Kikosi cha timu ya Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa katika picha ya pamoja.
Kikosi cha timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Mechi ya
Kirafiki kati ya timu ya Umoja wa Mataifa (Blue) na timu ya Wizara ya
Mambo ya Nje (Nyeupe) katika UN Family Day ya maadhimisho ya wiki ya
Umoja wa mataifa kusheherekea miaka 67 ya Umoja huo zikimenyana kwenye
viwanja vya Leaders Club jijini Dar.
Austin
Makani wa UNHCR (mwenye koti la suti) akiwapa mzuka timu ya Umoja wa
Mataifa wakati wa mechi ya kirafiki kusheherekea maadhimisho ya wiki ya
Umoja wa Mataifa ya miaka 67 tangu kuzaliwa kwa shirika hilo.
Hoyce
Temu akibadilishana mawazo na baadhi ya wafanyakazi wenzake wakati wa
mechi kati ya Umoja wa Mataifa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Mataifa katika
kusheherekea miaka 67 tangu kuzaliwa kwake.
Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na Wa Wizara ya Mambo na familia zao wakifuatilia mechi hiyo.
Kiongozi
wa Benchi la Ufundi la timu ya Umoja wa Mataifa Siraji Ismail akiwa
mbinu timu yake wakati wa mapumziko ya kipindi cha kwanza.
Mchezaji
wa timu ya UN akiruka sarakasi baada ya kurudisha goli kwa timu ya
Wizara ya Mambo ya nje katika kipindi cha pili cha mchezo huo.
Kiungo
wa timu ya Umoja wa Mataifa akijaribu kumtoka kiungo wa timu ya Wizara
ya mambo ya nje wakati wa mechi ya kirafiki ambapo timu zote mbili
zilitoka sare ya Bao 1-1.
Baba na Familia yake.
Jacqueline Namfua wa UNICEF (Kushoto) akifurahi jambo na wafanyakazi wenzake.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou
(katikati) akibadilishana mawazo na baadhi ya Wakuu wa vitengo vya Umoja
wa Mataifa wakati wa UN Family day kusheherekea miaka 67 tangu kuzaliwa
kwa shirika hilo.
Watoto walipata fursa ya kucheza michezo mbalimbali kama inavyoonekana pichani.
Mchezo wa kushindana kuvuta kamba kati ya watoto wa kike na wakiume ambapo watoto wa kike waliwashinda wa kiume.
Wakuu
wa Vitengo mbalimbali vya Umoja wa Mataifa wakiongozwa na Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou (mwenye
kofia) wakishindana kuvuta kamba na Wakuu wa vitengo mbalimbali vya
Wizara ya mambo ya Nje ambapo UN iliibuka kidedea katika mchezo huo.
Wizara ya Mambo ya Nje walionekana kuwa wengi na wenye fya na kushindwa katika mchezo.
Pichani juu na chini ni Mchezo wa kushindana kukimbia na magunia kwa wakubwa na wadogo.
Pichani
Juu na Chini ni Familia za Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na Wizara ya
Mambo ya Nje katika UN Family Day iliyofanyika jijini Dar es Salaam
viwanja vya Leaders Club.
Mtaalamu
wa Mawasiliano wa UN Tanzania Sangita Khadka Bista (kushoto) na
mfanyakazi mwenzake wakingalia taswira mbalimbali kwenye kamera.
MC wa UN Familya Day Austin Makani wa UNHCR.
Kwaito ilichezeka vilivyo katika kusheherekea miaka 67 ya Umoja wa Mataifa tangu kuzaliwa kwa shirika hilo.
Twende kazi mwendo mdundo.... "Delivering as One".
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou
akisalimiana na baadhi ya wachezaji wa timu ya Wizara ya Mambo ya Nje
wakati wa kukabidhi Kombe.
Watoto wakikabidhi Kikombe kwa Kapteni wa timu ya Umoja wa Mataifa Laurean Kiiza kwa niaba ya Dkt. Alberic Kacou.
Kapteni wa timu ya Wizara ya Mambo ya Nje akipokea Kikombe kwa wote baada ya kutoka sare ya Bao 1-1 na timu ya UN.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou akipozi na Timu ya Wizara ya Mambo ya nje.
Dkt. Alberic Kacou na timu ya vijana wa Umoja wa Mataifa.
Makpteni wakipongezana.
Dkt.
Alberic Kacou akifurahi jambo na mfanyakazi wa shirika la kazi Tanzania
(ILO) Bw. Emmanuel katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es
Salaam.
Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akishangaa jambo na wafanyakazi wenzake.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou na Mwakalishi wa UNESCO Tanzania Bi. Vibeke Jensen.
Ulifika wa kati wa msosi na watoto walitangulia na baadae kufuatia wakubwa.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou akifurahi jambo na Familia ya Usia Nkhoma- Ledama.
Familia ya Hoyce Temu.
Dkt.
Alberic Kacou (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na UN Cares
Team Veronica, Beatrice pamoja na Rosemary wa UNHCR. UN Cares Team
walikuwa uwanjani hapo kwa ajili ya kupima Afya, kutoa ushauri nasaha
pamoja na elimu ya jinsi ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi
kwa familia na Wafanyakazi wa UN na Wizara ya Mambo ya Nje
walishiriki katika wiki ya umoja wa mataifa kusheherekea miaka 67 ya
kuzaliwa kwa shirika hilo.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou katika picha ya pamoja na Vijana wa YUNA.
Hoyce Temu akizungumza jambo na Vijana wa YUNA.
No comments:
Post a Comment