Friday, June 30, 2017

Viongozi wa Dini kanda ya Ziwa Wabebeshwa mzigo, Utunzaji wa Mazingira Ziwa Victoria

Mkuu wa mkoa wa Mara Dkt. Charles Mlingwa, akifungua kikao hicho, pembeni kulia ni Mratibu wa LVEMP Bw. Omari Myanza.
Na Atley Kuni,  Mwanza.

Serikali mkoani hapa, imewapa jukumu kubwa viongozi wa dini kutoka baadhi ya mikoa ya kanda ya ziwa kuhakikisha wanakuwa bega kwa bega katika kulitunza ziwa Viktoria na Maliasili zake ili liweze kuwa tegemeo kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Akifungua Semina ya siku moja mkoani hapa Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, na risala yake kusomwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt. Charles Mlingwa, Mongella amesema, viongozi wa dini wanalo jukumu kubwa kwani wao husimamia imani za watu.
Baba Askofu Michael Msonganzila wa Jimbo katoliki Musoma Mkoani Mara akiongea na Waandishi wa habari nje ya Mkutano huo kuelezea umuhimu wa mazingira.

“Ninyi Viongozi wa dini dhima mliyonayo ndani ya jamii ni kubwa sana na chochote mtakacho waelekeza waumini wenu lazima waweze kukitekeleza, hivyo niwaombe sana viongozi wangu tulilinde ziwa viktoria kwa jitihada zetu zote’’ alisema Mongella.

Aidha Mongella amesema kuwa, kuwepo kwa Ziwa Victoria ni fursa ya uendelezaji ya kauli mbiu ya “Tanzania ya Viwanda” ambayo Serikali ya awamu ya Tano inasisitiza, “Ziwa hili linasaidia upatikanaji wa rasilimali zinazotumika kwa matumizi ya nyumbani na viwandani, usafiri na usafirishaji na uzalishaji wa nishati ya umeme Hivyo basi hatuna budi kuhifadhi mazingira ya Ziwa na Bonde lake” amesisitiza Mkuu huyo wa mkoa.

Kwa upande wao, viongozi wa dini wakiongea wamesema, wao wanatambua na hata vitabu vya dini vinaelekeza juu ya mwanadamu anachopaswa kufanya katika kulinda mazingira ikiwepo ziwa Viktoria.
Sheik Hassan Kabeke, akiafafnua jambo kwa waandishi wa habari nje ya Warsha hiyo namna suala la mazingira linavyo tajwa katika Kuran tukufu.

Mwenyekiti mwenza wa Kamati ya amani ya madhehebu ya dini katika Mkoa wa Mwanza, Sheik Hassan Kabeke, amesema katika Uislam na hususan ni katika mafundisho ya Mtume Muhama S.A.W, inafafanua juu ya mito miwili yaani mto Nile na Furabu ambayo mtume aliipitia huku akisema kwamba, Mto Nile ambao unafungamanishwa na Ziwa Viktoria Mtume amesisitiza kuyatunza mazingira, “Katika kupanda miti kwenye uislamu mtu hupata thawabu, tunaimani kabisa kwamba kila mmoja wetu akitunza mazingira ni sehemu ya Ibada, amesema Kabeke.

Naye Baba Askofu Michael Msonganzila wa Jimbo Katoliki la Musoma, kwa upande wake amesema kwa habari ya mazingira, tunaona ni jukumu la jamii nzima bila kujali itikadi zetu “ Kukutana kwetu hapa tunataka kuangalia nikwa namna gani tutaziangazia sababu za kiuchumi na kijamii, alisema Msonganzila na kuongeza kwamba kwa sasa wao katika Mkoa wa Mara wanayo kampeni kwenye eneo la Serengeti ambayo wanaendelea kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa Utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya hali ya nchi.
Mratibu wa LVEM Akitoa maelezo ya awali kabla yakuanza kwa Warsha hiyo ilikutanisha Viongozi wa Serikali na Dini katika baadhi ya Mikoa ya kanda ya ziwa (Picha zote na Ofisi ya mkuu wa Mkoa Mwanza).

