Friday, September 30, 2016

TASWIRA MBALIMBALI UZINDUZI WA DAWATI LA JINSIA ILOMBA JIJINI MBEYA

 Bendi ya Jeshi la Askari Magereza Likiongoza maandamano Kutokea Stendi ya Mabasi ya mzunguko maharufu kwa jina la Daladala Kabwe na kuelekea katika uwanja wa Ccm Rwanda Nzovvwe Jijini Mbeya kuajili ya kuzinduwa Jengo Moja lililo jengwa na Shirika la "UNICEF" Eneo la Ilomba Jijini Hapo kwa kazi maalum ya kuwasaidia watoto wanaofanyiwa vitendo vya kikatili na kuchukuliwa hatua kali za kisheria na Dawati Hilo la Kijinsia ambalo lipo chini ya Jeshi la Polisi Mkoa Wa Mbeya pamoja na Wadau wa Dawati la Jinsia.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla akifurahi Jambo wakati akihutubia katika uzinduzi huo wa Dawati la Jinsia Ulio fanyika katika Uwanja Wa Rwanda Nzovwe Jijini Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla mwenye Suti ya Bluu akikata Utepe kuashiria kuwa Kituo Hicho Kimeanza kufanya kazi rasmi na Hakita munea huruma yoyote Atakae husika na kubainika ni miongoni mwa waalifu wanao fanya Vitendo vya Kikatili kwa Watoto Ikiwemo Ubakaji na Kulawiti watoto Jeshi La Polisi kupitia Dawati la Jinsia Litawashughulikia Vilivyo Waalifu na kuwafikisha kwenye Vyombo Vya Sheria.
 Baadhi ya wadau wa Dawati la Jinsia wakiburudika kwa pamoja katika Uzinduzi huo Wa Dawati la Jinsia Ulio Fanyika Uwanja wa Rwanda Nzovwe Jijini Mbeya.

WAZIRI MKUU ATIMIZA AHADI YA KUHAMIA DODOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiwapungia akiwapungia wananchi wa Dodoma baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Septemba 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea ufunguo ikiwa ni ishara ya kukaribishwa Dodoma na Meya wa Manispaa ya Dodoma Jafar Mwanyemba katika mapokezi yaliyofanyika kwenye makazi yake , Mlimwa Septemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha ufunguo aliokabidhiwa na Meya wa Manispaa ya Dodoma, Jafar Mwanyemba (kushoto) kuashiria kupokewa rasmi kwenye manispaa hiyo. Makbidhiano hayo yalifanyika kwenye makazi yake eneo la Mlimwa Septemba 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wazee wa Dodoma baada ya kukaribishwa kimira na wazee hao Septemba 30, 2016.
Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa akizawadiwa kimira na wanawake wa Dodoma ikiwa ni ishara ya kumkaribisha karika Manispaa hiyo, Septemba 30, 2016.
Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa akizawadiwa kimira na wanawake wa Dodoma ikiwa ni ishara ya kumkaribisha karika Manispaa hiyo, Septemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa na mkewe Mary wakiagana na watuimishi wa Makazi ya Waziri Mkuu ya Dar es salaam kabla ya kuondoka kuelekea Dodoma Septemba 30, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakisalimiana na Madiwani wa Manispaa ya Dodoma baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Septemba 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakisalimiana na Madiwani wa Manispaa ya Dodoma baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Septemba 30, 2016.

Waziri Mkuu, Kasim Majliwa akiwapungia wananchi baada ya kuwasili kwenye makazi yake mjini Dodoma Septemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wananchi wa Dodoma wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye makazi yake eneo la Mlimwa Septemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Waziri MKUU Kassim Majaliwa amesema kuanzia sasa mtu yeyote mwenye shida ya kuonana naye itabidi amfuate Dodoma na kwamba atarudi Dar es Salaam pindi akiitwa na Mheshimiwa Rais au Makamu wa Rais.


Ametoa kauli hiyo leo jioni (Ijumaa, Septemba 30, 2016) wakati akizungumza na viongozi mbalimbali na wakazi wa mji wa Dodoma waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili mjini hapa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa Julai 25 kuwa atahamia Dodoma ifikapo Septemba mwaka huu.



“Tukio hili la kuhamia Dodoma si la mzaha, hakuna siasa na wala si jaribio. Tumeshakeleza. Kama kuna waliokuwa wanafiria kwamba halitekelezeki watambua kwamba tayari tumeshafika. Na kuanzia sasa atakayetaka huduma ya Waziri Mkuu



Waziri Mkuu amesema Dodoma si ndogo kama baadhi ya watu wanavyodai na kwamba  huduma zilizopo zinatosha kukidhi mahitaji ya sasa. "Mkakati uliopo wa kupanua huduma za tiba, maji, umeme na masoko utawezesha watumishi wote kuishi bila bugudha yoyote."


