Wednesday, September 30, 2015

WATANO WAFARIKI DUNIA KATIKA MATUKIO TOFAUTI MKOANI MBEYA WAMO RAIA WA ETHIOPIA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi.
     Na Jamiimojablog.
       Watu watano wamefariki dunia   Mkoani Mbeya katika matukio matatu tofauti likiwemo la ajali ya haice iliyosababisha vifo vya watu wanne mkoani hapa.
       
         Katika tukio la kwanza gari  lenye namba za usajili  T.519 Akh aina ya Toyota Haice ikiendeshwa na dereva  asiyefahamika kugongana na pikipiki yenye namba za usajili  T.535 Awc aina Ya T-Better eneo la Nanenane Jijini Mbeya.

      Ajali hiyo imetokea Septemba  29 majira ya  Saa 4 usiku katika eneo la   Nane-Nane, Kata Ya Isyesye,  barabara Kuu ya Mbeya/Njombe .

        Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ndugu Ahmed Msangi amewataja waliokufa katika ajali hiyo kuwa mwendesha  pikipiki ambaye bado jina lake halijafahamika sanjali na wengine watatu raia wa Ethiopia ambao majina yao bado hayajafahamika mara moja  ambao walikuwa  wamepakizwa kwa pamoja kwenye pikipiki hiyo kwa mtindo maarufu wa Mshikaki.

       Aidha Katika ajali hiyo  Edward Aloyce (42) Mkazi Wa Uyole ambaye alikuwa abiria kwenye  Haice alijeruhiwa na amelazwa katika   Hospitali ya Rufaa Mbeya. 

          Kwa mujibu  wa  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ndugu Msangi  amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa gari hiyo ya abiria pamoja na pikipiki hiyo.

       Amesema  dereva wa hiace alikimbia mara baada ya kusababisha ajali hiyo ambapo jitihada za kumsaka zikiendelea kufanyika na jeshi hilo miili ya  marehemu imehifadhiwa  Hospitali Ya Rufaa Mbeya.

        Katika tukio jingine mtu mmoja  Mkazi wa  Masoko Wilaya ya Rungwe  Ndugu  Tukupyelesya Enock Mwakifuna (54) amefariki dunia mara baada ya gari walilokuwa wakisafiria  T.913 Amb aina Ya Toyota Hillux ikiendeshwa na dereva asiyefahamika  kuacha njia na kupinduka  huko katika kijiji cha  Masoko,  Wilaya Ya Rungwe, Mkoa Wa Mbeya bararabara ya Tukuyu/Lwangwa.

      Aidha Katika ajali hiyo abiria Watatu wanawake wawili na Na mwanaume mmoja walijeruhiwa na wamelazw katika hospital ya  Hospitali ya Wilaya Rungwe huku chanzo cha . ajali hiyo ni mwendo kasi  dereva .

     Kufuatia matukio hayo Kamanda wa Polisi Mkoa Wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi Wa Polisi Ahmed Msangi ametoa o wiito  Kwa madereva kuwa  Makini wanapotumia vyombo vya moto ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza Kuepukika.

EALA ROOTS FOR CONCERTED EFFORTS IN COMBATING CORRUPTION

 Heads of Anti-Corruption Authorities from Republic of Kenya (left), South Sudan (centre) and the Federal Republic of Ethiopia stand for the Anthem at the start of the meeting in Entebbe earlier today
 Rt Hon Daniel F. Kidega (right) Speaker of EALA, Hon Shem Bageine, Minister for EAC Affairs, Uganda and Lady Justice Irene Mulyagonja, inspector General of Uganda at the meeting earlier today.  The EALA Speaker opened the meeting
A section of delegates at the meeting in Entebbe

East African Legislative  Assembly

EALA ROOTS FOR CONCERTED EFFORTS IN COMBATING CORRUPTION
Speaker Kidega tells Anti-Corruption stakeholders Assembly keen to close ranks to fight off vice

East African Legislative Assembly,Entebbe,Uganda,29th September 2015 –  EALA Speaker, Rt. Hon Daniel Fred Kidega wants Anti-Corruption Authorities in the EAC region to further concert efforts, establish linkages and support enactment of a regional law in their quest to rid the region of corruption. 

Consequently, the regional Assembly is set to collaborate with the anti-graft authorities under the aegis of the East African Association of the Anti-Corruption Authorities (EAAACA).  

The EALA Speaker this morning presided over the opening ceremony of the 9th EAAACA Annual General Meeting themed; Strengthening Efforts to eradicate Corruption in Entebbe, Uganda.