Mradi wa Hifadhi ya Mazingira wa Ziwa Victoria (LVEMP II) utakamilika mwezi Disemba, 2017, aidha warsha hiyo ni kati ya warsha nne zilizoandaliwa na Mradi kwa madhumuni ya kukusanya maoni ya wadau ambayo yatawezesha kuandaa awamu ijayo ya Mradi inayotarajiwa kuanza kutekelezwa kuanzia mwaka 2018.

Kikao hicho kimewakutanisha Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa pamoja na Viongozi wa dini kutoka mikoa ya Mwanza, Geita, Kagera, Simiyu na Mara.
Baadhi ya Viongozi wa dini kutoka mkoa wa kagera wakiwa katika Warsha hiyo.

TANZANIA NA NORWAY KUSHIRIKIANA KATIKA MASUALA YA SIASA NA DIPLOMASIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufalme wa Norway, Mhe. Borge Brende wakiweka saini Mkataba wa Makubaliano kuhusu kushirikiana katika Mashauriano ya Kisiasa na Kidiplomasia kati ya Tanzania na Norway.Ttukio hilo lilifanyika jijini Dar Es Salaam kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere na kuhudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Norway mwenye makazi yake nchini Sweden, Mhe. Dora Msechu, Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Hanne Marie Kaarstad, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya, Bi. Mary Matari, pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga (hawapo pichani). 
Waheshimiwa Mawaziri wakibadilishana mikataba mara baada ya kuweka saini 
Dkt. Mahiga akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza zoezi la uwekaji saini na Mgeni wake. 
Mhe. Brende naye akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa Habari. 
Balozi wa Tanzania nchini Norway mwenye makazi yake nchini Sweden, Mhe. Dora Msechu (wa pili kutoka kulia), Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Hanne Marie Kaarstad (wa kwanza kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya, Bi. Mary Matari (wa kwanza kushoto) pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga wakifuatilia kwa makini mkutano wa waandishi wa habari na Mawaziri wa Mambo ya Nje. 
Sehemu ya ujumbe ulioambatana na Waziri wa Norway nao wakifuatilia mkutano wa waandishi wa habari na Mawaziri wa Mambo ya Nje. 
sehemu ya waandishi wa habari wakiwasikiliza kwa makini Mawaziri walipokuwa wakiendelea kuzungumza (hawapo pichani). 

 


Tanznaia na Norway kushirikiana katika masuala ya siasa na diplomasia

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga ameeleza kuwa kusainiwa kwa Mkataba wa Makubaliano (MoU) kuhusu kushirikiana katika Mashauriano ya Kisiasa na Kidiplomasia kati ya Tanzania na Norway kumefungua sura mpya ya mahusiano kati ya nchi hizo mbili. 

Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar Es Salaam wakati anaongea na waandishi wa habari baada ya shughuli ya uwekaji saini wa makubaliano hayo aliyoifanya kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway, Mhe. Borge Brende kukamilika.

Alisema kusainiwa kwa MoU hiyo kutazifanya nchi hizo kuwa na mahusiano ya karibu zaidi katika kubadilishana mawazo kuhusu masuala ya kisiasa na kidiplomasia ambayo kimsingi yalikuwepo tokea zamani lakini leo yamerasimishwa. 

Mhe. Mahiga amewambia wanahabari kuwa Tanzania na Norway zimekuwa zikishirikiana kiuchumi, kiteknolojia na kijamii kwa takribani miaka 55 sasa. Baadhi ya maeneo aliyoyataja ambayo nchi hizo zimekuwa zikishirikiana katika kipindi hicho ni pamoja na uzalishaji wa nishati ya umeme hususan vijijini, afya, elimu, kilimo na utunzaji wa misitu. 

Mhe. Mahiga aliendelea kueleza kuwa katika kikao chao, wamejadili maeneo mapya ya ushirikiano yakiwemo utunzaji wa mazingira na kusisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano wa sekta binafsi za nchi hizo mbili kinyume na awali mahusiano zaidi yalikuwa baina ya Serikali mbili.

Waziri Mahiga ameishukuru Norway kwa jitihada zake ziliozasaidia uvumbuzi na uchimbaji wa gesi asilia nchini kupitia kampuni ya Statoil ambayo imewekeza nchini mtaji mkubwa kuliko mahali popote Afrika.

