Tuesday, May 8, 2012

TANZANIA YAANZA KWA KISHINDO MASHINDANO YA NETIBOLI YA AFRIKA

Kikosi cha timu ya Lesotho.
Kikosi cha timu ya taifa ya Netiboli ya Tanzania 'Taifa Queen's.
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete akikagua timu ya Lesotho.
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete akikagua timu ya Taifa Queen's.
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete akikumbuka enzi zake wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo.
Mshike mshike katika mchezo huo wa Ufunguzi.
Mfungaji wa timu ya Taifa Queens, Mwanaid Hassan akitafuta mbinu za kumtoka mlinzi wa Lesotho, Tjabane.
Mchezo huo ulikuwa ni wa vuta nikuvute.
Taifa Queen's wakipiga jaramba.
Waamuzi wa mchezo huo wakisalimiana na mgeni rasmi.

TIMU ya taifa ya netiboli ya Tanzania, Taifa Queens, leo imeanza vema mashindano ya Afrika baada ya kuichapa timu ya Lesotho kwa magoli 57-13, katika mechi ya ufunguzi iliyorindima kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, Taifa Queens ikiongozwa na wafungaji wake, Mwanaidi Hassan ‘Pereirra’ (GS) na Irene Elias (GA), ambao walikuwa wakiunganishwa vema na kiungo, Faraja Malaki (C), Evodia Kazinja (WA), na Restuta Boniface (WD), hadi robo ya kwanza inamalizika, walikuwa mbele kwa magoli 13-3.

Robo ya pili, Taifa Queens ilizidi kuchanua mbele ya mgeni rasmi, Mke wa Rais Kikwete, Mama Salma, ambapo hadi inamalizika walitoka na magoli 23-9 huku robo tatu wakimaliza kwa 40-13.

Robo ya nne, ukuta wa Taifa Queens uliokuwa chini ya Lilian Sylidion (GD), na Doritha Mbunda (GK), uliwabana vilivyo wafungaji wa Lesotho na hadi mchezo unamalizika, waliibuka kidedea kwa ushindi huo wa magoli 57-13.

Michuano hiyo inayoshirikisha nchi nane, inaendelea tena leo kwa mechi kati ya Botswana na Zambia, Malawi na Zimbabwe, huku wenyeji Tanzania wakitupa karata tena kwa Zambia.Picha na Habari na Francis Dande wa Globu ya Jamii.

2 comments:

  1. KAMUA KAMUA DADA ZETU...TUNAWATEGEMEA.....ZAMU HII TUTASUKA MPAKA KIELEWEKE. TUMEZOEA KUNYOLEWA

    ReplyDelete
  2. Tatizo wanamichezo yetu maumbo madogo hawana stamina. si football wala netball, hata basketball tunachukua watu wadogo ndo maana ushindi ni duni

    ReplyDelete