Sunday, July 31, 2011

mambo yalivyokuwa siku ya Tamasha la 17 la Mzanzibari

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed akizinduwa Tamasha hilo la 17 la Mzanzibari kwa kupiga  bastola kuashiria kuanzisha resi za ngalawa.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud  akitowa hutuba ya Ufufunguzi wa Tamasha la 17 la Mzanzibar lililofanyika katika Ufukwe wa Pwani ya Nungwi.
Ngoma ya Mwanandege ikiwa ni moja ya kivutio cha Tamasha hilo
WASANII wa Oman wakifuatilia maonesho ya tamasha la Mzanzibar, nao walialikwa kuonesha ngoma za Utamaduni wa kwao. 
KIKUNDI cha Taarab cha Sanaa wakiimba wimbo maalum wa Zinduzi wa Tamasha


Ngalawa tayari kuanza resi

NGALAWA zikianza mashindano hayo katika ufukwe wa pwani ya Nungwi ikiwa ni moja ya Maonesho ya Uzinduzi wa Tamasha la Mzanzibar.
watu walijaa tele Nungwi siku hii
WANANCHI wa Kijiji cha Nungwi  wakiangalia resi za ngalawa zikiza mashindano hayo. 

MAMBO ngoma ya Bomu hayoooo..
WASANII kutoka nchi Oman wakifuatilia ngoma za Utamaduni wa Zanzibar katika maonesho ya Tamasha la Mzanzibar,   
WATOTO kutoka Skuli ya Kidutani wakicheza ngoma ya Bomu
WASANII kutoka Pemba wakicheza ngoma ya Njuguu  katika tamasha la Mzanzibar.
WASANII kutoka Nchi Oman wakionesha Ngoma za Utamaduni wa kwao katika maonesho ya Uzinduzi wa Tamasha la Mzanzibar katika ufukwe wa pwani ya Nungwi.

MSANII kutoka Nchini Oman akionesha umahiri wake wa kupuliza  zumari wakati wa Uzinduzi wa Tamasha la 17 la Mzanzibar lilifanyika katika ufukwe wa pwani ya Nungwi.
NGALAWA ya kwanza inayoongozwa na Nahodha wake Ramadhani Khamis ikiwasili katika ufukwe wa Nungwi, baada ya kushinda resi hizo, iliozijumuisha ngalawa 14 katika mashindano hayo 
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed akimkabidhi zawadi mshindi wa resi za Ngalawa Ramadhani Khamis.
WANAFUNZI wa Skuli ya Chekechea ya Kidutani  wakionesha maonesho ya mavazi mbalimbali katika maonesho ya uzinduzi wa Tamasha lililofanyika Viwanja vya Nungwi.





VIONGO wa meza Kuu wakishangilia Watoto wa skuli ya chekechea walipokuwa wakionesha mitindo ya mavazi wakipita na vazi la asili ya Zanzibar baibui la ukaya na kazu.


MWANAFUNZI waskuli ya Kidutani akionesha vazi la kanga  na akiwa akisuka ukili.
WATOTO wa skuli ya Kidutani wakicheza beni (mbwa kachoka) katika sherehe za uzinduzi wa Tamasha la Mzanzibar la 17 lililofanyika katika ufukwe wa pwani ya Nungwi.

KIKUNDI cha Sanaa wakicheza ngoma ya Msewe yenye asili yake kisiwani Pemba katika Tamasha la Mzanzibar.
                                                

No comments:

Post a Comment