Alihitimisha hotuba yake kwa kusema kuwa Tanzania itaendelea kufaidika kwa kiasi kikubwa na ushirikiano wake na Norway kwa kuwa nchi hiyo ina utajiri mkubwa katika sekta ya mafuta misitu na teknolojia ya hali ya juu katika sekta mbalimbali.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway alieleza kuwa Norway imekuwa ikishirikiana na Tanznaia katika sekta za maendeleo tokea mwaka 1964 na kuahidi kuwa nchi yake itaendelea kuisaidia Tanzania hadi hapo nchi hiyo itakapokuwa na uwezo wa kugharamia miradi yake yenywe. 

Waziri Borge kabla ya kuondoka nchini leo join, atashiriki uzinduzi wa programu ya kushirikiana katika masuala ya kodi na uzinduzi wa awamu ya pili ya programu ya kuendeleza mafuta(oil for development program) utakaofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro. 


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 
Dar es Salaam, 30 Juni 2017

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA UMOJA WA WANAMICHEZO WA MPIRA WA MIGUU KUTOKA FC GRACE UNITED STATES LEO OFISINI KWAKE MJINI DODOMA.

Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akizungumza pale ugeni kutoka Umoja wa Wanamichezo wa Mpira wa Miguu kutoka FC GRACE UNITED STATES ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. wa pili kulia ni Mwenyeji na kiongozi wa Msafara Bishop Oscar John.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikat) akimsikiliza Mheshimiwa William Ngeleja akizungumza wakati Umoja wa Wanamichezo wa Mpira wa Miguu kutoka FC GRACE UNITED STATES ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akimsikiliza Bishop Oscar John (aliesimama) akizungumza, pale ugeni kutoka Umoja wa Wanamichezo wa Mpira wa Miguu kutoka FC GRACE UNITED STATES ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) akizungumza na ugeni kutoka Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania ulioongozwa na Rais wa Chama hicho Ndg. Mwadini Jecha (katikati) na Mratibu wa Mawasiliano Ndg. Anne kilimo (kushoto) uliomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Washindi wa Medali za Dhahabu katika Mashindano ya kimataifa ya Mazingira na Sayansi yaliyofanyika hivi karibuni nchini Marekani. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Shule ya Wavulana ya Feza Ndg. Ibrahim Rashid, anaefuata ni Ndg. Rashid Kikwete, kulia ni Mhe. Hawa Ghasia, wa pili kulia ni Ndg. Kassi Nkamia na watatu kulia ni Ndg. Abdallah Rubeya, waliotembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na ugeni kutoka Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania ulioongozwa na Rais wa Chama hicho Ndg. Mwadini Jecha (kushoto waliokaa) baada ya kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) akimsikiliza Rais wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania Ndg. Mwadini Jecha (katikati) pale ugeni kutoka Chama hicho ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, kushoto ni Mratibu wa Mawasiliano Ndg. Anne kilimo.

MAEGESHO YA KIVUKO LINDI KUKAMILIKA MWEZI NOVEMBA MWAKA HUU

Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS). Mkoa wa Lindi,Eng. Issack Mwanawima (mwenye koti la draft), akimweleza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa maegesho hayo, Mkoani humo, wakati Waziri huyo alipotembelea mradi huo hivi karibuni.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), akiangalia ujenzi wa wa maegesho ya kivuko unaojengwa katika mkoa wa Lindi alipotembelea mradi huo hivi karibuni. Mradi huo utahusisha maegesho ya kivuko na ujenzi wa mita 150 za barabara ya lami upande wa Kitunda.
Tinga Tinga likiendelea na ujenzi wa maegesho ya kivuko Mkoani lindi. Ujenzi wa maegesho hayo unatarajiwa kukamilika mwezi Novemba mwaka huu.
Meneja wa Bandari ya Mtwara, Eng. Juma Kijavara (katikati), akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), eneo la gati ya Lindi ambalo litatakiwa kuchimbwa ili kuongeza kina cha gati hilo, alipotembelea gati hiyo hivi karibuni.
Meneja wa Bandari ya Mtwara, Eng. Juma Kijavara (katikati), akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), wakati Waziri huyo alipotembea alipotembelea gati la Lindi kuona hatua mbalimbali za utekelezaji wa upanuzi wa gati hiyo hivi karibuni.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akienda kuangali sehemu ya kwanza ya upanuzi wa gati la Lindi ambalo kwa sasa linatakiwa kuongezewa kina ili meli kubwa ziweze kutia nanga.



…………………..

Serikali imesema ujenzi wa maegesho ya kivuko Mkoani Lindi utakamilika mwezi Novemba mwaka huu ili kurahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo kwa wakazi wa eneo la Kitunda Mkoani Lindi.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alipokagua maendeleo ya ujenzi wa maegesho hayo na kusema ujenzi huo umegharimu kiasi cha Tsh, bilioni 1.8 ambazo zitahusisha maegesho ya Kivuko na kujenga barabara ya kiwango cha lami mita 150 upande wa Kitunda Mkoani Lindi.

‘Tuliahidi na sasa tunatekeleza, nimefurahi kuona ujenzi unaendelea vizuri na ninawahakikishia mwezi Novemba tutakuja kuzindua kivuko’ alisema WazirI Profesa Mbarawa.

Aidha,Waziri Mbarawa amemtaka Mkandarasi anaejenga magesho hayo kuzingatia thamani ya fedha wakati wa ujenzi wake ili mradi huo uweze kudumu kwa muda mrefu.

‘hakikisha unajenga maegesho haya kwa kuzingatia viwango tulivyokubaliana, hatutaki kuona kasoro mara tu baada ya mwezi mmoja, hizi ni fedha za walipa kodi na tunategemea miundombinu hii ikae muda mrefu’ alisisitiza Waziri Prof. MBARAWA.

Kwa upande wake Msimamizi wa Mradi huo, Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads), mkoa wa Lindi, Eng. Issack Mwanawima amemuhakikishia Waziri Profesa Mbarawa kuwa watasimamia mradi kwa kuzingatia viwango katika ujenzi huo na kuhakikisha unakamilika kama mkataba unavyosema.

Katika hatua nyingine Waziri Profesa Mbarawa amekagua maendeleo ya ujenzi wa Gati la Lindi na kusema kuwa Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kuongeza kina cha Gati hiyo mara baada ya kutokea changamoto ya upana wa Gati hiyo kuwa mdogo.

‘Baada ya kujenga sehemu iliyopo sasa tuligundua kuwa bandari inatakiwa kuongezwa kina hivyo tukalazimika kufanya usanifu upya ili tuongeze upana wa mita 60 mpaka 500kwa eneo lote vinginevyo meli zisingeweza kufunga nanga’ alisisita Waziri Prof Mbarawa.

Waziri Prof. MBARAWA aliongeza kuwa lengo la Serikali katika kufanya usanifu upya ni kuhakikisha Gati ya Lindi inakidhi mahitaji halisi na kuchochea uchumi wa mkoa huo.

Kwa upande Meneja Bandari ya Mtwara Eng. JUMA Kijavara amesema Mamlaka ya Bandari Nchini TPA imejipanga na iko katika hatua za mwisho za mazungumzo na Mkanadarasi ili aanze kazi hiyo.

Mradi wa upanuzi wa Gati la Lindi utahusisha miradi ya Gati hiyo, Bandari ya Lushungi pamoja na bandari ya Kilwa.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

DC MKURANGA AZINDUA JUKWAA LA UWEZESHAJI WANAWAKE WA WILAYA HIYO

MATUKIO KATIKA PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 57 MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO JUNI 30, 2017

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiongoza kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais(TAMISEMI) Mhe,Selemani Jafo akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha hamsini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Mwigulu Nchemba akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha hamsini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Isack Kamwelwe akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Naibu Waziri Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angeline Mabula akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Eng,Edwin Ngonyani akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe.George Simbachawene akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Mbunge wa Mafinga Mjini Mhe.Cosato Chumi akiuliza swali katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dk.Ashatu Kijaji akiteta jambo na Mbunge wa Karagwe Mhe.Innocent Bashungwa katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Shally Raymond akiuliza swali katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe.Dk Mary Mwanjelwa akiuliza swali katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Mbunge wa Bububu Mhe.Mwantakaje Juma akiuliza swali katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Washindi wa Medali za Dhahabu katika Mashindano ya Kimataifa ya Mazingira na Sayansi yaliyofanyika nchini Marekani Kutoka kushoto Ndg.Rashid Kikwete,Kassi Juma Nkamia na Abdallah Rubeya wakiwa bungeni kujifunza shughuli balimbali za Bunge.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Prof Jumanne Maghembe akimsikiliza Mbunge wa Vunjo Mhe.Eng.James Mbatia katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017. Picha Zote na Daudi Manongi- Dodoma

Megawati 5000 kupatikana 2021, Ni baada ya kukamilika kwa mradi wa Stieglers Gorge

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani ( wa pili kulia mbele) akimwongoza Waziri wa Maji, Nishati na Umwagiliaji kutoka Ethiopia, Dk. Seleshi Bekele (katikati mbele) kwenye ziara ya kukagua eneo la ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za maji la Stiegler’s Gorge, Rufiji mkoani Pwani katika ziara hiyo.
Na Greyson Mwase, Rufiji.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani amesema Tanzania inatarajia kupata umeme wa uhakika wa Megawati 5000 ifikapo mwaka 2021, mara baada ya kukamilika kwa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia  nguvu za maji katika maporomoko ya maji ya Mto Rufiji kwenye  eneo la Stiegler’s Gorge  lililopo  Rufiji mkoani Pwani ambao utaongeza umeme wa kiasi cha Megawati 2100 katika  gridi ya taifa.

Dk. Kalemani aliyasema hayo jana tarehe 29 Juni, 2017 katika ziara ya Waziri wa Maji, Nishati na Umwagiliaji kutoka  Ethiopia, Dk. Seleshi Bekele aliyeambatana na wataalam wa masuala ya ujenzi wa mitambo  ya kuzalisha umeme kwa kutumia maji kutoka  Ethiopia kwenye eneo  la mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji ya Stieglers Gorge wilyani  Rufiji mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani akishuka kwenye boti kwa ajili ya kuelekea kwenye eneo la Stieglers Gorge kutakapojengwa mradi huo.

Wengine walioshiriki katika ziara hiyo ni pamoja na wataalam wa masuala ya  umeme na ujenzi wa mabwawa kutoka Tanzania,  Shirika la Umeme  Tanzania (TANESCO) na Wizara ya Nishati na Madini.  Ziara  hiyo inafuatia maombi ya  Rais John Magufuli kwa Waziri Mkuu wa Ethiopia ya kutuma wataalam wa masuala ya ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za maji kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na  wataalam wa masuala ya umeme na ujenzi wa mabwawa kutoka Tanzania.

Dk Kalemani alisema kuwa kupatikana kwa umeme wa uhakika ifikapo mwaka 2021 kutachochea ongezeko la viwanda hivyo kuongezeka kwa fursa za ajira na biashara na kukuza uchumi wa nchi.
Alisema mradi huo mkubwa ni moja ya mikakati ya Serikali  kuhakikisha nishati inakuwa na mchango mkubwa katika  kufikia malengo  ya  Dira ya Maendeleo ya Taifa yenye lengo la kuhakikisha kuwa nchi inatoka katika orodha ya nchi maskini duniani na kuingia katika orodha ya nchi zenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Waziri wa Maji, Nishati na Umwagiliaji kutoka Ethiopia, Dk. Seleshi Bekele (kushoto) akieleza jambo kwa Mhaidrolojia Mwandamizi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Stanislaus Kizzy (kulia) katika ziara hiyo. Anayesikiliza katikati ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani.

Alisisitiza kuwa mbali na mradi huo mkubwa, serikali imeweka mikakati ya kutumia vyanzo vingine vya nishati kama vile Gesi, Makaa ya Mawe, Jotoardhi, Upepo ili kuhakikisha kuwa nchi inapata umeme wa uhakika. Akielezea mafanikio ya mradi huo mbali na upatikanaji wa umeme wa uhakika, Dk. Kalemani alisema kuwa mradi huo utachochea ukuaji wa shughuli za uvuvi katika mkoa wa Pwani.

