Monday, October 15, 2012

ALIYEKUWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA MAREHEMU BARLOW AAGWA NA MAELFU UWANJA WA MICHEZO NYAMAGANA LEO



Mwili wa aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza marehemu Liberatus Barlow ukiandaliwa kushushwa toka katika gari maalum lililoubeba mwili huo kutoka Hospitali ya rufaa Bugando kwenda nyumbani kwake kisha uwanja wa Nyamagana ambapo ibada ya kuuaga mwili huo imefanyika.


Askari wa vikosi maalum wakiulaki mwili wa aliyekuwa Kamanda wa jeshi la polisi Mwanza Liberatus Barlow.


Kwa mwendo wataratibu kikosi maalum kikiwa kimeubeba mwili wa marehemu Barlow kuupeleka mahala maalum pa ibada na heshima za mwisho kwa wakazi wa kanda ya ziwa.







Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo  alisema kuwa Kamanda Barlow alikuwa ni kiongozi wa mfano na alikuwa mhimili mkubwa katika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama kutokana na kutoa michango mbalimbali muhimu ya namna ya kudhibiti masuala ya uhalifu muda wote.


Makamanda wa jeshi la wananchi wakiwa wamesimama kusubiri hatua 


Eneo la jukwaa kuu viongozi mbalimbali ndani ya  uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza. 


Maelfu ya wananchi waliofurika kutoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa kamanda wao.

Akiongoza misa hiyo Paroko Raymond amesema kuwa tukio la kuuawa kwa kamanda wa polisi wa mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow linapashwa kulaaniwa na kuwataka waumini wa dini mbalimbali kuwaombea wale waliofanya tukio hilo ili watubu kwani wamefanya kitendo ambacho sio cha kiungwana.


Waziri wan chi ofisi ya waziri mkuu,Bunge, sera na uratibu William Lukuvi akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow, katika ibada maalum iliyofanyika uwanja wa Nyamagana.


Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo akitoa heshima kwa kamanda wa polisi mkoa wake marehemu Liberatus Barlow aliyeuawa majuzi na watu wasiojulikana.


Lawrance Masha ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa  (NEC - CCM)  wilaya ya Nyamagana akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza marehemu Liberatus Barlow.


Masista kutoka Parokia ya Nyakahoja wakitoa heshimazao za mwisho.


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Joseph Kasheku Musukuma akifuatiwa na mkuu wa wilaya ya Magu Jaquline Liana wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa kamanda wa polisi Mwanza Liberatus Barlow.


Mbunge wa viti maaalum (CCM) Maria Hewa akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza. 

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa (NEC - CCM) wilaya ya Tarime Christopher Gachuma akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow.


Mbunge wa Rolya Lameck Airo akiongoza wabunge wenzake kuuaga mwili wa marehemu aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mwanza Liberatus Barow.


Mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya uuzaji mafuta ya MOIL Altaf Hiran Mansoor 'Dogo' akitoa heshima zake za mwisho.


Maafisa wa jeshi la wananchi walipata fursa pia kutoa heshima zao.





Mfanyanyabiashara ambaye pia ni kada wa CCM kata ya Kirumba Jackson Robert (Jack Fish) akitoa heshima zake kwa mwili wa marehemu Kamanda Liberatus Barlow.


Maafisa wa jeshi la wananchi walipata fursa pia kutoa heshima zao.


Maafisa wa jeshi la wananchi walipata fursa pia kutoa heshima zao.


Mwili wa marehemu Barlow umesafirishwa  leo jioni kuelekea nyumbani kwake Ukonga jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuagwa na ndugu na jamaa zake kabla ya kusafirishwa kwenda kijijini kwake Koro wilaya ya Moshi vijijini kwa ajili ya mazishi. Picha zote na G. Sengo

BWANA AMETOA NA BWANA
AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE

No comments:

Post a Comment