Saturday, May 7, 2011

Orodha kamili ya wanamichezo bora wa 2010

Riadha
1. Wanaume: Marco Joseph- Alishika nafasi ya nne katika mbio za meta 10,000 michuano ya Jumuiya ya Madola New Delhi, India.

2.Wanawake: Mary Naali –Alikuwa Mtanzania pekee aliyefuzu mashindano ya dunia ya junior yaliyofanyika Canada na kuwa katika kumi bora.
-Alishiriki Safari International Half Marathon-Arusha na kushika nafasi ya pili
-Alishiriki Wachau Int Half Marathon Austria na kuwa wa kwanza akiweka rekodi yake mpya na nzuri zaidi kwa mwaka wote wa 2010 ya saa 1:12:16.
WAVU
1: Wanaume: Kevin Peter
-Ni mchezaji wa Magereza Wanaume. Aliipa ubingwa wa Muungano timu ya Magereza mwaka 2010
-Alikuwa mchezaji nyota wa michuano hiyo.
-Alichangia ubingwa wa vyuo timu yake ya IFM alikokuwa akisoma.
-Alichanguliwa Mchezaji Bora (MVP) wa Kombaini ya Afrika Mashariki na Kati akiwa pia ni kocha kitaaluma wa mchezo mwenye cheti cha ukocha Level 1.

2: Wanawake: Hellen Richard Mwegoha (Magereza Wanawake).
Ni nahodha wa Magereza aliyewaongoza wenzake kutwaa mfululizo ubingwa wa Tanzania Bara.
-Aling’ara katika mashindano ya wavu Bara na Muungano mwaka jana.
-Pia ni nahodha wa timu ya taifa.
Netiboli
Mwanaid Hassan (JKT Mbweni)
-Aliiwezesha timu yake ya JKT Mbweni kuibuka bingwa ligi daraja la kwanza 2010
-Aliibuka mfungaji bora katika michezo ya ligi daraja la kwanza 2010
-Aliiwezesha timu ya Mkoa wa Temeke kuibuka bingwa wa Taifa Cup 2010
-Aliibuka mfungaji bora wa michuano ya Taifa Cup 2010
-Aling’ara katika mashindano ya Singapore mwaka 2010 akiwa ni mmoja kati ya wafungaji bora
-Alikuwa Mfungaji Bora katika mashindano ya nchi za Afrika yaliyofanyika Afrika Kusini mwaka 2010

Kikapu
1:Wanaume: George Otto Tarimo (Savio-DSM)
Mashindano aliyocheza: RBA, NBL, Muungano, Majiji ya Afrika Mashariki, Klabu Bingwa Kanda ya Tano

Mafanikio: Mzuiaji Bora Majiji ya A/Mashariki, Amesaidia timu yake kutwaa ubingwa wa vikombe vitatu na kuwa Mchezaji Bora RBA, NBL na Muungano.

1. Wanawake : Faraja Malaki (Jeshi Stars DSM).

Mashindano: RBA, NBL, Majiji ya A/Mashariki, Klabu Bingwa Kanda ya Tano
Mafanikio:
Mchezaji Bora wa Ligi ya RBA na ameisaidia timu yake kuwa bingwa wa RBA.
Amecheza NBL kwa kiwango cha juu na kuisaidia timu yake kuwa Mabingwa na Mchezaji Bora.
Pia ameisaida timu yake kutwaa kombe la Muungano na kuwa mchezaji bora

SOKA
Wanaume: 1: Shadrack Nsajigwa-Yanga
--Aliisaidia timu ya Yanga kushika nafasi ya pili Ligi Kuu 2009/2010
--Aliisaidia timu ya Taifa ya Tanzania Bara kutwaa Kombe la Chalenji baada ya kulikosa kwa miaka 16.
-Bao lake la penalti mchezo wa fainali kati ya Tanzania Bara na Ivory Coast ndilo lililoipa ubingwaTanzania Bara.
-Alionesha uwezo mkubwa katika michuano ya Chalenji –Alikuwa Mchezaji Bora wa Mashindano ya Chalenji.

