Tuesday, August 7, 2012

KAMPUNI YA STEPS YASHIRIKIANA NA WASANII KUWAKAMATA WEZI WA KAZI ZAO

MSANII MOHAMED NICE 'MTUNISI' AKIZUNGUMZA JINSI WALIVYOKAMATA MZIGO FEKI WA KAZI ZA WASANII MBALIMBALI KWA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA STEPS ENTATAINMET YA JIJINI DAR ES SALAAM INAYOSAMBAZA KAZI ZA WASANII NCHINI PICHA NA .www.burudan.blogsports.com
MTUHUMIWA WA KURUDUFU KAZI ZA WASANII AKIWA CHINI YA ULINZI BAADA YA KUKAMATWA
MSANII MOHAMED 'NICE' AKILIA KWA UCHUNGU BAADA YA KUKUTA KAZI ZAO ZILIZOKUWA ZIKIUZWA KATIKA MOJA YA DUKA MTAA WA MAGILA NA LIKOMA LEO


Msanii wa filamu nchini Mohamed Nice 'Mtunisi' kushoto na Jacob Stevin 'JB' wakiwa katika duka ambalo lilikuwa linauza kazi zao ambazo ni feki ambapo walikamatwa kwa kushilikiana na Kampuni ya usambazaji ya Steps Entantainment ya jijini Dar es salaam picha na  www.burudan.blogspot.com
Moja ya gari lililokuwa limejaa kazi za wasanii mbalimbali nchini zinazouzwa kiholera baada ya kurudufu kinyume na sheria na kukosesha wasanii mapato mazuri.Picha na www.burudan.blogspot.com

Baazi ya watu wakiwa wamezagaa kushudia ukamatwaji wa kazi za wasanii mtaa wa Magili na Likoma Dar es salaam leowww.burudan.blogspot.com

Baazi ya wasanii pamoja na askari polis wakiwa wamerizingira duka lililokuwa linauza kazi za wasanii fekiwww.burudan.blogspot.com
Gari lenye namba za T 608 BWD lililokamatwa na kazi mbalimbali za wasanii zikiwemo zinazosambazwa na Kampuni ya Steps ya jijini Dar es salaam linalofanya kazi na wasanii hawowww.burudan.blogspot.com
BAADHI YA KAZI FEKI ZA WASANII ZILIZOKAMATWA LEOwww.burudan.blogspot.com
MSANII MOHAMED NICE 'MTUNISI'  KUSHOTO AKITOA MAELEZO MBALIMBALI KWA MAOFISA USALAMA WALIOFIKA KATIKA UKAMATAJI WA KAZI FEKI ZA WASANII.www.burudan.blogsports.com

BAADHI YA WANANCHI WAKISHUDIA TUKIO HILO
MSANII KAPTEN RADO AKIKAGUA KAZI ZAKE MPYA AMBAPO KAZI YAKE MPYA IJULIKANAYO KAMA 'HATIHANI' ILIYOINGIA MTAANI LEO ILIKUWA IMESHA CHAKACHULIWA NA KUINGIZWA SOKONI .www.burudan.blogsports.com
MSANII WWA MZIKI WA TAARABU,MZEE YUSUFU KUSHOTO AKIANGALIA MOJA YA KAZI YAKE ILIYOKUWA FEKI ZILIZOKAMATWA NA WASANII WENYEWE KWA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA STEPS ENTANTAINMENT YA JIJINI DAR ES SALAAM.www.burudan.blogsports.com
WASANII MZEE YUSUFU KUSHOTO NA MOHAMED NICE WAKIWA KATIKA DUKA LILILOKAMATWA KWA KUUZA KAZI FEKI ZA WASANII MSAKO HUO ULIWASHILIKISHA KAMPUNI YA STEPS ENTATAINMENT PAMOJA NA WASANII WENYEWE.www.burudan.blogsports.com
BAADHI YA MIZIGO YA DVD MPYA KABISA ZILIZO FEKI ZIKIWA ZIMEKAMATWA LEO
KAMPUNI ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam inayosambaza kazi za wasanii kwa kushirikiana na wasanii wamekamata kazi mbalimbali za wasanii hawo zinazorudifiwa kinyume na taratibu na kutofaidika kwa wasanii wanaotoa kazi hizo

Msemaji wa Kampuni ya Steps  Kambarage Ignatios amesema kuwa ukamataji huo si wa zimamoto watahakikisha wanashilikiana na wasanii wenyewe kukamata kazi zao mana wasanii wengi wanadai kuwa kazi zao zinatoka sana kumbe zinachakachuliwa na kuwapa faida watu ambao wanakaa tu na kusubili kazi za wasanii ameiomba serekali kuchukua atua kali ili iwe fundisho kwa watu wanaorudufu na kunyonya kazi za wasanii hawo

Na mmoja ya wasanii waliojitokeza katika kamatakamata hiyo iliyofanyika makutano ya mtaa wa Magila na Likoma Kariakoo, Msanii Mohamedi Nice 'Mtunisi' amesema watu hawa wana akili za ziada kwani katika kava ya mbele wanaweka stika yetu halali na dvd ndio inakuwa imechakachuliwa akiangua kilio na kusema wasanii  wakifa wanakufa masikini kumbe ni watu wachache ndio wamekuwa wakinufaika na kazi zao bila kushiriki chochote

Baadhi ya wasanii walioshiliki katika kamata kamata hiyo ni pamoja na Jacobo Stevin 'JB' Mzee Yusuph wa kundi la Taarabu la Jahazi Simoni Mwapagata (Rado) Mussa Msuba wa iliyokuwa Segere Orginal Seles Mapunda ,Mohamed Nice 'Mtunisi' na wengine wengi wasanii hawo wameungana pamoja kwa ajili ya kutetea kazi zao ili zisirudufiwe kiolela na kuiomba serekali  kupitisha sheria kali kwa mtu anaekamatwa na kazi kama hizo zilizokamatwa

2 comments:

  1. athali, subili, mana, hawo, kiolela n.k manemo haya hayamo ktk lugha sanifu ya kiswahili.

    Pamoja na kukerwa na kiswahili cha blogger au wasanii wenyewe, hii ni habari mbaya sana ya watu kufaidika kwa njia haramu ya kudurufu kazi za wasanii.

    Napendekea sheria kali zipitishwe Bungeni na kukaziwa na Mahakama ila wizi huu wa kazi za wasanii ukomeshwe.

    Mdau
    Msafi

    ReplyDelete
  2. kuna watu wamemchomea jamaa nuksi sana hawa watu, mambo kibao mafisadi wanayafanya lakin mbona hawakamwatwi, wanakula nchi kama wamerisi kutoka kwa baba zao.
    ujinga mtuupu

    mdau kariakoo

    ReplyDelete