“Awamu ya kwanza inaanzia Septemba hadi Februari mwakani. Mimi nimeshatangulia na wanaofuata ni mawaziri na manaibu wao wote, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wote. Natambua kwamba wote wana nyumba za kuishi na kama wapo ambao hawana hawazidi asilimia tano na nyumba zipo



Amewataka watumishi wote wa Serikali watambue kwamba safari imeshaanza na kila mmoja ajipange, na akarudia wito wa Mheshimiwa Rais kwamba atakayegoma kuhamia Dodoma atakuwa amejifukuza kazi.



Waziri Mkuu amewataka watendaji wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) wasifanye kazi kwa mazoea, bali wabadilike na kwa kuwa amehamia Dodoma ameahidi kuafuatilia kwa karibu zaidi.



Mapema akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Nchi (OWM SUBKAV), Jenista Mhagama amesema kilichofanyika leo ni uthibitisho kuwa yale ambayo Serikali ya Awamu ya Tano iliahidi sasa hivi imeanza kuyatekeleza.


"Tuliahidi kukusanya kodi, tuliahidi elimu bure, tuliahidi kupambana na mafisadi, tuliahidi kuondoa watumishi hewa, tuliahidi kuifufua ATCL na kununua ndege mpya na yote tumetekeleza,” amesema.



Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bw. George Simbachawene amesema uamuzi wa kuhamia Dodoma ni uthibitisho kuwa  viongozi wetu kweli wamedhamiria kutekeleza ahadi ya Baba wa Taifa ya kuhamishia makao makuu ya nchi hapa Dodoma.


"Dodoma imeanza kuchangamka na hii ni fursa tosha kwa mkoa wetu kubadilika. Tushirikiane na CDA kuijenga Dodoma mpya. Kitendo cha Mheshimiwa Waziri Mkuu kuingia Dodoma leo hii maana yake ni kwamba Serikali iko rasmi Dodoma," amesema.



Hafla hiyo ilihudhuriwa na Manaibu Waziri Anthony Mavunde na Dk. Ashatu Kijaji, Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Rais (Utumishi), Wakuu wa Wilaya za Mkoa huo, wazee wa mkoa huo, viongozi wa dini, viongozi wa taasisi zilizoko mkoani na baadhi ya wananchi.






IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

S. L. P. 980,

DODOMA

IJUMAA, SEPTEMBA 30, 2016.

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU NCHINI WATOA MICHE YA MITI 600 KUUNGA MKONO KAMPENI YA UPANDAJI MITI JIJINI DAR ES SALAAM

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Luhaga Mpina akipanda mti katika Shule ya Sekondani ya Mama Salma Kikwete, Jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni kuunga mkono kampeni ya upanadaji miti Jijini Dar es Salaam iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda, Kampeni hiyo ijulikanayo kama "Mti Wangu"  itazinduliwa kesho Oktoba Mosi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan. Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania umechangia miche ya miti 600 katika shule hiyo na miche ya miti mingine 3,000 itatolewa kesho wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo kwa ajili ya Jijiji la Dar es Slaam, katika awamu ya pili watachangia tena miche ya miti 5,000.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Luhaga Mpina (wa pili kulia) akimkabidhi Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mama Salma Kikwete, Elestina Chanafi (wa pili kushoto) baadhi ya miche ya miti kati ya miche 600 iliyotolewa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa ajili ya shule hiyo kuunga mkono Kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya upandaji wa miti Jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (kulia) akimkabidhi Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Luhaga Mpina (wa pili kulia) miche 600 ya miti iliyotolewa na ofisi yake kwa ajili ya shule ya Sekondani ya Mama Salma Kikwete Jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni hatua ya kuunga mkono Kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya upandaji wa miti Jijini Dar es Salaam ijulikanyo kama “Mti Wangu” . Katika uzinduzi huo TFS imechangia miche ya miti 3,000 kati ya miche 8,000 ambayo imepanga kutoa kwa ajili ya kupandwa katika Jiji la Dar es Salaam. 
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo.
Msanii wa Filamu nchini, Jackline Wolper (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo kuhusu kampeni yake ya "Think Green" katika kuunga mkono Kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ijulikanayo kama "Mti Wangu" ambayo itazinduliwa kesho Oktoba Mosi na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan . Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Luhaga Mpina.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (kushoto) akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mama Salma Kikwete Jijini Dar es Salaam leo katika hafla fupi ya upandaji wa miti shuleni hapo kuunga mkono Kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ya upandaji wa miti, Prof. Silayo amewaasa wanafunzi hao kuwa mstari wa mbele katika utunzaji wa mazingira na upandaji wa miti. Katika hafla hiyo TFS wamekabidhi jumla ya miche ya miti 600.
Picha ya pamoja kati ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Luhaga Mpina (wa tano kushoto), Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (wa sita kushoto), Msanii Jackline Wolper, Watumishi na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Mama Salma Kikwete.
(Picha na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii)