2: Wanawake: Asha Rashid
-Alitoa mchango mkubwa kufanikisha Twiga Stars ifuzu fainali za Afrika kwa wanawake
1. Ngumi za kulipwa: Karama Nyilawila
We have picked Karama Nyilawila as our professional boxer for the year 2010, thus qualify to contest for the best sports personality of the year award 2010.

The pugilist is the World Middleweight title holder recognized by World Boxing Federation (WBF). He won the title in Prague, Czech Republic on 3rd day of December 2010 against Albanian Kreshnik Qato on points.


8: Ngumi za ridhaa: .Selemani Kidunda
-Alipata medali ya shaba katika mashindano ya tano ya ngumi ya Jumuiya ya Madola New Delhi, India.
-Alipata medali ya dhahabu katika mashindano ya Taifa ya klabu bingwa ya Taifa Julai 2010
-Alipata medali ya dhahabu katika mashindano ya Taifa ya bingwa wa mabingwa
-Alishiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola New Delhi, India hakupata medali.

9: Baiskeli
Wanaume: Hamis Clement:
-Alikuwa mshindi wa kwanza mashindano makuu ya riadha ya Vodacom 2010 Kilometa 190 yaliyofanyika Mwanza
2: Wanawake:
1:Sophia Anderson-Alikuwa mshindi wa kwanza mashindano makuu ya riadha ya Vodacom 2010 Kilometa 80 yaliyofanyika Mwanza

10:Kriketi
Wanaume: Kassim Nassor
-Helped Tanzania finish fourth in the last year’s ICC World League Division 4 in Italy
-Won Man of the Match award in the ICC World League Division 4 match against Cayman Island
-Led his club, Academy Boys, to win the last year’s Mwalimu Nyerere Memorial Cup tournament
-Helped his team, Twiga Warriors, emerge champions of this year’s Advanced Players League (APL)
-Won the best all rounder award in this year’s APL
Wanawake: Mariam Said
-Helped the national U-19 women cricket team reach the final of the last year’s East Africa U-19 women championship played in Dar es Salaam
-Was the second best all rounder in the last year’s East Africa U-19 women championship played in Dar es Salaam
-Helped Zanaki Secondary School cricket team emerge champions of the TCA Schools league last year.

11: MWANAMICHEZO BORA CHIPUKIZI
Lilian Sylidion-Filbert Bayi
-Aling’ara katika mashindano yaliyofanyika Singapore, ambapo Taifa Queens ilishika nafasi ya tatu kuwania kufuzu michezo ya dunia.
-Aliibuka Mchezaji Bora wa mashindano hayo ya kimataifa ya Singapore.
-Ni mchezaji wa timu ya Filbert Bayi ya mkoani Pwani.

12: MWANAMICHEZO BORA WA NJE ANAYECHEZA TANZANIA
Emmanuel Okwi: Ametoa mchango mkubwa kwa Simba kutwaa ubingwa 200/2010
-Aling’ara mwaka 2010 akichezea Simba michezo mbalimbali.

13:MWANAMICHEZO BORA WA TANZANIA ALIYEPO NJE
Hasheem Thabeet: Amekuwa mstari wa mbele kwa kushiriki katika shughuli za kijamii amechangia ujenzi wa shule za sekondari mkoa wa Pwani kama shule ya Hanasif, Mkuraga.

Amekuwa Balozi wetu nchi za nje ameshiriki katika mipango mbalimbali ya kusaidia huduma za afya na elimu kwa kushirikina na wadau wengine huko Marekani kwa manufaa ya Tanzania.

Agosti mwaka 2010 aliendesha kliniki ya vijana wadogo chini ya umri wa miaka 17, karibu vijana 350 Dar es salaam na kutoa vifaa vya michezo kwa wachezaji wote hao, pia aliandesha kliniki nyingine huko Senegal kwa vijana toka bara zima la Afrika, ambapo Mtanzania Alpha Kisusi nae alishiriki.