Alitaja mafanikio mengine kuwa ni pamoja na kukuza sekta ya Utalii katika  mkoa wa Pwani pamoja na kuzuia mafuriko ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara katika mto Rufiji na kuathiri makazi  ya wakazi waishio pembezoni na mto huo. Akielezea hatua iliyofikiwa ya maandalizi ya ujenzi wa mradi huo mkubwa, Dk. Kalemani alisema baada ya timu ya wataalam kutoka Tanzania na Ethiopia kufanya ziara katika eneo la mradi hatua inayofuatia ni wataalam kukaa vikao mbalimbali kujadili namna bora ya kutekeleza mradi pamoja na kubadilishana uzoefu.
Mhaidrolojia Mwandamizi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Stanislaus Kizzy (kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Maji, Nishati na Umwagiliaji kutoka Ethiopia, Dk. Seleshi Bekele ( wa pili kushoto). Katikati ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani.

Alisema mara baada ya ujenzi wa mradi huo kukamilika, moja ya kazi zitakazofanywa ni pamoja na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme hadi Chalinze yenye urefu wa kilomita 200 na njia ya kusafirisha umeme kutoka  eneo la Mradi hadi  Singida yenye urefu wa kilometa 800.

Waziri Kalemani aliwataka wananchi na taasisi mbalimbali kuunga mkono  juhudi za Serikali  ya Awamu ya Tano  ikiwa ni pamoja na kulinda vyanzo vya maji  hususan katika mto Rufiji.
Wakati huohuo, katika  ziara hiyo Waziri wa Maji, Nishati na Umwagiliaji kutoka  Ethiopia, Dk. Seleshi Bekele alisema kuwa mradi huu mkubwa ni mzuri na unatekelezeka na kuongeza kuwa  Ethiopia ipo tayari kutoa ushirikiano mkubwa kupitia wataalam wake lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa mradi unafanikiwa na kukamilika kwa wakati.
Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga (kulia) akipokewa na Meneja Mkuu wa Hoteli ya Serena Mivumo River Lodge, Ellieta Mbisse (kushoto) mara bada ya kuwasili katika uwanja mdogo wa Stiegler’s Gorge, Rufiji mkoani Pwani kabla ya kuanza kwa ziara ya Waziri wa Maji, Nishati na Umwagiliaji kutoka Ethiopia, Dk. Seleshi Bekele aliyeambatana na wataalam wa masuala ya ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia maji kutoka Ethiopia pamoja na wataalam wa masuala ya umeme na ujenzi wa mabwawa kutoka Tanzania wakiongozwa na mwenyeji wao Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani akishuka kwenye helikopta, mara bada ya kuwasili katika uwanja mdogo wa Stieglers Gorge, Rufiji mkoani Pwani kabla ya kuanza kwa ziara ya Waziri wa Maji, Nishati na Umwagiliaji kutoka Ethiopia, Dk. Seleshi Bekele aliyeambatana na wataalam wa masuala ya ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia maji kutoka Ethiopia pamoja na wataalam wa masuala ya umeme na ujenzi wa mabwawa kutoka Tanzania.
Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga (kushoto) akielezea maandalizi ya mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za maji wa Stieglers Gorge kwa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Ethiopian Construction Design and Supervision kutoka Ethiopia, Dk. Negede Kassa (kulia) katika ziara hiyo.
Kipimo cha kupimia kina cha maji (water gauge) katika sehemu ya mto Rufiji uliopo katika wilaya ya Rufiji mkoani Pwani.
Waziri wa Maji, Nishati na Umwagiliaji kutoka Ethiopia, Dk. Sileshi Bekele ( wa tatu kushoto) akieleza jambo katika ziara hiyo.
Sehemu ya Mto Rufiji kutakapojengwa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za maji katika eneo la Stieglers Gorge wilayani Rufiji mkoani Pwani.
Waziri wa Maji, Nishati na Umwagiliaji kutoka Ethiopia, Dk. Seleshi Bekele (wa saba kulia) na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani (wa nane kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na timu ya wataalam kutoka Tanzania na Ethiopia katika ziara hiyo.