Ankal habari !
Ukoo wa Manambi Choka unaendelea na libeneke la harusi kwa kwenda mbele. Safari hii ni Luteni Abdulkadir Manambi Choka ni mpwa wangu amemposa Bi Amina binti Shaban Sato! Jumamosi Mei 26, 2012 tuliwasilisha mahari kwa Bi Harusi mtarajiwa BL 41 Kinondoni ambapo baada ya kutoa mahari ikafuatiwa na mnuso wa nguvu halafu Adfande Abdul akamvisha pete ya uchumba Bi Harusi mtarajiwa .
Muihtasari wa habari katika picha ni:
Mjomba wa Bwana Harusi Mtarjiwa Mzee Issa E.C.Manambi akitoa dibaji ya ulipaji mahari ambapo aliwaambiwa Wazazi wa Bi Haruisi Mtarajiwa kuwa unalipwa mzigo kamili, picha inafuatiwa Mzee Issa Maanambi anakabidhi 'mzigo' kamili kwa Baba Mdogo wa Bi harusi Mtarajiwa Mzee Yahya Sato , mzigo huo baadae unahakikiwa na Mjomba wa Bi Harusi Mtarajiwa nakuonekana umetimia.
Mnuso uliofuata na halafu Bi Harusi Mtarajiwa analetwa katika hadhara na Afande Abdul Choka anamvisha pete ya uchumba 'rasmi'! Picha nyingine ni za ukumbusho Mama Mzazi wa Bwana Harusi Bi Mwajellah Manambi Choka na Mama Mdogo wa Bi Harusi Mtarajiwa Bi Simtovu Bakari Msonde ( mwenye mikongojo) na Maharusi Watarajiwa na nyingine za upande wa Bwana Harusi Mtarajiwa na Bi harusi Mtarajiwa.
Ankala usinichoke naomba uchapishe kwa usanifu wako picha hizi katika blog yako.
Shukran !
Wasalaam
Mdau - Midladjy Manambi Maez
Mei 28, 2012
Dar es Salaam.
Mzigo ukihesabiwa
Mnuso wa hafla
Hapa tonge nyama
Bw Harusi Mtarajiwa aingia
Akutana na mtarajiwa mwenza
Baadhi ya mashuhuda
Mtarajiwa apiga goti kuomba chanda cha pete
Abusu chanda kilichorembwa pete yake
Hii hapa....
Chereko chereko...
Wazaa chema wafurahia
Picha ya pamoja
Picha nzuri and i wish you best of luck to your upcoming weeding day.kubwa ni uvumilivu,upendo na uaminifu.Hamza sato.
ReplyDeleteAfande Choka umefunika ile Mbaya nakukaribisha kiumeni Baba.Mimi niko kwenye Ndoa Miaka Mitatu sasa,Nakutakia Mafanikio na Shemeji yangu Inshalaaah.Ni mimi Chokest your Class mate(Ihongoo).
ReplyDelete