Tuesday, March 22, 2016

TBS YATAKIWA KUHAKIKI VILAINISHI NA MITAMBO KUTOKA NJE YA NCHI.

 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Kiwanda cha Nondo cha Kamal Steels Ltd. kilichopo Chang'ombe, DSM, pembeni yake ni Gagan Gupta ambaye ni Mwenyekiti na Mtendaji wa Kiwanda hicho.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji akiangalia makopo yanayotumiwa na Kiwanda cha Kamal kama nalighafi za kiwanda akiwa na uongozi wa kiwanda.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji akimuangalia fundi wa kusawazisha chuma kwa kutumia Shaper Mashine.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akipanda Mti wa kumbukumbu mara baada ya kukitembelea Kiwanda cha Kamal.
Wafanyakazi wa kiwanda cha Kamal wakishuhudia ziara ya Waziri kiwandani hapo.  

WAZIRI wa viwanda,biashara na uwekezaji, Charles Mwijage amelitaka shirika la viwango hapa nchini (TBS) kuhakikisha wale wote wanaotaka kuingiza vilainishi mitambo kutoka nje ya nchi wanatoa taarifa kabla ya tarehe 1 mwezi wa 5 mwaka huu ili kupambana na bidhaa bandia.

  Mwijage ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika viwanda vitatu vya vilainishi mafuta na kiwanda kimoja cha nondo vilivyopo manispaa ya temeke jijini Dar es Salaam  ambapo ameeleza kuwa ziara hyo imelenga kuhakikisha watanzania wanapata bidhaa bora na  zinazokidhi mahitaji ya watumiaji wa bidhaa hizo.

Aidha  Mwijage amewaagiza waendeshaji wa viwanda hivyo kuhakikisha wanazalisha bidhaa zenye ubora kwani vilainishi mitambo vina umuhimu mkubwa sana hasa kudhibiti ajari mbalimbali katika mitambo ya uendeshaji shughuli za kimaendeleo.


Katika ziara hiyo mh. Mwijage alianza katika kiwanda cha nondo cha kamal steel, akaenda kiwanda cha vilainishi mitambo cha fuchs pia alienda katika kiwanda cha vilainishi mitambo cha general petroleum na kumalizia ziara yake katika kiwanda cha kuzalishilia vilainishi vya mitambo cha oryx vyote vikiwa manispaa ya temeke jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment