Wednesday, July 6, 2016

MBUNGE MWAMOTO AIBUA UFISADI WA MWENDOKASI WA PESA ZA MADAWATI YA MFUKO WA JIMBO

Madawati  yaliyotengenezwa kwa  pesa  za  mfuko  wa   jimbo la  Kilolo ambayo mbunge  Mwamoto ameyakataa kutokana na  kukosa  ubora  ukilinganisha na thamani ya  pesa iliyotumika 
Mbunge  Mwamoto  katikati  akikimbia  kwenda  kukagua  madawati  katika   kijiji  cha Nyanzwa  leo
Kazi  ya  kuwatumikia  wananchi  ni ya mwendokasi  zaidi
Mbunge wa  Kilolo Bw Venance  Mwamoto akikagua madawati  yaliyotengenezwa kwa  pesa za mfuko wa  jimbo
Mwamoto  akitazama  madawati yaliyotengenezwa chini ya  kiwango
Haya ndio madawati  yaliyotengenezwa  kwa  pesa  za  mfuko wa jimbo la Kilolo ila  yapo chini ya  kiwango
Madawati ya  kisasa  yaliyotengenezwa kwa   michango ya  wanakijiji ambayo  yametengenezwa kwa  gharama  ndogo kwa  ubora  mkubwa
Wananchi wa Nyanzwa  wakiwa  katika  mkutano wa  kimaendeleo na mbunge  wao
Mbunge Venance Mwamoto akipinga madawati kutengenezwa chini ya kiwango
madawati yaliyotengenezwa na kijiji kwa Tsh 20,000 
madawati yaliyochini ya kiwango yaliyotengenezwa na ofisi ya Mbunge ambayo yamechakachuliwa kila moja limechongwa kwa Tsh 50,000

Na Matukiodaimablog

HOFU  ya kutafunwa kwa fedha milioni 30  zilizotolewa na mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto kuchonga madawati imetanda baada ya mbunge huyo kuibua ufisadi  wa mwendokasi na kulazimika kuyakataa madawati 40 yaliyotengenezwa kwa fedha za mfuko wa jimbo yaliyopelekwa kijiji cha Nyanzwa na Halmashauri kuwa hayana ubora.
Mbunge Mwamoto amesema kuwa hajapendezwa na kiwango cha utengenezaji wa madawati hayo ambayo ni mabovu na upo uwezekano wa kuharibika zaidi ndani ya siku mbili baada ya wanafunzi kuanza kutumia.
Akizungumza leo na wananchi wa kijiji cha Nyazwa baada ya kukagua madawati hayo yaliyotengenezwa kwa pesa za mfuko wa jimbo ,kuwa hajapendezwa na ubora wa madawati hayo na hatakuwa tayari kupokea madawati hayo.
Kwani alisema ofisi yake imetoa fedha za kutengeneza madawati kwa ajili ya kusaidia kupunguza kero za madawati katika shule za wilaya hiyo ya Kilolo lengo ni kuona wanafunzi hawapati tena kero ya madawati.
Mbunge huyo alisema kuwa ametoa jumla ya Tsh milioni 30 kutoka mfuko wa jimbo kwa ajili ya madawati 600 ili kiwango cha madawati hayo 40 ambayo yamepelekwa kijiji cha Nyanzwa hajafurahishwa nacho.
Hivyo ameutaka uongozi wa serikali ya kijjji hicho kutokubali kupokea madawati hayo ambayo yapo chini ya kiwango kwani hayupo tayari kuona watu wanachakachua fedha hizo.
Mwamoto alisema haiwezekani madawati ya kijiji yaliyotengenezwa kwa Tsh 20,000 yakawa bora zaidi kuliko madawati ya mfuko wa jimbo ambayo yametengenezwa kwa gharama kubwa ya Tsh 50,000 kwa kila dawati.

No comments: