Tuesday, July 31, 2012

HOJA YA HAJA: MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII (Social security funds)


UTANGULIZI
Kwa mujibu wa Shirika la Kazi Duniani, Mfuko wa hifadhi ya jamii ni mfumo ambao jamii husika imejiwekea kwa lengo la kuwakinga watumishi wa umma au binafsi (waajiriwa) dhidi ya matukio yasiyotarajiwa (Contingencies). Matukio hayo ni kama maradhi, ulemavu, kupoteza kazi, kuacha kazi kwa sababu ya uzee (kustaafu) aidha kwa hiari au kwa lazima, na mengineyo ikiwamo huduma za matibabu, ghalama za msiba ikiwa mteja atafariki au kufiwa na mtu ambaye mfuko husika huchangia. Vile vile iwapo mteja atafariki kabla ya kustaafu basi mafao yake hulipwa kwa warithi wake ambavyo huweza kusaidia kusomesha watoto wa mhusika.  
Hifadhi kutoka kwa jamii ni haki ya kila mtu kama ilivyotajwa na katiba ya jamhuri ya Muungao wa Tanzania, 1977 (kama ilivyofanyiwa marekebisho mara kwa mara) katika ibara ya 11, ibara ndogo ya (1) kwamba:
“Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu unaofaa kwa ajili ya kufanikisha utekerezaji wa haki ya mtu kufanya kazi, haki  ya kupata elimu na haki  ya kupata msaada kutoka kwa jamii wakati wa uzee, maradhi au hali ya ulemavu, na katika hali nyinginezo za mtu kuwa hajiwezi...”
Hivyo hivyo, ndivyo inavyotaja ibara ya 22 ya Tamko la Ulimwengu la haki za Binadamu la mwaka 1948, ambayo pia inataja kuwa ni haki kwa kila mtu kupata hifadhi ya kijamii kupitia utaratibu uliowekwa.
KWA NINI KUNA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII
Kutokana na hali ya maisha kutotabilika, wafanyakazi wengi hujikuta wakiishi maisha magumu mara baada ya kumaliza muda wao wa utumishi (kustaafu). Lakini pia hata kabla ya kustaafu, wafanyakazi hujikuta wakipitia hali ngumu za maisha kutokana na maradhi au ulemavu ambavyo huweza kusababisha kupungukiwa au kukosa kabisa kipato hivyo kushindwa kumudu ghalama za matibabu na za kimaisha kwa ujumla. Hiki ndicho kipindi ambacho umuhimu wa Mifuko ya hifadhi ya jamii huja, kwani baada ya kuridhika kuwa mteja anastahiri huduma kutoka kwenye mfuko husika, huweza kupatiwa ghalama za matibabu na matunzo kutoka katika mfuko huo kulingana na taratibu zilizowekwa. Ila inatakiwa iwe imetajwa kuwa mfuko husika hutoa huduma husika na mteja amekidhi sifa za kupata huduma hiyo (pensionable fund) kwa maana ya kutabulika kama mteja na kuchangia kwa utaratibu uliowekwa.
WAKATI AMBAO MTU ANAWEZA KUPATA MAFAO YAKE AU HUDUMA KUTOKA KWENYE MFUKO HUSIKA
Ifahamike kuwa mifuko ya hifadhi ya jamii ni maalum kwa ajili ya kumsaidia mfanyakazi  kumudu mahitaji yake ya uzeeni pindi anapostaafu kama si mahitaji mengine yaliyotajwa hapo mwanzo.  Sababu kubwa iliyopelekea kuwepo kwa mifuko wa hifadhi ya jamii ni baada ya kubainika kuwa wakati wa ujana, wafanyakazi wengi hushindwa kujiwekea akiba ya kutosha kukidhi mahitaji yao ya uzeeni au kumudu ghalama za maisha yao pindi itokeapo hali yoyote ya kutojiweza.
Tofauti na benki au taasisi nyingine za kifedha, mifuko ya hifadhi ya jamii hutoa mafao kwa mteja wake pindi awapo na uhitaji wa kidharula (mfano: Maradhi, ulemavu au hali nyingine ya kutojiweza ), au kustaafu kazi kwa misingi ya uzee kwa mujibu wa sera za kazi na utumishi na si vinginevyo. Kwa mantiki hiyo mteja wa mfuko husika hawezi kudai mafao yake kwa misingi yoyote ile tofauti na ile iliyowekwa na mfuko husika (mfano: kuhitaji pesa kwa ajili ya kuanzisha biashara, kununua vyombo vya starehe kama gari, pikipiki na vinginevyo) kama kustaafu kazi au kupoteza kazi. Kwa hiyo bila uhitaji wa namna hiyo mteja hawezi kulipwa mafao yake ya aina yoyote ile mpaka pale atakapofikia umri wa kustaafu aidha kwa hiari au kwa lazima ambao kwa Tanzania ni miaka 55 hadi 60, mtawalia*.
Mifuko ya ifadhi ya jamii ni kama ilivyo sera ya bima yaani mtu hulipwa pale anapopatwa na janga, na ni mahususi kumsaidia mfanyakazi kununua vitu vya thamani kama vile viwanja au kujenga nyumba anapostaafu au anapoelekea kustaafu. Kwa hiyo, hiyo ndiyo maana halisi na lengo la mifuko ya hifadhi ya jamii.
