Esta Zelamula ambaye ni mhariri kutoka Channel 10 akiuliza swali wakati wa mkutano wa wahariri na waandishi wa habari waandamizi kuhusu sensa ya watu na makazi iliyotarajiwa kufanyika tarehe 26 Mwezi wa nane mwaka huu uliofanyika jana mjini Morogoro. Zaidi ya shilingi bilioni 141 zitatumika katika zoezi hilo.
Mussa Twangilo ambaye ni mhariri kutoka TBC Taifa akiuliza swali wakati wa mkutano wa wahariri na waandishi wa habari waandamizi kuhusu sensa ya watu na makazi iliyotarajiwa kufanyika tarehe 26 Mwezi wa nane mwaka huu. Mada mbalimbali zilijadiliwa katika mkutano huo wa siku moja ulifanyika jana mjini Morogoro.
Afisa Uhamasishaji sensa ya watu na Makazi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Said Amir akiwaonyesha wahariri na waandishi wa habari waandamizi (hawapo pichani) kitabu cha ufafanuzi wa maswali ya sensa ya watu na makazi mwaka 2012. Wanahabari hao walihudhuria mkutano wa siku moja wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 ulioandaliwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu uliyofanyika mjini Morogoro.
Mtakwimu Mohamed Kilonzo kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu akiwaelekeza wahariri na waandishi wa habari waandamizi jinsi ya kujaza dodoso refu litakalojazwa wakati wa sensa ya watu na makazi inatarajia kufanyika kote nchini kuanzia tarehe 26 Mwezi wa nane mwaka huu. Wanahabari hao walihudhuria mkutano wa siku moja wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika jana mjini Morogoro.
Afisa Uhamasishaji sensa ya watu na Makazi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Said Amir akifurahia jambo wakati akiwaonyesha wahariri na waandishi wa habari waandamizi (hawapo pichani) dodoso refu litakalojazwa wakati wa sensa ya watu na makazi inatarajia kufanyika kote nchini kuanzia tarehe 26 Mwezi wa nane mwaka huu. Zaidi ya shilingi bilioni 141 zitatumika katika zoezi hilo.
Baadhi ya wahariri na waandishi wa Habari waandamizi wakiangalia na kujaribu kujaza dodoso refu litakalojazwa wakati wa sensa ya watu na makazi inatarajia kufanyika kote nchini kuanzia tarehe 26 Mwezi wa nane mwaka huu. Wanahabari hao walihudhuria mkutano wa siku moja wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika leo mjini Morogoro ambapo mada mbalimbali zilijadiliwa katika mkutano huo.
Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi waliohudhuria mkutano wa siku moja wa sensa ya watu na makazi uliofanyika jana mjini Morogoro wakisikiliza mada ya nafasi ya vyombo vya habari katika kufanikisha sensa ya watu na makazi mwaka 2012 iliyotolewa na Afisa Uhamasishaji sensa ya watu na Makazi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Said Amir. Zaidi ya shilingi bilioni 141 zitatumika katika zoezi hilo.Picha na Anna Nkinda - Maelezo
No comments:
Post a Comment