Wednesday, October 10, 2012

Mkutano wa 22 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa PPF wafunguliwa leo Jijini Arusha

 Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 22 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa PPF,Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Saada Mkuya Salim akitoa hotuba yake wakati akifungua mkutano huo unaofanyika leo kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,jijini Arusha.
 Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka akizunguza machache na Wanachana na Wadau PPF wanaoshiriki kwenye Mkutano huo unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha leo hii.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mh. Magesa Mulongo akitoa salamu zake na kuwakaribisha Wanachana na Wadau wote wa PPF waliofika kwenye Mkutano huo na kutaka kutokuwa na mashaka yeyote kwani kila kitu kinakwenda sawa kabisa chini ya uongozi wake.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa PPF,Dk. Adolf Mkenda akitoa hotuba yake mapema leo asubuhi wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 22 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau PPF unaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF,William Erio akizungumza machache na kutoa utambulisho wa baadhi ya viongozi wakuu wa PPF wakati wa Mkutano wa 22 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau unaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha leo.
Mwenyekiti wa Wakuu wa Mashirika ya Hifadhi za Jamii nchini,Daudi Msangi akitoa shukrani kwa mgeni rasmi na kwa wadau wote kwa ujumla kwa kuitika kwao wito wa Mkutano huo.
Wakurugenzi wastaafu wa PPF,David Mataka (kulia) na Naftali Nsemwa wakifuatilia Mkutano huo.
Wakurugenzi wa Mashirika ya Hifadhi za Jamii nchi za Jirani,wakiongozwa na Bi. Magreth Osure (katikati) ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Mashirika ya Hifadhi za Jamii kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa PPF,William Erio wakifuatilia Hotuba ya Mgeni Rasmi kwa umakini.
Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 22 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa PPF,Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Saada Mkuya Salim akikabidhi tuzo na Cheti cha ushindi kwa Meneja wa Fidia na Faida wa Benki ya CRDB,Anamen Shangali Mosha baada ya Benki hiyo kushika nafasi ya Pili kwenye Kipengele cha Sekta ya Fedha.
Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 22 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa PPF,Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Saada Mkuya Salim akikabidhi tuzo na Cheti cha ushindi kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania,Rosemary Lulabuka baada ya kushika nafasi ya pili katika kipengele cha Elimu na Mafunzo.
Meneja wa CRB kanda ya Kaskazini,Evod Lyamuya akipokea tuzo na cheti kutoka kwa mgeni rasmi  baada ya kushika nafasi ya kwanye kwenye sekta ya Ujenzi.
Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka akipokea tuzo na cheti kwa niaba ya Dk. Shukuru Kawambwa ambaye amepata tuzo hiyo kwa kuwa mstari wa mbele kwenye malipo ya PPF.
Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 22 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa PPF,Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Saada Mkuya Salim akimabidhi tuzo kwa Mkurugenzi wa Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania,Julius Angelo (pili kulia).Benki Kuu ndio walioibuka washindi wa Jumla wa tuzo hizo.
Wafanyakazi wa Benki Kuu wakiwa kwenye Picha cha Pamoja na Uongozi mzima ulopo meza kuu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa PPF,Dk. Adolf Mkenda akielezea jambo wa Mgeni Rasmi wa Mkutano wa 22 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa PPF,Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Saada Mkuya Salim kabla ya kufunguliwa kwa Mkutano huo unaofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF,William Erio (kushoto) akitoa ufafanuzi wa jambo flani kwa Mgeni Rasmi wa  Mkutano wa 22 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa PPF,Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Saada Mkuya Salim kabla ya kufunguliwa kwa Mkutano huo wa Wanachana na Wadau PPF,unaofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha.Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa PPF,Dk. Adolf Mkenda.
MC anaeongoza Mkutano huo,Bw. Mavunde akiwajibika.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF,William Erio akizungumza machache na kutoa utambulisho wa baadhi ya viongozi wakuu wa PPF wakati wa Mkutano wa 22 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau unaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha leo.
Mkurugenzi wa Mfuko wa Jamii wa LAPF Eliud Sanga (kulia) na Mwenyekiti wa Wakuu wa Mashirika ya Hifadhi za Jamii nchini,Daudi Msangi wakiwa kwenye Mkutano huo.
Wadau wakiwa kwenye Mkutano huo.
Picha ya Pamoja na Wadau wa PPF.
Picha ya Pamoja na Wakurugenzi wa Mashirika Mbali mbali ya Hifadhi za Jamii.
Picha ya Pamoja na Wafanyakazi wa PPF.
Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 22 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa PPF,Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Saada Mkuya Salim akisalimiana na Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa PPF.

No comments:

Post a Comment