Kabla ya kuhitimisha makala hii, tukizungumzia kidogo kuhusu pensheni ambayo hujulikana kama (Kiinua mgongo), ni kiasi cha pesa ambacho  hulipwa na serikali au kampuni binafsi kwa mtu ambaye ameacha kufanya kazi kwa sababu ya uzee au maradhi. Kwa maana hiyo mtu hawezi kupata pensheni mpaka ule umri wa kustaafu ambao umewekwa na serikali (miaka 60). Ieleweke na ndivyo ilivyo, ya kwamba mtu hawezi kupewa pensheni  katika umri wowote tofauti na umri uliotajwa kuwa ni umri wa kustaafu kwa lengo la kufanya biashara au kwa ajili ya lengo jingine lolote lile. Hii ni kwa sababu hela ya mteja husika hutumika kuanzisha vitega uchumi na taasisi husika na ndio maana mteja hupata mafao manono zaidi kuliko alivyochangia. Hii ni kama alivyo wahi kusema Mheshimiwa Irene Isiaaka  ambaye ni mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya udhiti wa mifuko ya hifadhi ya jamii (SSRA), kuzitaka taasisi za mifuko ya hifadhi ya jamii kubuni miradi endelevu na kuanzisha vitega uchumi mbalimbali ili kuziwezesha taasisi hizo kutoa huduma bora kwa wateja wake. Hii ndio sababu kubwa ambayo huipasa mifuko ya hifadhi ya jamii kukaa na pesa za wateja wake kwa mda mrefu zaidi ili kuwa na uhakika wa mafao bora wakati ambapo mteja huacha  kuchangia kwa sababu ya kuacha kulipwa mshahara na badala yake kuanza kulipwa mafao yake na mfuko husika kutokana na uzalishaji wa hela yake.
Ni muhimu kutoa pongezi kwa mamalaka ya udhibiti wa mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kutoa nafasi kwa wafanyakazi wanaokaribia kustaafu kupata sehemu ya pensheni zao kupitia sheria iliyopitishwa na bunge mwezi April mwaka 2012. Nafasi hiyo itawapa watumishi wa umma uwezo wa kujiandalia mazingira mazuri ya kustaafu ikiwa ni pamoja na kukununua viwanja, kujenga nyumba bora za kuishi na kusomesha watoto wao.
Napenda pia kuonesha kusikitishwa kwangu na watu wanaobeza  hatua hiyo iliyofikiwa na mamlaka ya udhibiti wa mifuko wa hifadhi ya jamii, huku wakidai ya kuwa umri wa miaka 55 hadi 60 ni mkubwa na kuwa una dalili za kibaguzi hivyo kuwa kinyume na haki za binadamu. Naweza kusema ya kuwa ni kuhoji mambo tusiyoyafahamu yanaendaje napengine kuigiza siasa hata kwenye mambo ambayo si ya kisiasa ambavyo ni hatari kwa maendeleo ya jamii yetu. Zaidi natambua kuwa wamo wanasheria na mashirika ya kutetea haki za binadamu wanaopanga kuzuia sheria hiyo kwa kigezo cha umri wa pensheni kuwa mkubwa. Ningependa kuwakumbusha kwamba penshion siyo mshahara, siyo mkopo na wala sio kama pesa iliyowekwa benki kwamba mtu anaweza kuidai pindi anapojisikia, kufanya hivyo ni kopotosha maana halisi ya dhana ya pensheni ambayo hata kamusi zote zinalitaja kuwa ni mafao ya uzeeni baada ya kuacha kazi, kupatwa na maradhi au kupata kilema kiasi cha kushindwa kuendelea na kazi ambazo ndio sifa za mtu kupata pensheni (pensionable) na si vinginevyo.
Ushauri wangu ni kwamba kama kuna mtu anahisi kuwa umri uliowekwa kwa mtu kupata pensheni ni mkubwa aombe serikali kubadili sera ya umri wa kustaafu na si kubadili maana ya pensheni kuwa kama mishaara au mifuko ya hifadhi ya jamii kuwa kama benki. Ijulikane kuwa ndio maana kuna benki na kuna mifuko ya hifadhi ya jamii.
 HITIMISHO
Ni muhimu tukielewa kuwa kulalamika pale tunapohisi kuwa haututendewi haki ni haki ya kila mmoja wetu kama watanzania. Lakini ni muhimu kuelewa na hata kutafuta kuelewa jambo ambalo hatulielewi vizuri. Hii itatusaidia kujikosoa pale tunapojikuta kuwa jinsi tulivyoelewa jambo ni tofauti na uhalisia wa jambo husika na si kukimbilia kulalamika kwa ushabiki wa kisiasa kwa mambo yasiyostaili kuingiziwa siasa. Mamlaka za mifuko ya hifadhi ya jamii ziandae elimu maalum kwa ajili ya wadau wake ili kuwawezesha kufahamu mfumo na jinsi mifuko hiyo ya hifadhi ya jamii invyofanya kazi. Hii itaondoa malalamiko yasiyo ya lazima kutokana na kutofahamu jinsi mifuko hii inavyotoa huduma zake.
Natanguliza shukrani
*Mtawalia: maana yake- Respectively- a kufuatana katika mpangilio
Davis Muzahula,
Mwanafunzi wa shahada ya kwanza ya sheria (mwaka wa nne),
Chuo Kikuu Cha Mtakatifu Augustino cha Tanzania
Simu: +255756829416
Barua pepe: davismuzahula@yahoo.com

