Monday, September 3, 2012

Mpangilio wa mradi wa mji wa Kigambo wawa kivutio Mkutano wa Miji na Makazi

 Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda (kushoto) akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi. Maria H. Bidila, Bolozi wa Tanzania nchini Italia, Dkt. James Alex Msekela na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe. Goodluck Ole Medeye -  wakipeana msimamo wa kitaifa mara kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 6 wa miji na makazi ulimwenguni, mjini Napoli Italia leo. Zaidi ya nchi 150 zinatajia kudhuria mkutano huo.
 Samani hizi zinafaa kwa matumizi ya nyumbani na ofisini
 Baadhi ya Wajumbe wa Bunge la vijana katika mkutano huo wakiwa kwenye picha ya pamoja na Spika wa Tanzania
 Banda la maonesho la Tanzania katika ukumbi wa mkutano huo.
 pika Makinda akipokelewa na kukaribishwa na maafisa waandamizi wa Wizara ya Ardhi, Numba na Maendeleo ya Makazi katika banda hilo.
 Balozi Msekela na Spika Makinda wakipata maelezo ya ujenzi wa mji wa Kigambo ambao umekuwa moja ya kivutio kikubwa katika maonesho haya.
  Ramani za mji mpya wa Kigamboni katika picha
 Afisa Mratibu wa Shirka la Makazi la Umoja wa Mataifa akiwa katika wakati mgumu baada ya kutoa nyaraka zilizolichanganya jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na la nchi ya Kenya. Spika wa Bunge, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Balozi wa Tanzania nchi Italia kwa kauli moja wameuagiza uongozi wa shirika hilo kuomba radhi kwa maandishi (note verbale)na hadharani mara moja, jambo ambalo maafisa husika wamekubali kulitekeleza.
 Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Goodluck Ole Medeye (kati) pamoja na Bolozi wa Tanzania nchini Italia Dkt J. A. Msekela (kushoto) wakiwa na mazungungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa International Ecological Safety Cooperative Organization Profesa Jiang Mingjun alipolitembelea banda la Tanzania.

  Balozi Msekela na Mhe. Susan Lyimo mjini Napoli
Mkukutano unalega kuzungumzia matumizi rafiki ya mazingira. Hizi ni baadhi ya samani za maboxi/karatasi kwenye maonesho. Picha zaidi tembelea www.prince-minja.blogspot.com) (Na Prosper Minja-Bunge)

No comments:

Post a Comment