Saturday, February 25, 2012

Rais wa Zanzibar,awaalika chakula cha mchana washiriki wa Halaiki Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akiwapungia mkono watoto walioshiriki katika maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar,wakati alipowaalika chakula cha mchana katika ukumbi wa Salama Bwawani Hoteli jana,(kulia) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Mwinyihaji Makame,na Waziri wa Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mhe.Mohamed Aboud Mohamed.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Walimu wa Halaiki katika viwanja vya ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar jana, wakati alipowaalika watoto walioshiriki katika maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar, katika chakula cha mchana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,wakati wa ghafla ya chakula cha mchana,walichoandaliwa watoto walioshiki katika Halaiki wakati wa Maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,huko Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar.
Walimu wa Halaiki wakiwa katika picha wakati wa kutambulishwa kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,wakati wa hafla ya chakula cha Mchana walichoandaliwa watoto walioshiriki Halaiki katika maadhimisho ya miaka 48 ya mapinduzi ya Zanzibar,hafla hiyo ilifanyika jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotelm Mjini Zanzibar.
Watoto walioshiriki katika Halaiki ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar,wakiwa wamevalia sare,wakisubiri kuanza kwa shuhuli hiyo ya chakula cha mchana walichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduziu Dk.Ali Mohamed Shein, jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar.
Baadhi ya watoto walioshiriki katika Halaiki ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar,wakichua chakula cha mchana walichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduziu Dk.Ali Mohamed Shein, jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar,pia wakiwa wamevalia sare maalum.
Baadhi ya watoto walioshiriki katika Halaiki ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar,wakila kwa utulivu chakula cha mchana walichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduziu Dk.Ali Mohamed Shein, jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar,pia wakiwa wamevalia sare maalum.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(wa tatu kulia) Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,(kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Mwinyihaji Makame,(wa pili kulia) na Katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abdulhamid Yahya Mzee,wakiitikia Dua iliyoombwa baada ya wa ghafla ya chakula cha mchana, walichoandaliwa watoto walioshiki katika Halaiki wakati wa Maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,huko Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Walimu wa kufundisha Halaiki ya watoto,baada ya hafla ya chakula cha Mchana walichoandaliwa watoto walioshiriki Halaiki katika maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar,hafla hiyo ilifanyika jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotelm Mjini Zanzibar.Picha na Ramadhan Othman IKULU.

No comments:

Post a Comment