18 comments:

  1. Ndg yangu nafurahi kwanza kabisa kwa maoni au maana halisi ya mifuko hii ya jamii. Napongeza kwa jitihada zako za kutoa maana halisi ya neno hilo.

    Wasi wasi wangu sio wetu bali wangu mimi. Watanzania wengi wapo kazini miguu nje na ndani je anapofukuzwa kazi maana hakuna sheria zinazowalinda wafanyakazi pindi wanapodai maslahi yao na haki zao za msingi, pindi wafanyapo hivyo hufukuzwa na kukosa kazi je niambia pindi anapokuwa nje ya ajira atakula nini? kama mifuko hii ingetamka bayana pindi mtu anapokuwa hana kazi basi atapata fedha ya kujikim hadi atakapopata tena hapo ningeelewa somo lako vinginevyo naomba serikali isitumie sheria dhaifu kuwakandamiza raia wake. kuna wazee wa east afrika hadi leo hawapati kitu na wanataabika kweli kweli je ingekuwa mifuko hii ina nia nzuri tungeona maisha ya watu hawa wanaishi kwa matumaini. penye ukweli sema ukweli na palipo na utapeli sema ili kuokoa jamii kubwa. inaweza kuwa sheria zipo lkn hazitekelezwi sasa kwa nini tuendelee kuumia kwa uzembe wa watu? kumbuka hizi pesa ni mali yangu kihalali sio za kufoji wala kuiba inakuwaje leo nipangiwe tena kwa masharti magumu? miaka 55 ni mingi sana ndg yangu hata hivyo wangepitisha white paper tujadili wadau sio kupangiwa na watu yamkini waliokubali sheria hii ni wale wasiochangia kama wewe maan wewe ni mwanafunzi hujui uchungu wo wote wa hizi fedha. tunateseka sana kuzipata leo natolewa kazini naambia hadi nifikishe miaka 55 nikiugua nitafanyaje kwetu umatumbini? acha ukandamizaji tuhurumiane wote mungu ametupa neema ya kuishi tusichuliana haki zetu> asante sana
    chris

    ReplyDelete
  2. Duh,ama kweli.Pongezi kwa kukaa na kutueleza maana halisi na kujitahidi kutetea uozo wa System Nzima ya Social Security ya Tanzania Yetu.

    Nafurahi kupata nafasi hii na mimi kutoa duku duku langu.Hii mifuko yote ya Jamii hapa Tanzania kusema ule ukweli ni mifuko ambayo ipo kwa miongozo ya Kikatiba na Kisera za yetu Tanzania.Tatizo hapa si umri wa kustaafu wala si kuchukua au kutochukua hayo mafao.Tatizo la mifuko hii imekuwa ikitumika na viongozi na marafiki zao kukopeshana bila kulipia riba na pia kingine hii mifuko kuwa na miradi isiyokuwa na tija-eg.Machinga Complex,UDOM Hostels,Mabibo Hostels,mradi wa nyumba za KInyerezi Segerea na mingine mingi kama hiyo na sasa mradi mkubwa wa Daraja la Kigamboni.Hii inamaana kuwa kama mfuko mmoja unaweza kuigharamia miradi yote hii kwa fedha za wanachama inamaana kuwa mfuko huo una kila uwezo wa kuwahudumia au kuboresha huduma za mafao yake kwa wanachama na kila mwanachama au asiye mwanachama wakawa na hamu ya kuendelea kuwa wanachama hata kama ajira ikikoma au hata akiwa mjasiliamali.Tatizo hapa ni kuweka pesa zetu kwenye hiyo mifuko halafu inatumika kienyeji bila hata kuwa na faida hata ya senti moja katika kila miradi wanayoisimamia wakati pesa zilizotumika katika kugharamia miradi hiyo ni pesa ya mwanachama ambaye sipati hata gawiwo inalotokana na faida katika miradi hiyo.Achilia kupata gawiwo basi hata hizo nyumba za Kinyerezi ingefaa tutangaziwe kwanza wanachama kama utapenda kukopeshwa hizo nyumba halafu dhamana iwe pesa niliyoiweka katika huo mfuko lakini mambo yakaenda kienyeji.Nyumba zile zikauzwa hata mwanachama mmoja kupata nyumba zile.Halafu unashaangaa eti saa hizi serikali inakuja na maelezo maarefu pamoja na wewe kibaraka unatuambia hapa kuwa eti maana ya mifuko ya jamii ni nanihiiii.... tupa kule walikuwa wapi siku zote hizo mpaka mwaka huu wanakuja na hiyo sheria mpya ya mifuko ya jamii baada ya kuona kuwa inafilisika.Na hili suala linataka kufanana na la MAREKANI kwani mtikisiko wa uchumi ulitokana na nini ni mifumo ya mifuko ya jamii na mashirika ya Insurance
    kushindwa kulipa mahitaji ya wateja wao katika mikopo ya nyumba na mambo mengine mengi.Sasa na hapa kwetu naona hilo linataka kutokea wameamua kuongeza muda wa kuchukua mafao ili waweze kupata muda wa kutunisha hiyo mifuko kifedha ili wawe na muda mzuri wa kutumia hizo fedha kwa matumizi yao binafsi badala ya serikali kujitahidi kuziba mianya ya walanguzi wasiolipa kodi kwenye migodi,bandarini,viwandani na kwa wafanyabishara wakubwa unakuja kuwanyanyasa wafanyakazi kundi ambalo piga ua ni lazima lilipe kodi na pia lazima achangie hiyo pesa ya mfuko wa jamii.
    Sasa kwa wale woote ambao hawachangii kipato chochote kwenye hii mifuko kama wewe MWANAFUNZI WA SHERIA TUNAOMBA USIJE NA HIZO MADA ZENU ZA AJABU HAPA.HAPA HAKUNA KUKUBALI WALA KUKAA ETI KIINUA MGONGO MPAKA 55 - 60.HAYO MAELEZO YAKO NA MAANA YA MIFUKO YA JAMII MIMI BINAFSI SIONI CHA MAANA HAPA TUPEWE CHETU THEN HAYO MAMBO MENGINE YAJE BAADAE.KWA KWELI WAFANYAKAZI WOTE NITASHANGAA SANA TUKIKAA KIMYA NA KUACHA SHERIA HII ITAWALE.

    ReplyDelete
  3. umejalibu kueleza ni jinsi gani unaelewa kuhusu hiyo mifuko,sawa na hongera kwa maelezo<lakini turudi kwenye umuhimu wa mfuko na sheria hizo je zimewekwa kwa maslahi ya nani,na zinataka kumnufaisha nani,kikubwa mifuko ingebuni miradi endelevu yenye uipatia fedha za kutosha kuliko kukimbilia majengo ambayo zinajenga kwa kasi bila kuwa na wapangaji,mifuko iwekeze kwenye miradi yenye kunufaisha wenye kuchangia mifuko.tujiulize daraja la kigamboni lina mchango gani kwa wenye kuifadhi hela zao

    ReplyDelete
  4. ndugu mtoa mada hongera kwa maelezo yako,mimi ni mwanafunzi lakini tunaona jinsi wazazi wetu wanavyopata shida kuzipata hizo fedha hayo mashirika hayana mfumo mzuri wa kuzitoa hizo fedha yaani mtu asipozifuatilia hizo fedha ndio imekula kwake, mbona wakati wa kuziweka hawasumbuliwi?wakitaka hivyo wanavyotaka kufanya waboreshe kwanza huduma zao ndio waongee kitu kama hiko ndugu mtao maada unadhani kama hizo hela zingekuwa na mfumo mzuri wa kutolewa uzeeni kwani watu wangelalamika?hivi unajua kwamba watu wamechoka na maneno?watu wanataka vitendo ndio waamini>asante

    ReplyDelete
  5. Kwa hakika kama kueleza maana halisi ya mifuko ya jamii umeeleza. Ni jambo la kushangaza sana kwamba hao wanaodai kuwa ni watanzania wenzetu wanabuni vitu vya hovyo kabisa ambavyo havimsaidii mtanzania bali kumkandamiza,siku zote tunahimizwa kujiajiri, ama kuwa wajasiriamali na nijuavyo mimi tulio wengi hatuna mitaji ya kujiajiri lakini tunaimani kwamba siku ajira ikikoma kwa namna moja au nyingine basi hivyo vijisenti vyetu vya akiba vitatusaidia kujiajiri si lazima kuajiriwa tena. sasa mnaposema miaka 55 mnategemea katika kipindi cha kuisubiri hiyo miaka tunaishije?, Tangiapo nimuunge mkono mchangiaji aliyetangulia kwamba " kwanini tupangiwe masharti tena magumu ili hali fedha ni yetu kihalali"?????.

