Wednesday, January 11, 2012

Maspika wa Mabunge ya nchi za Jumuiya ya Madola waendelea na Mkutano wao wa 21, mjini Port of Spain- Trinidad and Tobago

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (katikati) akiwa pamoja na baadhi ya Maspika Mbalimbali kutoka Mabunge ya nchi wananchama wa Jumuiya ya Madola wakati wa kujadili maada kuhusu nafasi ya Bunge Kuishauri na kuisimamia Serikali. Maspika wa nchi wananchama wa Jumuiya ya Madola wanakutana Port of Spain katika Visiwa vya Trinidad and Tobago kuazia tarehe 7 hadi 12 January, 2012 katika mkutano wao wa 21 kujadili maswala mbalimbali ya kuimarisha mabunge yao.
Mwenyekiti wa chama cha mabunge nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) , Mhe. Sir Alan Haselhurst, Mbunge kutoka Uingereza akichangia nae katika mojawapo ya mada zilizowasilishwa katika mkutano wa 21 wa maspika wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola.
Baadhi ya Burudani zikiendelea wakati wa chakula cha Jioni.

Spika wa Ushelisheli na Mwenyekiti wa CPA kanda ya Afrika akisisitiza jambo katika mkutano wa 21 wa Maspika wa nchi wananchama wa Jumuiya ya Madola unaofanyika mjini Port of Spain, Trinidad and Tobago. Kulia ni Spika wa Rwanda Mhe. Rose Mukantabama.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisalimiana na Katibu wa Bunge la Ghana Ndg. Emmanuel Anyimadu wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Visiwa vya Trinidad and Tobago Mhe. Proffesor George Maxwell Richards, kwa maspika wa nchi wananchama wa Jumuia ya Madola ambao wanahudhuria mkutano wao wa 21 katika Visiwa vya Trinidad and Tobago.
Spika Makinda akiteta Jambo na Spika wa Bunge la Kenya Mhe. Kenneth Marende (Mb) wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Visiwa vya Trinidad and Tobago Mhe. Proffesor George Maxwell Richards, kwa maspika wa nchi wananchama wa Jumuia ya Madola ambao wanahudhuria mkutano wao wa 21 katika Visiwa vya Trinidad and Tobago.

Rais wa Visiwa vya Trinidad and Tobago Mhe. Proffesor George Maxwell Richards, Rais wa Baraza la Senate la Visiwa hivyo Mhe. Timothy Hamel Smith, Spika wa Bunge la Visiwa vya Trinidad and Tobago Mhe. Wade Mark (Mb) na Mke wa Rais wa Trinidad and Tobago Dr. Jean Ramjohn-Richards wakifuatilia Burudani
Spika Makinda akiwa na baadhi ya Maspika wenzake pamoja na Raisi wa Visiwa vya Trinidad and Tobago Mhe. Proffesor George Maxwell Richards (Katikati) mara baada ya chakula cha Jioni. Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge.
Rais wa Visiwa vya Trinidad and Tobago Mhe. Proffesor George Maxwell Richards, akimkaribisha Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais huyo kwa maspika wa Nchi wananchama wa Jumuia ya Madola. Zaidi ya Maspika na viongozi mbalimbali wa kibunge 100 wanafanya mkutano wao wa 21 katika Visiwa vya Trinidad and Tobago.
Spika Makinda akiteta Jambo na Spika wa Bunge la Uganda Mhe. Rebbeca Kadaga (Mb) wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Visiwa vya Trinidad and Tobago Mhe. Proffesor George Maxwell Richards, kwa maspika wa nchi wananchama wa Jumuia ya Madola ambao wanahudhuria mkutano wao wa 21 katika Visiwa vya Trinidad and Tobago.

Mke wa Rais wa Trinida and Tobago Dr. Jean Ramjohn-Richards akimpongeza Spika wa Bunge la Tanzania kwa kuwa mojawapo wa viongozi wa kike katika bara la Afrika wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Visiwa vya Trinidad and Tobago Mhe. Proffesor George Maxwell Richards, kwa maspika wa nchi wananchama wa Jumuia ya Madola ambao wanahudhuria mkutano wao wa 21 katika Visiwa vya Trinidad and Tobago.

No comments:

Post a Comment