Saturday, January 9, 2016

WAZIRI NAPE NNAUYE AKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM

  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mh.Nnape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya Wakuu wa Idara ya Habari Maelezo na Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari  mapema leo,alipokutana nao na kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabiri tasnia hiyo,mkutano huo umefanyika kwenye moja ya ukumbi ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mh.Nnape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya Wakuu wa Idara ya Habari Maelezo na Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari 
  Kaimu Mkurugenzi Idara ya HabariMAELEZO Bi Zamaradi Kawawa akiwakaribisha Wahariri wa vyombo vya habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar,kwenye mkutano ulioitishwa na Waziri Nape kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali yanayoikabiri tasnia ya habari hapa nchini.Pichani kati ni Waziri Mh.Nape pamoja na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda.
 Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano huo wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa ukumbini humo.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mh.Nnape Nnauye akizungumza na Wahariri wa vyombo vya habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar,kwenye mkutano uliohusu kujadili mambo mbalimbali zikiwemo changamoto zinazoikabiri tasnia ya habari hapa nchini.Pichani kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda na kushoto ni  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa . 
 Mmoja wa Wahariri Kurwa Kaledia kutoka New Habari Hause akiomba ufafanuzi wa jambo kwa Mh Waziri Nape huku baadhi ya wahariri wakifuatilia kwa makini.
  Mmoja wa Wahariri Grace Hoka akifafanua jambo kwenye mkutano huo
  Baadhi ya Wahariri wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo
  Baadhi ya Wahariri juu pichani wakishiriki kuchangia mambo mbalimbali kwenye mkutano huo.
  Baadhi ya Wahariri juu pichani wakishiriki kuchangia mambo mbalimbali kwenye mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda akitoa muongozo kwa Wahariri wa Vyombo vya habari (hawapo nchini) kuhusina na mkutano wao ulioitishwa na Waziri Nape kujadili mambo mbalimbali na changamoto zinazoikabiri tasnia hiyo kwa ujumla.
 Mhariri akiuliza swali
Baadhi ya Wadau wakubwa wa habari pia walikuwepo kwenye mkutano huo .PICHA NA MICHUZI JR

 Mhariri wa Gazeti la the Citizen Bw Peter Nyanje akichangia jambo wakati wa kikao kati ya wahariri wa vyombo vya habari na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
 Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Jamhuri Media Ltd Bw.Deodatus Balile akichangia hoja katika kikao kati ya wahariri wa vyombo vya habari na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.




Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akiongea na wahariri wa Vyombo vya Habari(hawapo pichani) leo hii jijini Dar es Salaam.Mhe Nape alivipongeza vyombo vya Habari kwa kufanya wajibu wao katika kipindi cha uchaguzi mkuu na kuwahaidi kuwa serikali itakuwa karibu nao sana na kuhimiza kuwa serikali ya awamu ya Tano itatunga sheria nzuri itakayoraisisha utekelezaji wa majukumu yao.Kushoto kwake  ni Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Bw.Absalom Kibanda. 
 Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Bw.Absalom Kibanda  akiwahimiza wahariri wa vyombo vya Habari(hawapo pichani) kuhusu kutenda wajibu wao wakati wote wanapofanya kazi zao kwani uhuru waendani na wajibu leo jijini Dar es Salaam.kulia kwake ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye na wa mwisho ni Kaimu mkurugenzi mkuu Idara ya Habari-MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa.


Mhariri mkuu wa Gazeti la The Guardian Bw.Jesse Kwayu akichangia hoja wakati  wakati wa kikao kati ya wahariri wa vyombo vya habari na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Nape Nnauye.Bw Kwayu alimsihi Mhe Nape kuzidi kuwa karibu na waandishi na pia zitungwe sheria zitakazowawezesha waandishi wa habari kupata habari kwa urahisi na kufanya kazi yao ya kuhabarisha jamii. Picha na Daudi Manongi-Wizara ya habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo

No comments:

Post a Comment