    ReplyDelete
  6. Ni kweli ni nvyema kujiwekea akiba itayokusaidia pindi upatwapo na majanga, kukosa kazi ama kufikwa na uzee. Namana ulivyoandika mada yako inaonyesha wewe si mwanafunzi makini. unaongea hoja zako kwa kuangalia upande mmoja tu...na hivyo inanilazimu kuamini wewe ni mmoja wa hao SSRA na umetumwa kupotosha watu. Hujui tunavyoumia kufanya kazi hasa kwenye sector binafsi. Nakushangaa hadi hivi leo mwanafunzi wa sheria mwaka wa nne unaita kununua gari ni starehe!!! Are you serious? nani aliku-brainwash ndugu yangu? Kwako wewe kujenga nyumba na kununua viwanja are the only two things vinanyotambulika kuwa muhimu? Acha ndugu kupotosha umma, hili jambo ni zito na muhimu sana. SSRA walipaswa kutuuliza sis tunataka vp na tukajadili wote. Kwa mfano kwenye sector binafsi hasa sehemu hatarishi, mishahara waweza kuwa mzuri na mtu kuamua kufanya kazi kwa malengo, unakuta mtu anafanya kazi kwa malengo, miaka 7 hadi 10 tayari ashachangia million 30 hata 40, anahitaji kuzipata hizo nae awe bosi na kuajili watu...sasa bado unataka kusubiri miaka 55/60? kweli? au unataka afe ili mje kunyanyasa familia yake na huenda msiwape chochote? Endeleeni tuu...kwa imani yangu naamini kila mtu ataonja mauti na baada ya hapo ni hukumu, endeleeni kutunyanyasa na kutuibia, moto unawangojea. Hili swala ni zito sana acha mzaha ndugu na mwambie aliekutuma HATUTAKI KUIBIWA.

    ReplyDelete
  7. ni vizuri kuona kuwa mwandishi wa makala amejaribu kueleza ukweli na hakika ya mifuko ya jamii kwa mujibu wa malengo ya kuanzishwa na kuasisiwa kwa pamoja na kazi au jukumu linalotakiwa kutekelezwa ni mifuko hiyo.
    ni maelezo maelezo mazuri ambayo ambaye hajaelewa, basi hataki kuelewa tu na wala sio kuwa hayaeleweki. Nilichokiona cha ziada ni kuwa maelezo yako yamegusia na yamejiegesha kwenye misingi ya kisheria na kanuni za uanzishwaji na uendeshwaji wa mifuko husika. Hakuna awezae kupinga hakika hiyo.
    Suala moja ambalo nahisi ni muhimu tunapofanya uchambuzi wa mambo kama haya lazima pamoja na maelezo mazuri ya usuli wa jambo, tunatakiwa tuitizame hali halisi ya kijamii na kiuchumi ya hao wanufaika (beneficiaries) wa mifuko hiyo badala ya kujikita kwenye misingi ya kisheria na kisiasa pekee.
    1. Je ni kweli wanatambua ukweli huu?
    2. Je ni kweli kuwa uendeshaji wa mifuko hii unakidhi mahitaji ya wahusika wakati wa uhitaji?
    3. Je tunajua mfanyakazi wa Kitanzania anawafanyia kazi watanzania wangapi? Mf. anafanya kazi kwa ajili yake, mumewe/mkewe, watoto wake au na wazazi wake au na kaka na dada zake au na shangazi na wajomba wake n.k kwa vyovyote utakavoamua kuwa mkweli wa maisha halisi ya mfanyakazi na maana ya famila kwa mtanzania.
    4. Je ni wafanyakazi wangapi ambao wanafikisha miaka 55 na 60 kwa nchi yetu ili wanufaike na mafao hayo? Hakuna takwimu zozote zioneshazo kuwa umri wa kuishi (life expectancy) ya Tanzania 55!! Zote za ndani, za serikali, za NGO, za ILO zote zaonesha wastani wa umri wa kuishi ni chini ya miaka 55. Ni wachache sana watakaofikisha miaka 55 hasa wale wa ngazi za juu na vyeo vikubwa.
    Naomba tuwe wakweli na wenye kufikiria kwa niaba ya wengine.

