Monday, January 23, 2012

MAMA BALOZI UK JOYCE KALLAGHE AWAKARIBISHA WAHESHIMIWA WABUNGE WANAWAKE CHAKULA CHA JIONI NYUMBANI KWAKE

 Mwenyekiti wa TAWA Uk Mariam Kilumanga, Afisa ubalozi mambo ya utawala Mrs. Rose Kiondo na Deputy Chairman wa TANZUK Ma Nelly wakiwa katika pich aya pamoja na Mhe.Al-Shaymaa J. Kwegyir
 Mama Balozi Joyce Kallaghe akiw ana wageni waheshimiwa wabunge Beatrice Shelukindo na Mamlek Sokoine
 Mwana libeneke Jestina George akiwa katika picha ya pamoja na waheshimiwa Al-Shaymaa J. Kwegyir, Agripina Z Buyogera na Susan Lyimo
 Mwenyekiti wa TAWA UK Mariam Kilumanga na mwana libeneke Jestina George wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Al-Shaymaa J. Kwegyir
 Picha ya pamoja na waheshimiwa baada ya chakula cha jion
 Mh. Anna Abdallah mwenyekiti wa TWPG na kiongozi wa msafara
 Katibu wa Chama cha wanawake UK (TAWA UK) Mariam Mungula akiwaeleza waheshimiwa machahceh kuhusu chama hicho.
 Waheshimiwa Esther Matiku na Angela Kairuki wakipata Chakula
 Mhe. Susan Lyimo akipata chakula na waalikwa wengine
 Waheshimwa wabunge wakiwa tayari kwa kupata chakula cha jioni kilicho andaliwa maalumu kwaajili yao na mama Balozi Joyce Kallagehe nyumbani kwake
 Afisa wa Bunge Mrs Justina Shauri, Mhe. Esther Matiku, Mhe. Beatrice Shelukindo na Mama Balozi Joyce Kallaghe wakiwa wanamsikiliza mhe. Balozi akitoa ukaribisho
 Mhe. Balozi Peter Kallaghe akiwakaribisha waheshimiwa wabunge
Mhe. Beatirce Shelukindo akiwa na Mama Balozi Joyce Kallaghe


Wageni hao 12 wakiwemo Wabunge 11 na Afisa wa Bunge 1 waliotokea nyumbani Tanzania na kuja UK kwa Mualiko wa Commonwealth parliamentarians Group (CPA) walikaribisha chakula cha jioni na Mama Joyce Kallaghe Mke wa Balozi wa Uingereza akiwa na Viongozi wa Chama cha TA na TAWA nyumbani kwake Tanzania hao
 
Wabunge hao 11 wote wanawake na ambao miongoni mwao ni Viongozi wa wajumbe wa Tanzania Women Parliamentarians Group (TWPG) ,waliongozwa na Mwenyekiti wa TWPG Mheshimiwa Mama Anna Abdalla MP, na wakiwemo Mh.Susan Lyimo MP, Mh. Magdalena  h. Sakaya (MP) , Mh. Angela Kairuki (MP), Mh. Esther matiko (MP, Mh. Beatrice Shelukindo (MP), Mh. Riziki Omari Juma (MP), Mh. Namalek Sokoine (MP), Mh . Faharia Hamisi (MP) ,Mh. Al-Shaymaa J. Kwegyir (MP), Mh. Agripina Z Buyogera (MP) na Afisa wa Bunge Mrs Justina Shauri.
 
Wageni walikaribishwa na Balozi Mheshimiwa Peter Kallaghe na Mama Balozi Joyce Kallaghe , Mheshimiwa Balozi aliongea machache ya Ukaribisho na kumpa nafasi Mh.Mama Anna Abdalla ambae alishukuru kwa mualiko huo na kuelezea kuhusu Umoja wa Wabunge Wanawake (TWPG) ambao kila Mbunge Mwanamke wa Bunge la Tanzania ni mwanachama wake  na jinsi gani TWPG inavyofanya kazi kwa pamoja bila ya kujali itikadi za vyama vya kisiasa vya Waheshimiwa hao.  Usiku huo iliweza dhihirika kwa jinsi waheshiwa hao walivyokuja kujitambulisha kila mmoja alisimama na kujitambulisha na walilotilia msingi katika utambulisho wao ni kamati zao tofauti za Bunge ambazo wanahusika nazo na kuwa wnachama wa kikundi cha TWPG. Wageni waliokuwa pale walishuhudia zaidi ya nusu ya hawa wabunge waliongia na furaha bila ya kujali kuwa bado wana uchovu wa safari kutoka nyumbani wakisahau kutaja vyama vyao vya kisiasa. Mheshimiwa Mama Anna Abdalla alisisitiza kwamba ingawa vyama vya siasa ndio vilivyowapeleka wote bungeni lakini wakishaingia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano ,wanawake bungeni hawaangalii vyama vyao vya siasa bali huwa wakiwa Bungeni kabla ya sera yeyote kupita Wanawake huwa wote kwa Umoja wanaangalia hii itamnufaisha vipi Mwanamke na Mtoto wa Kitanzania.
 
Maneno haya ya Mheshimiwa Mama Abdalla yalidhihirishwa na jinsi Waheshiwa wote walipokaa katika meza moja na kuongea na kucheka kwa pamoja na kwa furaha huku wakila chakula kitamu cha jioni bila ya kujali pale kwenye ile meza kuna CCM, NCCR, CUF wala CHADEMA. Kitendo hiki kiliwavutia sana viongozi wa wanawake London ambao walikuwepo katika shuguli hii Bi. Nelly Msemwa (TA Taifa Deputy chair anaeshughulikia mambo ya wanwake  ),Bi. Mariam Kilumanga(TAWA Chair ), BI Mariam Mungula (TAWA Secretary) , Bi Rose Kiondo (Afisa Ubalozi) na Bi Jestina George (TA London na Blogger), kiasi ambacho walipopewa nafasi ya kuongeza machache walimpa nafasi hii Bi Mariam Mungula ambae aliwashukuru sana Waheshimiwa Wabunge wa kitendo hicho na somo walilompa  la kuwa hata Wakiwa Bungeni yeye akifikiri hakuna mashirikiano kati ya vyama tofauti kumbe sivyo kabisa wakiwa ndani na nje ya Bunge wanaweka wote ni kitu kimoja. BI Mariam Mungula vilevile alielezea kaazi za kikundi wa kina mama cha hapa UK ambacho yeye ni mmjoa wa viongozi wake Tanzania Women Association (TAWA)  na kumalizia kwa kuwaomba waheshimiwa wabunge kupitia TWPG wasihau kuwa kuna wanawake wengine wa kitanzania hata kama ni nje ya nchi na ambao wako tayari kushirikiana nao kwa lolote katika kumuendeleza MWanamke wa KItanzania.
 
Kikundi hichi cha Waheshimwa kimekuja Uingereza kwa Mualiko wa CPA kwa siku chache katika majukumu yao ya kila siku ya kumpingania Mtanzania.
 
Mungu Ibariki Tanzania.

Picha na Habari Jestina George 

No comments:

Post a Comment