Friday, June 3, 2011

FILAMU MPYA YAZINDULIWA LEO JIJINI DAR


Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Filamu ya CHUMO,Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dr. Haji Mponda akitoa hotuba ya uzinduzi wa Filamu hiyo inayoelezea athari za ugonjwa wa Malaria,Uzinduzi huo umefanyika usiku huu katika hoteli ya Movenpick jijini Dar.

Mtengenezaji Kiongozi wa Filamu hiyo,Jordan Riber akizungumza na vyombo vya habari kabla ya uzinduzi wa filamu hiyo katika hoteli ya Movenpick usiku huu.

Mkuu wa Mradi wa COMMIT,Rob Ainslic akizungumza katika uzinduzi huo usiku huu.

Meneja wa Mipango wa Mradi wa COMMIT,Waziri Nyoni akiwafafanulia jambo waandishi wa habari (hawapo pichani)kabla ya uzinduzi wa Filamu ya CHUMO inayoelezea athari za ugonjwa wa Malaria nchini,Katika hoteli ya Movenpick jijini Dar usiku huu.

Stelingi wa Fimumu hiyo,Jokate Mwegelo akizungumza na waandishi wa habari namna alivyoweza kufikisha ujumbe kwa jamii juu ya ugonjwa Malaria.

Mkuu wa Masoko na Ushirikiano wa Benki ya Stanbic,Abdallah Singano akiongea na Waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na ushirika wao katika Mpango wa kudhibiti malaria kwenye ujauzito wakati wa uzinduzi wa filamu mpya inayoelezea athari za ugonjwa huo katika jamii.

Mgeni Rasmi akiwasili.

Wadau wa Filamu,toka kulia ni Cloud,JB na Dr. Cheni wakiwakilisha ndani ya Movenpick usiku huu.

Mtengenezaji Maarufu wa Filamu za Kiafrika zikiwemo NERIA na YELLOW CARD,John Riber (kulia) akiwa na Dada Jackie Karanja.

John Riber akibadilishana mawazo na Muwakilishi wa USAID hapa nchini,Robetr Cunnen.

Mtengenezaji Kiongozi wa Filamu ya CHUMO,Jordan Riber (kati) akimuelezea Ankal juu ya Filamu hiyo inayoelezea athari za ugonjwa wa malaria katika jamii hapa nchini.kushoto ni baba wa Jordan ambaye pia ni mtengenezaji wa filamu wa siku nyingi,John Riber.

Kubadilishana mawazo.

Wadau.

Wageni waalikwa toka sehemu mbali mbali walihudhulia uzinduzi huo uliofanyika usiku huu katika hoteli ya Movenpick jijini Dar..

pia unaweza kutembelea katika mtandao wa filamu hiyo
kwa kubofya link hiyo.



No comments:

Post a Comment