Wednesday, July 18, 2012

MATUKIO MBALIMBALI BAADA YA KUZAMA KWA MELI YA MV. STAR GATE ZANZIBAR LEO

-Raia wa kigeni waliookolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.
Abiria waliyookolewa kutoka katika meli iliozama ya Star Gate katika bahari ya Chumbe Zanzibar.
Abiria aliyookoka katika Meli iliozama ya Star Gate akifarijiwa na Jamaa zake Baada ya kuteremka katika Meli iliowaokoa hapo Bandarini.
Askari wa Vikosi mbalimbali wakiwa katika kazi ya Uokozi kwa Abiria waliokuwa katika Meli ya Star Gate ambayo iliozama katika ikiwa imebeba abiria 250 huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar.
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Hamad Masoud Hamad akiwa katika hali ya huzuni Baada ya kushiriki katika uokoaji na kuwaona Majeruhiwaliookolewa katika Meli iliozama ya Star Gate wakiteremka hapo Bandarini Zanzibar.
hali ilivyo bandari ya Zanzibar.
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Hamad Masoud Hamad akizungumza na waandishi wa habari.
Majeruhi wakipatiwa Mablangeti kwa ajili ya kujihifadhi baada ya kuokolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.
Baadhi ya wafanyakazi wa Huduma ya kwanza wakiwa kwenye Bandari ya Zanzibar tayari kwa kutoa msaada.Idara ya Habari (MAELEZO) Zanzibar

1 comment:

  1. MUNGU WETU NI MKUU SANA, NA MATENDO YAKE SIKU ZOTE NI MAKUU SANA, KILA KITU KIMEUMBWA NA YEYE, NAKUOMBA UWAPOKEE NDUGU ZETU MAREHEMU WALIOTANGULIA MBELE ZA HAKI JANA NA WASAMEHE DHAMBI ZAO NA UWAPOKEE KATIKA NURU YAKO, WAPE NGUVU NDUGU ZETU AMBAO WAMEOKOLEWA WAPE AMANI MIOYONI NA WASAIDIE KUSAHAU TENDO HILO GUMU NA KUBWA SANA. EE BABA NAKUOMBA UWASAIDIE WALE WENGINE AMBAO BADO HAJAFIKIWA NA WAOKOAJI ILI NAO WAWEZE KUPATA UOKOZI HUO, BABA WASAIDIE. TENDO LA KIFO NI MOJA KATI YA MATENDO YAKO MAKUBWA NA MAKUU SANA. TUNAOMBA FARAJA MUNGU WETU.

    ReplyDelete