Saturday, April 28, 2012

Kongamano la Pili la Makatibu Muhtasi laendelea leo jijini Mwanza

 Mkuu wa Mkoa Mwanza,Eng.Evarist Ndikilo akitoa hotuba yake ya kufunga Kongamano la Pili la Makatibu Muhtasi nchini Tanzania (2th National Secretarial Confrerence) lililomalizika rasmi leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika Beach Resort,Jijini Mwanza. 
 Katibu Mkuu wa Chama cha Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA),Bhoke Matinyi akizungumza kwenye Kongamano la pili la Makatibu Muhtasi nchini ambalo limemalizika rasmi leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika Jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa Kumbukumbu na Nyaraka za Serikali nchini kutoka Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma,Charles Magaya akizungumza kwenye Kongamano la pili la Makatibu Muhtasi nchini (TAPSEA) linalofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika Jijini Mwanza.
Muwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma,Mama Wanderage akitoa maelezo ya namna Katibu Muhrasi anavyotakiwa kuwa kwenye kazi yake wakati wa Kongamano la pili la Makatibu Muhtasi nchini (TAPSEA) linalofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika Jijini Mwanza.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza,Eng.Evarist Ndikilo akitoa baadhi ya vyeti kwa washiriki wa Kongamano hilo lililomalizika rasmi leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Holeli ya Malaika,Jijini Mwanza. 
 Mkuu wa Mkoa Mwanza,Eng.Evarist Ndikilo akisoma moja ya majina ya washindi wa bahati nasibu iliyofanyika ukumbini hapo kwa baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo,ikiwa ni nafasi ya kwenya kusoma kozi ya Mdea 1 na Mdea 2 nchini Uganda.
Mkufunzi na Muwezeshaji wa Kongamano la Pili la Makatibu Muhtasi nchini,Carl Bosser akitoa mafunzo mbali mbali ya namna Makatibu Muhtasi wanavyotakiwa kutenda kazi zao kwa ufasaha pindi wawapo katika majukumu yao ya kikazi wakati Kongamano hilo linalofanyika hivi sasa kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika Jijini Mwanza.
MC wa Kongamano hilo,Maulid Kitenge akitoa taratibu kwa washiriki.
 MC Ephrahim Kibonde akiongoza shughuli hiyo.
 Picha ya Pamoja na Washindi wa Bahati nasibu ya kwenda kusoma kozi ya Mdea 1 na Mdea 2,nchini Uganda.
Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA),Pili Penda  akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Eng.Evarist Ndikilo mara baada ya kufunga rasmi Kongamano la Makatibu Muhtasi nchini,uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika,Jijini Mwanza.
Baadhi ya Washiriki wa Kongamano la pili la Makatibu Muhtasi nchini (TAPSEA) linalofanyika hivi sasa kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika Jijini Mwanza.

No comments:

Post a Comment