    ReplyDelete
  8. Ndugu yangu, pamoja na mawazo yako mazuri kwenye suala zima la mifuko ya pensheni, naomaba nikwambie yafuatayo:

    1. Hali ya uchumi ya Tanzania haijaiva kufuata uelekezi uliowekwa na mifuko ya hifadhi ya jamii dunianni ambako sisi tunacopy kila kitu na kubadili jina la nchi.

    2.Kwa taarifa tu, kibiashara ni afadhali kwa upande wa mifuko hiyo iwaqpo mfanyakazi atachukua mafao yake wakati wowote kuliko kusubiri mpaka uzeeni kwani ukishachukua mafao yako (akiba) mfuko haundelei kukulipa, ukishafikia level ya pensheni inamaana mfuko utaendelea kkukulipa mpaka ufe (kimsingi malipo inabidi yaendane na mfumuko wa bei). kwa elimu yako uliyokwisha pata piga hesabu uniambie wewe kama mkurugenzi wa mfuko ungependelea scenario ipi?

    3. Nimeshindwa kuelewa ni kwa nini unajikanganya kwani maelezo yako ya tafsiri za mifuko ya pensheni na manufaa yake haiendani na sifa unazoipa mamlaka ya kusimamia mifuko hiyo, kwa mfano kama akiba yangu itasubiri nifike miaka 55, je nikiumwa, nikipaata ulemavu wa kudumu nisubiri miaka 55 kulipwa? Kama mwanasheria mtarajiwa ninatumaini umeisoma sheria mpya, hakuna hizo provisions.

    4. Je haikutii shaka kama mwanasheria kuona sheria kama hiyo inayohusu suala la mtambuka (cross cutting issues) inatolewa bila guidelines na regulations? Kwa taaluma yako huoni hiyo ni hatari kwa usalama na imani ya wananchi baadae?

    4. Mwisho, ndugu yangu ingia kwenye soko la ajira kwanza kabla ya kutumia nadharia wakati reality on the ground huijui, na kama umewahi kuajiriwa ninasikia hofu kubwa kwa wewe kuwa na mtazamo huo wa sheria ya hifadhi ya jamii kwani ni wazi hukuelewa situation ya ajira on the ground.

    ReplyDelete
  9. Wakala nini!ishia huko huko na utawaliwa wako!!

    ReplyDelete
  10. Nashukuru sana mtoa hoja ya haja. Nusura nilainike kwa maelezo yako lakini ulivyohiyimisha tu nikashtuka. Mimi naona nia na madhumuni ya sheria ya kuanzishwa kwa mifuko hii ni nzuri ili tusipoteze nguvu kazi mapema kwa sababu ya "frustrations" za kustaafu . Lakini hatuoni kuwa kuna haja ya kumuokoa huyu mfanya kazi ambaye kafukuzwa kazi na yuko mtaani na watoto wanasoma na hana nyumba!!! ina maana sifa za kuokoa mtu huyu katika jukumu la kusomesha na kujenga nyumba mpaka awe amefikia karibu ya kufa???? tafsiri za dictionary zisitutishe sana maana tumeziandika wenyewe (Kinyago umekichonga mwenyewe halafu kinakutisha-Mzee Yusuph). Malamiko haya usiyashangae ndiyo yatakayobadilisha tafsiri ya pensheni. Wewe kwa sababu ni mwanafunzi na hapo unajua ukibadilisha chochote lazima utafeli na hutapata degree yako hivyo lazima uyaache kama yalivyo ni tofauti na mfanya kazi ambaye "keshaingia ndani ya ngoma" sasa ndio anajua mshindo wake. Bwana elimu yako uliyotoa hapa ni ya muhimu kujua maana ya mifuko hii lakini haiwafungi wananchi kulalamika maana sheria zinabadilishwa kila siku baada ya kupitwa na wakati. Na ndio maana sasa tuna tume ya warioba inafanyia kazi mambo hayo. Utasema ohhh shirika la kazi duniadi limesema...limesema...!! shirika la kazi duniani ndio sisi, tuna wawakilishi huko watasema watanzania wanasemaje kuhusu mifuko hii. Namalizia kwa kusema kuwa mifuko ni ya muhimu lakini wigo wa vigezo upanuliwe kulingana na washika dau watakavyopendekeza. Kuomba pesa yako uliyokatwa kwenye mshahara wako sio jinai. Ni suala linalojadilika. Kwa kumalizia , wafanya kazi wasishinikizwe kujiunga na mifuko hii, na hili litasaidia kupunguza malalamiko maana mtu atakuwa amejiunga huku akiwa anajua vema sheria na taratibu za mifuko husika.

