Wednesday, June 13, 2012

Vodacom yakutana na Wahariri wa Vyombo vya Habari mjini Dodoma leo

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw Rene Meza akielezea jinsi Vodacom ilivyochangia zaidi ya shilingi bilioni 700 katika malipo ya kodi ya serikali alipokutana na waandishi wa habari mjini Dodoma.
Ofisa Mkuu wa Mahusiano ya Jamii wa Vodacom, bi Mwamvita Makamba akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kukutana na kamati ya bunge ya miundo mbinu, sayansi na teknolojia mjini Dodoma.
Mhariri wa gazeti la The Guardian Bw. Florian Kaijage akiuliza swali kuhusiana na Vodacom Tanzania kuchangia zaidi ya shilingi bilioni 700 katika kodi za serikali katika mkutano na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza(Hayupo Pichani), kushoto kwake ni mhariri wa gazeti la Mwananchi Bw. Neville Meena.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza akishauriana jambo na Afisa Mkuu wa Mahusiano Bi Mwamvita Makamba na Mkurugenzi wa Fedha wa Vodacom Tanzania Bw. Tiaan Botha (kulia) baada ya mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia uchangiaji wa zaidi ya shilingi bilioni 700 katika kodi za serikali mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Fedha wa Vodacom Tanzania Bw. Tiaan Botha akishauriana jambo na Afisa Mkuu wa Sheria Bw. Walarick Nittu (wa pilli kulia), Afisa Mkuu wa Mtandao Bw. Alec Mulonga (kulia) na mkuu wa kitengo cha Uhandisi wa Vodacom Tanzania Bw. George Magonyozi (kushoto) baada ya mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia uchangiaji wa zaidi ya shilingi bilioni 700 katika kodi za serikali mjini Dodoma.
Mhariri wa gazeti la The Citizen Bw. Peter Nyanje akiuliza swali kuhusiana na Vodacom Tanzania kuchangia zaidi ya shilingi bilioni 700 katika kodi za serikali katika mkutano na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza(Hayupo Pichani), kati kati ni mhariri wa gazeti la Daily News Bw. John Kulekana na kushoto ni mhariri wa gazeti la Habari Leo Bw. Mgaya Kingoba.
Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza (hayupo pichani) wakati alipokuwa akiwaelezea uchangiaji wa Vodacom wa zaidi ya Shilingi bilioni 700 katika kodi za serikali alipokutana nao mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw Rene Meza akielezea jinsi Vodacom ilivyochangia zaidi ya shilingi bilioni 700 katika malipo ya kodi ya serikali alipokutana na waandishi wa habari mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment