Saturday, April 23, 2011

TAMASHA LA VODACOM SHUFFLE DANCE LAFANA UFUKWE WA SUNRISE DAR


Helkopta ikipita kandokando ya Bahari ya Hindi eneo la Ufukwe wa Sunrise Resort juzi, wakati wa Tamasha la Vodacom la ‘Shuffle Dance’, lililoandaliwa maalum na kampuni hiyo ya Vodacom kwa ajili ya kuweka na kuvunja rekodi ya dunia na kuweka kumbukumbi katika kitabu cha Matukio makubwa Duniani ‘Guinness Book Records’.Tamasha hilo lilifanyika jana, kwenye Ufukwe wa Hotel ya Sunrise Kigamboni Dar es Salaam.
Wasanii mbalimbali na vijana waliojitokeza kushiriki Tamasha la Vodaco ‘Shuffle Dance’, akicheza staili moja kwa pamoja wakati wa Tamasha hilo lililofanyika jana kwenye Ufukwe wa Hoteli ya Sunrise Kigamboni Dar es Salaam, likiwa na lengo la kuvunja na kuweka rekodi ya Dunia katika kitabu cha Matukio Makubwa yanayotokea Duniani, ‘Guinness Book Records’. Tamasha hilo liliandaliwa na kampuni ya simu za mkononi Vodacom Tanzania.

Baadhi ya watu waliojitokeza kushuhudia Bonge la staili za Tamasha hilo Shuffle Dance.

Eti huyu ni Dada Rose (kulia) akiwa na shosti wake 'Mtasha', wakipiga picha za kumbukumbu ufukweni hapo.

Twende kazi na staili za pamoja hapa huku wakirekodiwa
kwa ajili ya mambo fulani ya hapo baadaye.

Mkuu wa Udhamini wa Kampuni ya simu za mkononi Vodacom Tanzania, George Rwehumbiza, akizungumza na waandishi kufafanua juu ya Tamasha hilo.

Muongozaji wa Tamasha hilo wakati wa kurekodi akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa zoezi hilo.

Kitu kikitua kwenye Ufukwe hu. Picha zote na Sufiani Mafoto.

No comments:

Post a Comment