Hasheem aliendesha mafunzo kama hayo huko China, Taiwani n.k.
Aliandaa Hasheem Thabeet Basketball Bonanza la kuhamasisha vijana kwa kucheza na timu zote za Dar es salaam, shule za sekondari Dar es Salaam na timu za mitaani kwa siku mbili

14; Judo: Masoud Amour Kombo
-Alichaguliwa Mchezaji Bora wa Judo Afrika Mashariki mwaka 2010
-Alitwaa medali mbili za dhahabu kwa kategoria mbili tofauti mashindano ya Afrika Mashariki mwaka 2010.
Amekuwa akipata medali za dhahabu na kuibuka Mchezaji Bora wa Judo kwa miaka mitatu mfululizo.
Pia alipata medali ya dhahabu katika mashindano ya wazi ya judo mwaka 2010.
Amekuwa bingwa wa judo uzani wa Kilogramu 1000 kwa mwaka 2010 na kuweka rekodi ya kutwaa ubingwa huo kwa mwaka wa nne mfululizo.

15: Gofu:
WANAWAKE
1. Hawa Wanyeche- Ni mchezaji kutoka Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam. Nahodha wa timu ya Taifa ya gofu ya Wanawake na mchango mkubwa kuwezesha timu ya taifa kuweka historia ya kushika nafasi ya pili kwenye michuano ya Kombe la Challenge la Gofu la Wanawake Afrika ( All African Challenge Trophy) yaliyofanyika Abuja, Nigeria Novemba, 2010 na kuipa Tanzania heshima kubwa.
Alishika nafasi ya tano kati ya zaidi ya wachezaji 150 kwenye michuano ya wanawake ya Nigerian Open dhidi ya wachezaji wakali Afrika. Alitwaa taji la mashindano ya wanawake ya Coast Open, Mombasa, Kenya Agosti na taji la Wanawake Dar Open Oktoba. Mafanikio yake katika mashindano ya ndani na nje yamemwezesha kupewa tuzo ya Mchezaji Gofu Bora wa Mwaka Mwanawake (Best Lady Golfer of the Year) na Chama cha Gofu Tanzania (TGU) mwaka jana.

WANAUME

2.Frank Roman- Mchezaji wa Klabu ya Gymkhana Moshi.
-Ni nahodha wa timu ya taifa ambaye amekuwa na mwaka mzuri katika mashindano ya ndani. Februari mwaka 2010 Moshi aliibuka bingwa wa michuano ya taifa ya gofu ya Northern Province Open na kuwashinda wachezaji nyota wa timu ya taifa ya Kenya ikiwa ni ushindi wa kwanza kwa Mtanzania mbele ya Wakenya nyumbani. Mafanikio yake kwa kipindi cha mwaka jana katika mashindano tofauti ya taifa yalimuwezesha kupewa Tuzo ya Mchezaji Gofu Bora wa Mwaka wa Kiume (Best Golfer of the Year) na Chama cha Gofu Tanzania (TGU).

16: TUZO YA HESHIMA KWENYE MICHEZO:
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa-ametoa mchango mkubwa kufanikisha ujenzi wa uwanja wa Taifa Dar es Salaam, wakati akiwa Rais.
-Uwanja huu ni sifa kubwa na kielelezo cha namna anavyowathamini wanamichezo.

17: MWANAMICHEZO BORA WA TANZANIA MWAKA 2010 NI- MCHEZA NETIBOLI MWANAID HASSAN.

WANAMICHEZO WA MIAKA ILIYOPITA
2009-MWANAID HASSAN-NETIBOLI
2008-MARY NAALI-RIADHA
2007-MARTIN SULLE-RIADHA
2006-SAMSON RAMADHAN-RIADHA.


VIGEZO:
1.Mchango wa Mchezaji husika kufanikisha ushindi kitaifa/kimataifa
2.Nidhamu Bora ya Mchezaji Ndani na Nje ya Uwanja pamoja na moyo wa kizalendo
3.Uhusiano mzuri wa Mchezaji na Jamii/Kuwa mfano wa kuigwa kimaendeleo
4.Kipaji cha pekee kwa Mchezaji
5.Mwenye mvuto, mchagizaji, mhamasishaji na mwenye ushawishi kwa jamii.

Sifa ya Ziada
1.Awe hatumii dawa zisizoruhusiwa michezoni/dawa za kulevya

No comments:

Post a Comment