Rt. Hon Kidega said that EALA and the EAC were committed to combating the chronic cancer of corruption.   He said the Assembly would soon table and discuss key pieces of legislation to combat the scourge.

“On our part as an Assembly, you will be pleased to note that we are considering enacting 3 key Bills to confront corruption head-on. The envisaged Bills are the EAC Integrity and Anti-Corruption Bill, 2015, the EAC Procurement Bill, 2015 and the EAC Whistle Blowers Bill, 2015. The Laws passed by EALA supercede those of the Partner States on matters within the purview of the Community”, the Hon Speaker remarked.

He termed regional co-operation as a key component in containing corruption saying that it undermined good governance, erodes the rule of law and hampers economic growth. “If left unattended, it could spiral to uncontrollable levels given the other criminal activities such as money laundering, bribery and abuse of Office,” Rt. Hon Kidega remarked.  

The Speaker was emphatic that it was necessary for the Association to have a closer working relationship within the EAC.    “As a key institution in the eradication of corruption, it is vital and necessary for EAAACA to explore means and ways of working with EAC including been considered for Observer Status at the Community,” he remarked.

According to the Speaker, the Mbeki led Report on the High Level Panel on illicit Financial Flows released in February this year is telling. The Report narrates that illicit flows relate principally to commercial transactions, tax evasion, criminal activities such as money laundering, bribery, corruption and abuse of office, which he said promote corrupt tendencies. 

Moreover, it is reported that countries that are rich in natural resources and countries with inadequate or non-existent institutional architecture are most at risk of falling victim to illicit financial flows.  

In attendance at the two-day AGM are representatives of Anti-Corruption Authorities from Kenya, Rwanda, Uganda, Tanzania, Ethiopia and South Sudan. 

The meeting is being hosted by the Inspectorate of Government led by the Inspector General of Government of the Republic of Uganda Hon. Lady Justice Irene Mulyagonja Kakooza.   Lady Justice Kakooza maintained that ridding corruption needed political, legislative and the goodwill of all citizens.

The Minister for EAC Affairs, Hon Shem Bageine said corruption had spread its tentacles in various sectors in the region and largely manifested itself across the divide.  “Governments, Private and Public sectors must get to the bottom of and root out this evil,” Minister Bageine added.

On his part, the President of the EAAACA, Mr ClĂ©ment Musangwabatware reiterated the need to embrace good governance and total fight on corruption which he termed costly to governments and businesses.

Analysts contend that promoting and facilitating co-operation among Partner States is crucial in ensuring effectiveness of measures and actions to detect, investigate, punish and eradicate corruption.
is further expected to review its activities over the year as it strategises over how to make it more effective.

The AGM is the supreme governing body of the Association and comprises of Members of Anti-Corruption Authorities of EAAACA and Honorary Members.

TASOI YAZINDUA KAMPENI YA SARATANI KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO BILA MALIPO YOYOTE

Katibu Mkuu wa TASOI, Belinda Mlingo akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati endelevu wa kuendesha kampeni ya Mshikamano dhidi ya Saratani kwa kutumia technolojia ya mawasiliano bila malipo yoyote katika ukumbi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road leo jijini Dar.
Mshauri kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dk. Dominista Kombe ambaye akitoa takwimu ya wagonjwa wanaofika kutibiwa katika hospitali hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Kinga Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage  akizungumza jambo mbele ya waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road leo.
 Waandishi wa habari wakiendelea kuchuka habari.
 Mkutano ukiendelea

Na Michael Maurus, Dar es Salaam
ASASI isiyo ya kiserikali ya Tanzania Social Outreach Initiative (TASOI), imezindua kampeni rasmi mpango mkakati endelevu wa kuendesha kampeni ya Mshikamano dhidi ya Saratani kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano bila malipo yoyote.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa TASOI, Belinda Mlingo, alisema kuwa kampeni hiyo itatoa elimu, uhamasishaji na kutoa ushauri nasaha kwa wananchi kwa kupitia ujumbe mfupi wa simu (SMS).

Amesema kuwa katika kampeni hiyo, TASOI inashirikiana na wadau mbalimbali katika masuala ya afya, teknolojia na uhamasishaji wa jamii ili kutoa huduma hii muhimu bila malipo au gharama yoyote kwa watumiaji wa simu za mikononi.