TANESCO YAFANYA KIKAO CHA UJIRANI MWEMA NA VIONGOZI WA JAMII INAYOZUNGUKA VITUO VYA KUFUA UMEME WA GESI VYA KINYEREZI JIJINI DAR ES SALAAM


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

SHIRIKA la Umeme nchini TANESCO na viongozi wa dini, vyombo vya dola na viongozi wa Serikali za Mitaa sita inayozungu vituo vya kufua umeme wa Gesi asili vya Kinyerezi jijini Dar es Salaam, wamekubaliana kuweka mikakati ya pamoja kuhakikisha jamii inashiriki katika ulinzi wa miundombinu ya umeme.

Makubaliano hayo yamefikiwa leo Septemba 30, 2016, kwenye kikao cha ujirani mwema kati ya TANESCO, TPDC, viongozi wa dini, viongozi wa serikali za mitaa na vyombo vya dola ili kujadili namna bora ya kulinda miundombinu ya umeme kwenye vituo hivyo.

“Umeme wa Gesi ni umeme salama kabisa, hata hivyo ni wajibu wetu kushirikiana pamoja kuhakikisha miundombinu ya umeme huu wa Gesi inatunzwa na kulindwa,”, Meneja wa Kituo cha Umeme Kinyerezi I, Mhandisi Lucas Busunge alianza kwa kusema wakati akiwakaribisha wajumbe kwenye kikao hicho.

Tumeona tuitane hapa leo ili tujadiliane pamoja namna bora ya kuhakikisha umeme huu utokanao na Gesi ambao Serikali imeiingia gharama kubwa, miundombinu yake inalindwa na nyinyi viongozi mnao wajibu mkubwa wa kuwafikishia ujumbe wananchi wanaoishi maeneo yanayozunguka mitambo hii. Alisema Mhandisi Busunge.

Akitoa mada juu ya Mambo yanayoweza kusababisha uharibifu wa miundombinu ya umeme wa Gesi na hasara inayoweza kulikumba taifa na jamii kwa ujumla, Mkuu wa Usalama wa TANESCO makao makuu, Misana Gamba alisema, “Lazima tutambue kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi katika ujenzi wa vituo hivi na fedha hizi ni za walipa kodi wa Tanzania, kwa hivyo ni wajibu wetu sote na sio TANESCO pekee kuhakikisha tunalinda miundombinu hii kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo,” alisema Gamba

Akifafanua zaidi, Mkuu huyo wa usalama alibainisha mambo ambayo jamii inapaswa kuelewa kuwa ni hatari dhidi ya miundombinu ya umeme ambayo ni pamoja na kuwasha moto, kulima au kuchimba mchanga, mmomonyoko wa udongo, wezi wa vyuma, uvuvi haramu, kujenga, kufanya biashara au kuendesha magari makubwa sehemu ambayo miundombinu hiyo ya umeme wa Gesi inapita.

Mkuu huyo wa usalama wa TANESCO alisema, hatari inayoweza kutokea endapo mambo hayo yatafanywa ni pamoja na kurudisha nyuma jiyihada za Serikali katika kuwaletea umeme wananchi, lakini pia hatari ya kulipuka kwa mitambo hiyo ambapo madhama makubwa yanaweza kuwakumba wananchi.

Meneja wa Kituo cha kufua umeme kinyerezi I, Mhandisi Lucas Busunge, akifungua kikao cha ujirani mwema kati ya TANESCO, TPDC na viongozi wa jamii inayozunguka Vituo vya kufua umeme wa Gesi vya Kineterezi jijini Dar es Salaam Septemba 30, 2016.
Mkuu wa Kitengo cha Usalama, TANESCO Makao makuu, Misana Gamba


Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji (aliyesimama), akizungumzia umuhimu wa viongozi wa mitaa kushirikiana na TANESCO katika kuelimisha umma, kutunza miundombinu ya umeme.

Afisa Usalama wa TANESCO makao makuu, Fidelis Almasi, akielezea namna viongozi wanavyoweza kushiriki katika kuelimisha wananchi umuhimu wa kutunza miundombinu ya umeme na athari za zitokanazo na uharibifu wa miundombinu hiyo kwa jamii na serikali.

