
ReplyDelete