Friday, October 19, 2018

DKT TIZEBA AWATAKA WAKULIMA WA NYANYA IRINGA KUCHANGAMKIA FURSA YA UZALISHAJI SOKO LIPO


Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), (katikati) akikagua mtambo wa kuchakata nyanya akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard kasesela (Kulia) wakikagua kiwanda cha Darsh kilichopo Kijijini Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Iringa jana Alhamisi Octoba 19, 2018. Mwingine Pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha Darsh Ndg Bhadresh Pandit. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wakifatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), alipotembelea na kukagua kiwanda cha Darsh jana Alhamisi Octoba 19, 2018.
Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), (katikati) akikagua mitambo ya kuchakata nyanya akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard kasesela (Kulia) wakikagua kiwanda cha Darsh kilichopo Kijijini Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Iringa jana Alhamisi Octoba 19, 2018.
Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), akikagua mitambo ya kuchakata nyanya akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard kasesela wakikagua kiwanda cha Darsh kilichopo Kijijini Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Iringa jana Alhamisi Octoba 19, 2018.

Na Mathias Canal-WK, Mseke-Iringa

Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), amewataka wakulima wa nyanya Mkoani Iringa kuchangamkia fursa ya kuongeza uzalishaji wa nyanya ili kuakisi uhitaji wa viwanda vya nyanya ikiwa ni pamoja na kiwanda cha Darsh chenye uwezo wa kusindika Tani 250 za nyanya kwa siku.

Waziri Tizeba ametoa mwito huo jana Octoba 18, 2018 wakati akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda cha Darsh kilichopo Kijijini Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.

Kiwanda hicho kinafanya shughuli za ukusanyaji wa nyanya kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Iringa na mikoa ya jirani na kufanya usindikaji wa nyanya ambapo hupeleka kiwanda cha Arusha kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na nyanya ambazo huuzwa ndani na nje ya nchi.

Waziri Tizeba, aliwataka wakulima hao kujiunga kuanzisha kikundi cha ushirika ili kuwa na urahisi wa mikopo ili kuwezesha uwezo wa uwekezaji kupitia kilimo cha umwagiliaji kitakachoongeza tija katika kipato chao na jamii kwa ujumla.

“Wakulima wa nyanya hapa Igwachanya na hata katika maeneo mengi nchini wanalima kwa kutegemea mvua na uzalishaji huwa mdogo na usiokidhi mahitaji ya soko hivyo nawasihi kuongeza uzalishaji wa nyanya kwani soko la uhakika lipo” Alikaririwa Dkt Tizeba

Kadhalika, Waziri wa kilimo aliutaka uongozi wa kiwanda hicho kuongeza wigo wa ununuzi wa nyanya katika mikoa mingine ya uzalishaji ikiwemo mkoa wa Dodoama na Singida.

Awali akisoma taarifa ya kiwanda hicho mbele ya mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha Darsh Ndg Bhadresh Pandit ameishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuhimiza sera ya uchumi wa viwanda kwa kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na kuendelea kuzitafutia ufumbuzi changamoto chache zinazojitokeza hivyo kuendelea kulinda maslahi mapana ya Taifa.

Alisema uanzishwaji wa kiwanda hicho ulitokana na ushawishi uliopatikana kutoka kwenye muunganiko wa wajasiliamali vijijini (MUVI) na Techno Serve walipotembelea kiwanda cha Darsh Mkoani Arusha.

Naye Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela alimpongeza waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba kwa kutenga muda wake na kukubali kufanya ziara Wilayani Iringa ili kubaini changamoto zinazowakabili wakulima wa nyanya nchini.

No comments:

Post a Comment