Akichangia kwenye mazungumzo hayo, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji, ambaye ndiye alikuwa muendesha kikao, alisema, Shirika la Umeme Tanzania, TANESCO, imekuwa ikitoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kutunza miundombinu ya umeme kwa faida ya Watanzania wote, na hatua ya kikao hicho ni mwendelezo wa utoaji elimu na kuwataka viongozi hao kuwa mabalozi katika maeneo yao, kwenye nyumba za ibada, ili kusudi wananchi wengi waelewe umuhimu wa kuunza miundombinu ya umeme ambayo kimsingi ni mali ya Watanzania wote.

Naye afisa mwandamizi wa usalama Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini, (TPDC), Elias Muganda, alitahadharisha juu ya shughuli za kiuchumi kwenye eneo linakopita bomba la Gesi na ksuema hiyo ni hatari. “Kwa sasa kuna mabomba mawili yenye Gesi tayari, ambayo yako umbali wa mita 2 kwenda chini, yakipata mgandamizo unaosababishwa na magari makubwa kupita juu yake inaweza kupelekea leakge na kusababisha Gesi kuvuja na matokeo yake kila mtu anayajua ni moto.” Alifafanua

Akatoalea mfano wa mabomba yaitwayo Carthodic Protection, ambayo huzuia kutu, lakini tayari kuna watu wanang’oa vyuma hivyo na hii inaweza kusababisha kutu na mabomba kutoboka,alitahadharisha, Muganda.

Wakichangia mazungumzo hayo, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kanga, Shamte Mlanzi Mkali, alitoa wito kwa viongozi wenzake wa Mitaa, kila wanapokutana kwenye vikao, moja ya ajenda ya kuzungumza ni pamoja na usalama wa mitambo ya Gesi.Hata hivyo viongozi wengi walionyesha umuhimu wa TANESCO kutoa ajira kwa vijana waishio maeneo ya jirani na mradi ili waweze kuona manufaa ya moja kwa moja ya ujio wa mradi huo.

Mambo yaliyoazimiwa kwenye kikao hicho ni pamoja na ulinzi wa miundombinu ya Gesi iwe ni moja ya ajenda za vikao vya Serikali za Mitaa, na iwe marufuku kwa mtu kupita au kukatiza eneo la Mitambo bila ya kibali maalum, uwepo utaratibu wa kuwaalika viongozi wa TANESCO/TPDC kwenye vikao vya Serikali za Mitaa kama itahitajika.

Maazimio mengine ya kikao hicho kilichomuhusisha pia Mkuu wa upelelezi wa Kituo cha Sitakishari-Ukonga, SSP, Hassan Okello, ni pamoja na kampuni za ulinzi kwenye eneo la mitambo zijulikane kwa viongozi wa Serikali za mitaa yote inayozunguka eneo la mradi.

Mitaa iliyoshiriki kwenye kikao hicho ni pamona na Mtaa wa Kanga, Kibaga, Kinyerezi, Kichangani, na Kifura.
Mhandisi Busunge
Mkuu wa upelelezi, Kituo cha polisi Sitakishari-Ukonga, MrakibuMsaidizi wa Polisi, (ASP), Hassan Okello, akiwatoa hofu viongzoi hao kuhusu kutunza siri wanapotoa taarifa za wahalifu na uhalifu na kwamba yeye binafsi yuko tayari siku zote kuhakikisha usalama kwenye eneo hilo unazingatiwa
Afisa Usalama Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini, (TPDC), Eliasi Muganda, amesema, mabomba mawili ya gesi tayari yana gesi  na yako umbali wa kina cha mita 2 kutoka uso wa ardji na hivyo hayahitaji mgandamizo kutoka juu kwani ni hatari yanaeza kupata nyufa na kuvujisha Gesi.

Afisa Elimu wa Kata ya Kinyerezi, Mwalimu Mercy Mtei, (kulia), yeye amesema, atawashirikisha walimu na wanafunzi kueneza ujumbe kwenye jamii
Sheikh Juma Swaleh wa Msikiti wa Othman Bin-Afan wa Kinyerezi
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kichangani, Niyukuli Leonard (kulia)
Mchungaji Jacob Msami, akizungumza
Ustaadhi Ally akizungumza
Mchungaji Ariel Mungereja wa Kanisa la EAGT, Kinyerezi
Afisa Usalama wa Kituo cha Kinyerezi I, Furaha Munisi, akifafanua mambo mbalimbali ya kiusalama ambayo viongozi hao wanapaswa kuyachukua na kuwaelimisha wananchi
Picha ya pamoja baada ya kikao