Monday, October 1, 2012

Airtel kwa kushirikiana na Equity Benki yatoa mikopo kwa wafanyabiasha wadogowadogo



·         Zaidi ya wafanyabiashara (maarufu kama Machinga) 5000 kufaidika na mikopo hiyo

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Equity bank pamoja na Kampuni ya Ear promotion mwishoni mwa wiki hii imezindua mradi utakaowawezesha  wafanya biashara wadogo wadogo wa soko la machinga complex jijini Dar es saalam  kupata mikopo nafuu kwaajili ya kuendesha na kukuza biashara zao ambapo mikopo hiyo itatolewa na benki Equity kwa kupitia huduma ya Airtel money na wao kuwa wakifanya marejesho ya mikopo hiyo kwa kutumia Airtel money

Akizungumza wakati wa halfa ya uzinduzi wa mradi huo, Meneja uendeshaji wa benki ya Equity bw, David Mukaru  alisema” equity benki iko  mstari wa mbele kuisaidia  jamii katika huduma za kibenki ikiwemo mikopo ya riba nafuu hasa akina mama wa vikundi mbalimbali.

Benki yetu imekuwa sehemu ya maendeleo ya kukuza biashara na mtaji wa wafanyabiashara wadogo hadi wakubwa nchini. Leo kwa kushirikiana na Airtel kupitia huduma ya Airtel money tunawawezesha wafanyabiasha wa soko hili la machinga complex zaidi ya  efu tano kupata mikopo ya riba nafuu ambayo kwa hakika itakuza mitaji na kuwapatia ufanisi zaidi katika biashara zao”. 

Akiongea kwa niaba ya Airtel Meneja uhusiano wa Airtel bwn Jackson Mmbando alisema ”Airtel tunaendelea na mikakati yetu ya kusaidia jamii katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo kwa kupitia huduma  ya Airtel money, katika mradi hu Airtel tunarahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kupitia simu yako ya mkononi, tunawawezesha wafanyabiashara hawa kupokea na kufanya marejesho ya mikopo yao kwa kupitia huduma ya Airtel money”

“lengo letu  Airtel ni kurahisi uendeshaji wa mikopo hii,  kuhakikisha usalama wa fedha, na kupunguza usumbufu wa wafanyabiashara hawa kutembea umbali mrefu kufanya marejesho ya mikopo hii”.  aliongeza Mmbando.

Naye mwenyekiti wa wafanyabisahara wa soko la machinga complex bw. Abdubakar Rakesh alisema ”ninaishukuru  kampuni ya Airtel pamoja na Equity benki kwa kutufikia sisi wafanya biashara wadogowadogo kwa kupitia mradi huu wa mikopo nafuu. ni kwa muda mrefu wafanyabiashara wa soko la machinga complex wamekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kupata mikopo nafuu ambayo itawawezesha kukuza mitaji na kuweka bidhaa mbalimbali zitakazo wavutia wateja kufanya manunuzi katika soko hili, hivyo kwa kupitia mradi huu tunaamini tutafanikisha matarajio yetu ya kuwa na soko la kisasa lenye miundo mbinu na hadhi kwa wafanyabishara na wateja wetu.

Naye bw, Brian Kikoti Mkurugenzi wa Ear promotion Kampuni inayosimamia na kuratibu mradi huo amewasifu Equity Benki pamoja na Airtel kwa kuungana nao katika kusaidia kusimamia ufanisi wa soko hilo na la wafanyabiashara wadogowadogo.

Mbali na ushirikiano huu wa kibiashara na  Equity bank,  Airtel tayari inashirikiana na mashirika mbalimbali yakiwemo GEPF , LAPF, DAWASCO, TANESCO, USA EMBASSY, COCACOLA na mengine mengi katika kutoa huduma zao kupitia huduma ya Airtel money.

No comments:

Post a Comment