Tuesday, September 18, 2012

SERIKALI IMESHATUMIA ZAIDI YA BILIONI 34 KUKARABATI ENEO KATI YA STESHENI ZA KILOSA NA GULWE HADI SASA

Kwa muhtasari Dk Tizeba alisema umefika wakati wananchi wa Gulwe na hasa waishio kandokando ya reli ya kati kujiepusha na vitendo vyenye kuleta athari kwa reli ya kati na hasa eneo kati ya Kilosa na Gulwe ambapo kazi ya ukarabati wa eneo hilo tayari ,limeshaigharimu Serikali kiasi cha Shilingi 34 bilioni na kwamba kwa mwaka wa fedha 2012/13 zimepangwa kutumika Sh bilioni 20 zaidi.
Akatahadharisha kuwa endapo wananchi hawatochukua hatua za makusudi basi fedha hizo zinazokadiriwa kuwa Shs bilioni 55 zitakuwa zimepotea bure.

Mhe Tizeba am,wataka wakazi wa maeneo hayo kujiepusha na kuendesha kilimo hatarishi katika Milima Wota ambayo husababisha mmong’onyoko wa ardhi na kusababisha kuporomoka udongo, miti mkubwa na mafuriko katika reli ya kati. Alishauri kama ni lazima wananchi kuendesha shughuli za kilimo basi maafisa ugani watoe mafunzo ya mbinu za kilimo katika milima. Halikadhalika aliwataka wananchi wasilime ndani ya mita 30 za kila upande wa reli au kulingana na mazingira husika kwa vile baadhi ya sehemu zinatakiwa zilimwe nje ya mita 100 kulingana na mazingira ya eneo husika.

Aidha alisema hivi sasa kampuni ya Kichina mojawapo imepewa kandarasi ya kujenga bwawa la kwanza la kudhibiti maji yanayosababasisha mafuriko Katika eneo hilo na kwamba kihistoria eneo la kuanzia mikoa ya Manyara, Dodoma na Morogoro lilikuwa na mabwawa 5 yaliyotumika kudhibiti maji ya mvua yanayoingia katika mito kadhaa ya eneo hilo ikiwemo Mzaganza na Mkondoa. Alisisitiza hatua za serikali ili zifanikiwe ni lazima ushirikinao baina ya wananchi na Serikali za ngazi zote lazima uwe imara.

Aidha naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Rehema Nchimbi alisitiza kuwa matatizo ya mafuriko na uharibifu wa mazingira ambao hatimaye unaharibu njia ya reli yanatokana na vitendo vya binadamu hivyo wakati umefika kujirekebisha ili hatua za Serikali kugharamia ukarabati uwe na tija.

Halikadhalika naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Joel Bendera alitoa tahadhari kwa wananchi wanaolima au wamejenga ndani ya mita 30 za reli kila upande kuwa mkoa wake ukianza zoezi la zafias zafias hautokuwa na simile. Amewataka ili kuilinda reli ya kati kila mtu kwa nafasi yake ashikiri katika zoezi hili kikamilifu.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mpwapwa alitoa historia fupi ya eneo hilo na jinsi ya uharibifu wa mzingirta ulivyoahtiri njia ya reli na kwamba aliitaka Serikali ichukue uamzi mgumu wa kujenga mabwawa matano yalikuwepo siku za nyuma inakadiriwa bwana moja linagharimu takriban shilingi bilioni 5.
Naibu Waziri Uhcuikuzi Dk Tizeba hatimaye kama hitimisho la kuunga mkono ujenzi wa ofisi ya Serikali ya Kijiji alianzisha harambee ya papo kwa papo ambapo ilizaa matunda kwa kupatikana jumla ya shilingi 1,030,000/= ambazo alikabidhiwa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji Mzee Wilfred Madelemo ambaye aliwashukuru Viongozi na Taasisi zilizochangia harambee hiyo.
 Mhe Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Rehema  Nchimbi akitoa changamoto kwa wananchi wa  Gulwe kushiriki katika kuilinda reli ya kati na kuwataka wajiepushe na vitendo vyote vyenye kuleta athari dhidi ya  miundo mbinu ya reli.
 Viongozi  na Wanakijiji wa Gulwe wakiwasikiliza Naibu Waziri na Wakuu wa mikoa ya Morogoro na Dodoma kuhusu wito wa kujiepusha na vitendo vya uharibifu wa mazingira katika Milima ya Wota na kandokando ya tuta la reli ya kati.
 Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Gulwe Mzee Wilfred Madelemo akiheasabu mkwanja wa harambee ya papo kwa papo ya Dk Tizeba ambapo jumla ya Shilingi 1,030,000/= zilikusanywa kusaidia ujenzi wa Ofisi ya Serikali ya Kijiji Gulwe

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra  Alhaj Ahmad S.K.Kilima kulia  akiwatambulisha wageni kwa wananchi wa Gulwe 
 Picha ya pamoja ya msafara wa Naibu Waziri na Wakuu wa mikoa ya Morogoro na Dodoma na wasaidizi wao waandamizi mara ulipowasili katika Stesheni ya Gulwe kabla ya kufanya mazungumzo na wakazi wa Gulwe, ikiwa ni hitimisho la ziara ya ukaguzi 
 Naibu Waziri wa Uchukuzi  Dk Charles Tizeba akiweka saini katika kitabu cha wageni katika Stesheni ya Gulwe akishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Joel Bendera kulia , Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra  Alhaj Ahmad S.K.Kilima wa pili kushoto na Stesheni Masta wa Gulwe Nd. Hassan Idiru wa katikati  anayetabasamu.
  Mhe Joel Bendera Mkuu wa Mkoa wa Morogoro akimkaribisha  Naibu Waziri wa Uchukuzi  Dk Charles Tizeba ( wa tatu  kulia) wakati wa kupanda viberenge  umewadia, wa kwanza kulia ni Mhe Mustafa Nkullo Mbunge wa Kilosa
 Picha ya pamoja
 Mazungumzo stesheni ya Gulwe
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra  Alhaj Ahmad S.K.Kilima na Mhe Joel Bendera Mkuu wa Mkoa wa Morogoro wakiweka sahihi

No comments:

Post a Comment