    ReplyDelete
  11. naona huyu mwanafunz anadhan hapa yupo kwenye chumba cha mthan na kaambiwa atoe tafsiri ya socia security. mwachen abwabwaje akija kitaa ataona jins mabwanyenye wanavyofaid pesa za watumwa wanaotinga migodini tena bila hata kujua kesho yao. daah ipo haja ya hawa wanachuo kwenda field attachment walau mara moja kwa mwaka yan wanandoto za alinacha!! wanadhan sie hatupend kutunza pesa zetu na sie tunaakili dogo ila tunaangalia vitu kama Mfumuko wa bei, life expectancy, poor govt record keeping,money value, ufisadi, nguvu ya kuwekeza ukiwa na miaka 55. anyway kubishana na huyu dogo n kimkomaza acha amalize shule kwanza aje kitaa lugha ztaelewana tuu.

    ReplyDelete
  12. Ndugu mwombaji,
    i ni Bw James BILLINGS binafsi mkopo Taasisi, anayetoa mkopo katika kiwango cha chini sana riba ya 3% sisi kutoa kila aina ya mkopo kama.
    Elimu ya mkopo, mkopo Biashara, mkopo nyumbani, mkopo wa Kilimo, mkopo binafsi, mkopo auto na nyingine nzuri Sababu, mimi pia kutoa mikopo
    kutoka mbalimbali ya $ 5,000 USD-$ 800,000.00 USD katika kiwango cha 3% riba. Muda wa 1 - miaka 50 kulingana na kiasi unahitaji kama loan.contact nasi kupitia barua pepe:
    onlinesloanservice412@outlook.com
    Kindly JAZA MAOMBI YETU MFUMO NA GET BACK Marekani haraka iwezekanavyo
    MAELEZO YA KWANZA'S zinahitajika NI:
    1. Kamili majina:
    2. anwani:
    3. nchi:
    4. jimbo:
    5. Jinsia:
    6. umri:
    7. Hali ya ndoa:
    8. kazi:
    9. Namba ya simu:
    10. Kiasi zinazohitajika:
    11. Duration:
    12. Madhumuni ya mkopo:
    13. barua pepe:

    ReplyDelete
  13. Attn:

    Usikose nje kutoka kutoa yetu mega kama wewe ni katika haja ya mkopo au kama wewe
    wasiwasi juu ya madeni yako na kuwa na historia mbaya ya mikopo, tuna
    vifaa katika nafasi ya kukusaidia kurejesha udhibiti wa fedha yako.

    Huduma zetu ni pamoja na:

    - Business mikopo kwa ajili ya kuanza-up na refinancing biashara zilizopo
    - Binafsi mkopo hadi $ 500,000
    - Home mkopo
    - Muda mfupi mkopo
    - Mkopo wa gari na mikopo kwa ajili ya madhumuni yoyote worthwhile.

    Pamoja na mchakato wetu masaa 24 ya uamuzi huo, tunaweza kufadhili kwa ajili yenu ndani ya 2 hadi 3
    biashara siku moja kwa moja kwenye akaunti yako ya benki. Sisi kufikiria ni
    radhi kufanya biashara na wewe.

    Alitaka kuokoka? sisi kutoa kwa kukodisha taratibu zetu
    wanatakiwa kupata mkopo mapema. Tuna mtandao unaweza kujiinua
    juu ya!

    Reply nyuma kama una nia ya lindomartinez67@gmail.com

    Regards,
    Global Finance Services

    ReplyDelete
  14. Kutoa mkopo kuomba sasa katika fredpetersonworldloan@yahoo.com

    ReplyDelete
  15. haja ya chini kiwango cha riba mkopo
    .................................................................................................................................................................................................................................................................
    Habari

    Mimi ni Mheshimiwa Galvin, binafsi mkopo Taasisi ambayo inatoa mkopo kwa riba ya 2
    %, Mimi kutoa mikopo kwa watu binafsi na makampuni au makundi ya watu ambao
    kifedha chini. Ni fursa ya kifedha katika hatua yako mlango
    leo na kupata maoni ya haraka ya mikopo huko.

    Kuna fursa nyingi fedha na kusaidia katika nyanja zote na
    Bado kuhesabu. Lakini ni fursa ya kifedha juu ya doorstep,
    na msimu wa ukame ni kuja mwisho, na huwezi miss hii ya kipekee
    nafasi. Je, unahitaji msaada wa kifedha? Je, unahitaji mkopo kwa
    kupanua biashara yako? Je, unahitaji mkopo wa kuanzisha biashara juu ya kubwa
    wadogo? Unahitaji mkopo ambayo inaweza kubadilisha maisha yako na sasa wako
    hali ya kifedha? Je, Unahitaji mkopo haraka kuweka mambo
    katika mahali pa haki? Basi hakuna kuangalia zaidi, kwa sababu mkopo wako ni ndoto yako
    mlango hatua leo.

