Sunday, July 29, 2012

BALOZI WA PAPA ATOA SAKARAMENT YA KIPAIMALA KWA MARA YA KWANZA KATIKA KANISA LA MT. PETRO, OSYTERBAY

Balozi wa baba Mtakatifu hapa nchini Askofu Mkuu Fransisko Montecillo Padilla akitoa sakaramenti ya kipaimala kwa Aivan Catrece wakati wa ibada iliyofanyika katika kanisa la mtakatifu Petro Osyterbay jijini Dar es Salaam, Jumla ya watoto 72 walipata ekaristi takatifu ya kipaimala.Wapili kulia ni Paroko wa kanisa hilo Padri  Joseph Mosha.
.Balozi wa baba Mtakatifu hapa nchini, Askofu Mkuu Fransisko Montecillo Padilla akimpaka mafuta ya kipaimala Theodory Helon  wakati wa ibada ya Sakaramenti ya kipaimala iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Osyterbay jijini Dar es Salaam, Jumla ya watoto 72 walipata sakramenti hiyo, kushoto ni mzazi wa kiroho  Daniel Mwisongo akiwa ame mweke mkono.

 Mmoja wa watoto waliopta sakaramenti ya kipaimala katika kanisa la Mtakatifu Petroa Aivan Catrece akionyesha kipaji chake cha kupiga ngoma wakati wa Ibada hiyo.
 Balozi wa baba Mtakatifu hapa nchini Askofu Mkuu Fransisko Montecillo Padilla akibariki misalaba wakati wa ibada ya sakaramenti ya kipaimala iliyofanyika katika kanisa la mtakatifu Petro Osyterbay jijini Dar es Salaam, (katikati) Paroko wa kanisa hilo Padri  Joseph Mosha na Kushoto ni Frateli Richard.Jumla ya watoto 72 walipata sakaramenti hiyo.
 Balozi wa baba Mtakatifu hapa nchini Askofu Mkuu Fransisko Montecillo Padilla akimkabidhi Aivan Catrece zawadi ya msalaba m wakati wa ibada ya Kipaimala iliyofanyika katika kanisa la mtakatifu Petro Osyterbay jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya watoto kati ya 72 waliopata sakaramenti ya kipaimala wakionyesha vyeti vyao baada ya kukabidhiwa na Balozi wa baba Mtakatifu hapa nchini Askofu Mkuu Fransisko  Padilla, wakati wa ibada hiyo iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Osytarabay jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa baba Mtakatifu hapa nchini Askofu Mkuu Fransisko Montecillo Padilla, akikabidhiwa zawadi ya mbuzi na Catrece Theodory ambaye ni mmoja wa wajumbe wa kamati wakati wa Ibada ya kipaimla iliyofanyika jumapili katika kanisa la mtakatifu Petro oysterbay jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Paroko wa parokia hiyo Joseph Mosha. 
 ;Balozi wa baba Mtakatifu hapa nchini Askofu Mkuu Fransisko Montecillo Padilla akitoa mahubiri wakati wa ibada ya sakaramenti ya  kipaimala  iliyofanyika katika kanisa la mtakatifu Petro Osyterbay jijini Dar es Salaam, Jumla ya watoto 72 walipata ekaristi takatifu ya kipaimala.Kushoto ni Paroko wa kanisa hilo Padri  Joseph Mosha.
 Balozi wa baba Mtakatifu hapa nchini Askofu Mkuu Fransisko Montecillo Padilla akiwahutubia watoto wa kipaimala  wakati wa ibada ya sakaramenti iliyofanyika katika kanisa la mtakatifu Petro Osyterbay jijini Dar es Salaam, Jumla ya watoto 72 walipata ekaristi hiyo.
  Juu na chini Balozi wa baba Mtakatifu hapa nchini Askofu Mkuu Fransisko Montecillo Padilla akitoa baraka kwa waumini wa kanisa la Mtakatifu petro Oysterbay wakati wa Ibada ya Kipaimala,Askofu huyo ilikuwa mara yake ya kwanza kuongoza ibada katika kanisa hilo ambapo alisalimiana na waumini waote kwa kuwapa mikonoa na baraka. PICHA ZOTE NA ALBART JACKSON.

No comments:

Post a Comment