Sunday, April 29, 2012

BIAFRA KIDS YASHINDA MECHI YAKE DHIDI YA AFRICAN TALENT

Kinyang'anyiro cha mashindano ya Copa Coca Cola chini ya miaka 17 wilaya ya Kinondoni kimeendelea tena leo katika uwanja wa Mwl. Nyerere, Magomeni Makurumla kwa kuzikutanisha timu za Biafra Kids dhid ya African Talent. Mechi hiyo iliyokuwa ichezwe majira ya saa 10 jioni ilichezwa saa 5 asubuhi kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo waandaaji.
Biafra Kids wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa klabu ya michezo ya Biafra muda mfupi kalba ya kuanza mechi

Mechi hii, wachezaji walipania sana kushinda baada ya kupoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Eleven Boys kwa magoli 4 - 1. Hivyo walifanya mazoezi ya nguvu na kujiongezea ari kubwa ya ushindi na hatimaye kuichabanga timu ya African Talent kwa mabao 3 - 1.


Biafra Kids katika picha ya pamoja na wanachama na mashabiki

 Hamasa ya ushindi pia ilichangiwa na mashabiki wengi waliofunga safari kuja kuishangilia timu hiyo. kama picha inavyojieleza hapo juu, wanachama na mashabiki hao hawakujali mvua iliyokuwa ikinyesha bali walichohitaji ni ushindi tu na si vinginevyo. Mashabiki hao wake kwa waume waliishangilia timu yao tangu mwanzo hadi mwisho wa mchezo.
Biafra Kids - kikosi kilichoanza (first eleven) katika picha ya pamoja


Wachezaji wakipasha misuli kabla ya kuingia uwanjani


 Mfungaji wa goli la kwanza Abu Selemani (wa kwanza kushoto) na mfungaji goli la tatu Khamis Ibrahim (wa katikati)


Mabeki Machachari wa Biafra Kids Fareed Massoud (kushoto), Ahmad Ibraheem (kulia) na Abdul Moshi (nyuma)


tayari kwa ukaguzi na kuanza kwa mechi


Timu mwenyeji wa mechi hiyo African Talent wakisalimiana na Biafra Kids


Manahodha wa timu zote mbili katika picha ya pamoja na refa wa mchezo huo


Biafra Kids wakilisakama lango la African Talent

Karamu ya magoli ilifunguliwa na Abuu Selemani dakika ya 18 baada ya kupokea krosi safi ambapo aliiunganisha nyavuni na kumwacha kipa wa African Talent akiruka bila kuupata mpira. Baada ya kufunga tu goli hilo, kasi ya mchezo ilingezeka maradufu na mnamo dakika ya 24 Babulu Hamad aliipatia Biafra Kids bao la pili. African talent walijipatia bao la kufutia machozi kwa njia ya penati baada ya mchezaji wao kujidondosha katika eneo la hatari na kumhadaa refa kuwa amechezewa rafu . Dakika ya 41 karamu ya magoli ilihitimishwa na Khamis Ibrahim ambaye aliutia mpira nyavuni kiufundi. 

Mara baada ya nusu ya kwanza ya mchezo kukamilika, Biafra Kids walitanza soka la ukweli na kusababisha kosa kosa kadhaa na magoli ambayo refa aliyakataa.

Biafra Kids inatarajia kujitupa tena uwanjani tarehe 1 Mei, 2012  kuchuana na Vijana Muslim pale pale kwenye uwanja wa Mwl. Nyerere.

MUNGU IBARIKI TIMU YETU!

No comments:

Post a Comment