    huduma hutolewa kwa watu binafsi, biashara
    na watu wa biashara. Kiasi cha mikopo inapatikana katika aina mbalimbali ya $
    1,000.00 kwa dola za Marekani 500,000,000.00 au uchaguzi wako mimi kutoa mikopo kwa ajili ya
    mradi, biashara, kodi, bili, na sababu nyingine nyingi, mkopo wetu
    ni rahisi na * censored * kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa barua pepe
    : Internationalpropertyloan@gmail.com

    MAOMBI YA MKOPO
    ================================
    Jina: ...................
    Jina la pili: ..................
    Kuwasiliana Anwani: .................
    Nchi: ...................
    Umri: ..........................
    Jinsia: ....................
    Nambari ya simu: ..............
    Hali ya: .................
    Kazi: ...............
    nafasi: .................
    mapato ya kila mwezi: ..............
    Mkopo Kiasi: .................
    Madhumuni ya mkopo: ...............
    muda: ....................
    Je, kutumika kwa ajili ya mkopo kabla ya: ............
    wewe kuelewa Kiingereza: .................

    Baadhi ya maswali akajibu (Frequently Asked Questions) Tuna rahisi
    kuunda ajili yenu kujaza kuomba mkopo. kujaza fomu hiyo na kutuma
    kwangu. maombi inashughulikia mada zifuatazo. * Authorization *
    Mikopo Borrower information1.

    Ni kiwango cha riba ni nini? kiwango cha riba inategemea mradi.
    kiwango ni 2% riba kila mwezi tu kwa mwaka kiwango cha riba inayolipwa.
    2. Je, mikopo yangu jambo? si
    3. Wapi mkopo? Sisi mkopo Dunia
    4. Muda gani kuchukua ili kufadhili? Baada ya kuwasilisha mkopo
    maombi, unaweza kutarajia jibu awali chini ya masaa 24
    na fedha ndani ya masaa 72-96 baada ya kupokea taarifa tunahitaji
    kutoka kwako.
    5. Nini malipo yangu kuwa? Ambayo itakuwa mahesabu kwa wewe na
    alimtuma kwenu juu ya ratiba ulipaji alongwith suala mkopo.
    Sisi ni kuangalia mbele kwa biashara imara na uhusiano na wewe.
    Dhati,

    ReplyDelete
  16. Je, wewe katika haja ya mkopo haraka ya kulipa bili, upanuzi wa biashara, miili ya ushirika au mkopo binafsi? Wasiliana nasi leo kwa ufanisi na kuaminiwa yako haraka mkopo leo katika kupitia barua pepe: elenanino07@gmail.com

    Regards
    Bi Elena

    ReplyDelete
  17. Loan Kutoa @ cha 2% !!!

    kampuni yetu ni shirika ya kisheria ambayo iliundwa kusaidia watu ambao wanahitaji msaada, kama vile misaada ya kifedha. sisi ni USA msingi kampuni ya fedha.
    Hivyo kama wewe ni katika matatizo ya kifedha katika fujo fedha, na unahitaji fedha ya kuanzisha biashara yako yenyewe, au unahitaji mkopo kulipa madeni au kulipa bili yako, kuanza biashara nzuri, au ana Matatizo zilizokopwa zaidi ya benki za mitaa, wasiliana nasi leo Barua pepe: ohioloans85@gmail.com


    Mr Scotty

    ReplyDelete
  18. Mkopo wa Mkopo kwa hatua yako ya mlango

    Je! Unahitaji mkopo wa haraka?
    Unahitaji mkopo wa biashara?
    Unahitaji mkopo kwa uwekezaji wako?
    Unahitaji mkopo kutoa fedha yako tatizo?
    Unahitaji mkopo wa kibinafsi?
    Unahitaji biashara ya mkopo na mkopo?

    Ili kujitambulisha mwenyewe, mimi ni Steven George mwenyekiti binafsi ninawapa mkopo kwa kiwango cha riba 3%. Ni fursa ya kifedha kwenye mlango wako hadi sasa na kupata mkopo wa papo hapo. Kuna wengi huko nje wanatafuta chaguzi za kifedha au kusaidia karibu na mahali na hawana uwezo wa kupata moja, lakini ni fursa ya kifedha kwenye hatua yako ya mlango na hivyo huwezi kukosa fursa hii. Huduma hii ni kwa watu binafsi, makampuni, wafanyabiashara na wanawake. Kiwango cha mkopo kinapatikana kutoka $ 1,000.00 hadi $ 500,000,000.00, au idadi yoyote ya chaguo lako kwa habari zaidi wasiliana nasi kwa: stevengeorge168@gmail.com

    Kama kusubiri majibu yako ya haraka,
    Kwa heshima, Steven George.

    ReplyDelete