Saturday, July 16, 2011

Jukwaa la wahariri wazuru kiwanda kipya cha sbl mjini moshi,wakwaana na wafanyakazi wake kimtanange ccp-moshi jioni ya leo.

Nako 2 Nako Soldia wakikamua usiku huu ndani ya Ushirika mjini Moshi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2011.








Mmoja wa wachezaji wa timu ya TEFF,akitaka kumchomoka mchezaji wa timu ya kampuni ya SBL lwenye moja ya uwanja wa CCP-Moshi jioni ya leo,katika mchezo huo timu hizo zimeibuka na sare sare ya bila kufingana.Mchezo wa timu hizo mbili umefanyika mara baada ya kumalizika kwa mkutano ya Jukwaa la Wahariri uliofanyika ndani ya hotel ya Kibo Palace,jijini Arusha leo
 Hatoki mtu hapa na wala hapangui mtu hapa.
Mgeni rasmi katika mpambano huo ambaye pia ni Mhariri mkuu wa Gazeti la Habari Leo Joseph Kulangwa, akisalimiana na mshabuliaji wa timu ya Serengeti Breweriers ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL Teddy Mapunda kabla mchezo huo haujaanza, kulia ni kocha wa timu ya Jukwaa la Wahariri  na mhariri wa Spoti Starehe Masoud Sanane.
Mshabuliaji wa timu ya Serengeti Breweriers ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL Teddy Mapunda akiongoza timu yake kupeana mkono wa heri kabla mchezo huo kuajaanza jioni ya leo kwenye moja ya uwanja wa CCP-Moshi.
 Kikosi cha timu ya SBL katika picha ya pamoja jioni ya leo.
 Timu ya Jukwaa la wahariri kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja.
Bwa.Titus Gitonga mabye ni mmoja wa wafanyakazi waandamizi wa kiwanda hicho kipya akitoa maelekezo kwa Wahariri wa Vyombo vya habari mbalimbali wapatao 80 kutoka Tanzania Bara na Visiwani kabla ya kuingia ndani ya kiwanda hicho na kujionea namna kiwanda hicho kinavyofanya kazi jioni ya leo mjini Moshi,kushoto kwakwe ni Mkurugenzi wa Mawasiliano,Teddy Mapunda.
Pichani juu na chini Wahariri wakielea kuangalia mitambo ya kiwanda hicho pamoja na namna kinavyozalisha bidhaa zake.

 Bwa.Titus Gitonga kutoka SBL akitoa maelezo kuhusiana na moja ya mashine inavyofanya kazi.
 Pichani namna uzalishaji wa bia unavyofanyika.
Mmoja wa wafanyakazi wa SBL akifafanua jambo mbele ya Wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali,ambao wamemaliza mkutano wao wa Jukwaa la Wahariri uliokuwa ukifanyika leo jioni,na baadaye Wahariri hao waliombwa kutembelea kiwanda kipya cha bia cha SBL kilichopo mjini Moshi na baadaye kutoana jasho na kipute.
 Pichani juu na chini ni wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwa kazini jioni ya leo.


No comments:

Post a Comment