Sunday, April 8, 2012

RAIS KIKWETE AHANI VIFO VYA IGP MSTAAFU HARUN MAHUNDI NA MCHEZA SINEMA STEVE KANUMBA LEO JIJINI DAR

 Rais Jakaya Kikwete akiwasili nyumbani kwa IGP mstaafu Marehemu Harun Mahundi sehemu za Mikocheni jijini Dar es salaam alikokwenda kuhani msiba huo
 Rais Kikwete akisalimiana na ndugu, jamaa na marafiki msibani hapo
 Rais Kikwete akisalimiana na mtoto wa marehemu
 Rais Kikwete akisalimiana na mtoto wa marehemu





Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Inspekta Jenerali wa Polisi Mstaafu,Marehemu Harun Mahundi aliyefariki Dunia april 5, 2012 na kuzikwa jana jijini Dar es salaam. Hapo ni nyumbani kwa marehemu Mikocheni barabara ya Rose Garden,jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwafariji watoto wa Inspekta Jenerali wa Polisi Mstaafu,Marehemu Harun Mahundi aliyefariki april 5, 2012 na kuzikwa jana jijini Dar es salaam.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Steven Charles Kanumba Sinza 'Vatican' jijini Dar es salaam leo na kutoa mkono wa pole kwa wafiwa.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na waombolezaji nyumbani kwa marehemu Steven Charles Kanumba Sinza 'Vatican' jijini Dar es salaam leo alikofika kuomboleza nao msiba huo mkubwa kwa taifa letu kiujumla.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili nyumbani kwa marehemu Steven Charles Kanumba,Sinza 'Vatican' jijini Dar es salaam leo kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kwa wafiwa,hapa akisalimianaa na mdogo wake na Marehemu Steven Kanumba.
Rais Kikwete akiwafariji wafiwa nyumbani kwa marehemu Steven Charles Kanumba Sinza 'Vatican' jijini Dar es salaam leo alikofika kuomboleza nao msiba huo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wanakamati ya msiba wa marehemu Steven Charles Kanumba Sinza 'Vatican' jijini Dar es salaam leo alikofika kuomboleza nao kifo hicho.
Rais Kikwete akiaga waombolezaji nyumbani kwa marehemu Steven Charles Kanumba Sinza 'Vatican' jijini Dar es salaam leo.
Rais Kikwete akiongea na waandishi wa habari wakati akiondoka msibani hapo.

2 comments:

  1. Naamini kuwa kifo kimeumbwa kwa viumbe wote, lakini sijui kwa nini inakuwa ngumu kuamini kuwa huyu kijana ameondoka.Nimeumizwa sana na kuondoka kwako Kanumba, licha ya kwamba si ndugu yangu. Tutakumiss Kanumba!

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli kama utaingia kwa kila moyo wa kila mmoja na kuona maumivu mtu aliyokuwa nayo kwa kifo cha huyu Kijana,utashangaa na kujua kwa jinsi gani alikuwa wa muhimu sana katika jamii ya watanzania kwa ujumla..binafsi nimeumia sana na hiki kifo na mpaka muda huu napoandika haya maoni yangu siamini kwa kweli,lakini ukweli unabaki palepale kuwa Steven Kanumba hayupo tena katika dunia yetu hii...kikubwa ni kumuombea wazazi wake na ndugu zake Mungu awape faraja ya hali ya juu maana kwa wao wenyewe hawataweza kwa kweli,kingine ni kumuombea Bint yetu Lulu Mungu amuepushe na hili tukio linalomuhusisha yeye,kwa upande wangu<Lulu hana kosa lolote kwa kweli,kifo kinamfika mtu wakati wowote na kwa njia yoyote inapofika wakati wake,inachotafuta ni sbb ndogo ili mtu aweze kuondoka muda ule na wakati ule anaohitaji kuondoka,hivyo msimuhukumu huyu mtoto,samahani kama nitawaudhi kwa hili swali nauliza je ingekuwa imekukuta wewe au yeye Lulu ndio kaondoka mgesemaje(Mungu ampe uhai mrefu)tukubali muda wa kuondoka Kanumba ulifika na ulikuwa unatafuta sbb na ukaipata,kikubwa ni kuomba Mungu atusaidie katika wakati huu mgumu Ameeen..R.I.P STEVEN CHARLES KANUMBA

    ReplyDelete