“Kwa kumnukuu Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Yasiyoambukiza Wizara ya Afya, Profesa Ayoub Mgimba, ‘Hali halisi inadhihirisha kwamba magonjwa yasiyoambukiza kama saratani hivi sasa yamekuwa ni tatizo kubwa hasa katika nchi kama yetu ambapo ufahamu na mwamko ni mdogo sana juu mazingira hatarishi, viashiria, matibabu na matunzo ya wahanga wa magonjwa haya. Saratani inasababisha madhara makubwa ambayo yanaelekea kuwa majanga kwa jamii na kiuchumi kwa Taifa.”

Akielezea jinsi kampeni hiyo itakavyoendeshwa, Hellen alisema kuwa kwa muda wa miezi sita, watumiaji wa simu za mkononi za mitandao yote nchini, wataweza kupata taarifa za saratani kwa kupitia namba 15774 kwa kutuma neno CANCER au SARATANI kwenda namba hiyo na kuchagua lugha anayotaka kupokea taarifa hiyo, iwe ni Kiswahili au Kiingeza.

“Hapo utapokea ujumbe wenye elimu juu ya saratani, kati ya za viungo vya uzazi, yaani tezi dume, saratani ya matiti na shinga ya kizazi. Huduma hii itapatikana kupitia mitandao yote ya simu nchini, Vodacom, Airtel, Tigo, Zantel na TTCL,” alisema.

Ameongeza, “Tungependa pia kuwashirikisha wananchi wote kuchangia kwa hiyari ili tutimize malengo haya kwa pamoja. Na hii unaweza kuchangia Sh 1200 kwa mwezi au Sh 300 kwa wiki.

“Hili utaweza kulifanya kwa kukubali kupokea ujumbe mfupi kutoka kwetu ambao utakuwa na gharama ndogo ya Sh 150 tu. 

Pia unaweza kuchangia kupitia ezypesa, m-pesa, tigopesa, airtel money. Uchangiaji huu ni wa hiyari na hauzuii kupata huduma ya elimu ya saratani.”

Kwa upande wake, Daktari bingwa wa kwanza wa saratani mwanamke Tanzania, Dominista Kombe wa Ocean Road Cancer Istitute, amesema kuwa ni kweli saratani ni janga la jamii, hali halisi hapa Tanzania, saratani ni tatizo kubwa na linaongezeka kwa kasi, ni jumla ya ugonjwa wa HIV na ugonjwa wa TB, tatizo la saratani lilitakiwa kupewa kipaumbele zaidi.

“Tatizo jamii huwa haipo tayari kuweka wazi juu ya uginjwa huu kwa kuogopa aibu ya kutengwa, haya yote yakitokana na uhafamu mdogo juu ya ugonjwa huu,” amesema.

Amesema kuwa serikali imekuwa ikijitahidi kupambana na ugonjwa huu kwa kutoa huduma bure, lakini hata hivyo imejikuta ikishindwa katika kukabiliana nalo kwani tatizo ni kubwa mno, akiitaka jamii kusaidia katika vita hiyo kama walivyoamua kufanya TASOI waliokuja na mpango wao wa kampeni kupitia simu kuiwezesha jamii kujua juu ya viashiria vya janga hilo.

Amesema kuwa tatizo la saratani ni la dunia nzima, hivyo kuna ulazima wa jamii kujenga utaratibu wa kupima afya mara kwa mara kama ilivyo kwa nchi za Ulaya ambako imesaidia kupunguza ukubwa wa janga hilo kupitia chanjo.

Amesema kuwa Ocean Road hupokea wagongwa wapya 5000 kwa mwaka, kati yao asilimia 80, wanafika wakiwa katika hali mbaya kiasi kwamba hupewa tiba ya kuwaongezea siku tu, huku asilimia ndogo sana, huwahi na kupewa tiba inayowawezesha kuishi.

ROCK CITY MARATHON 2015 YAZINDULIWA, KUTIMUA VUMBI NOVEMBA 15

 Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi  (wa kwanza kushoto) akiwa kwenye hali ya furaha mara baada ya kuzindua msimu wa saba wa mbio za Rock City Marathon zinazotarajiwa kufanyika Novemba 15 mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Wengine ni pamoja na Meneja Mkuu wa kampuni ya Capital Plus International (CPI) ambao ndio warataibu wa mbio hizo Bw Erasto Kilawe (mwenye shati jeupe), Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. Salim Kimaro (wa pili kulia) na Bi Ummy Hassan kutoka idara ya Uhusiano NSSF ambao ni moja wa wadhamini wakuu wa mbio hizo.
 Meneja Mkuu wa kampuni ya Capital Plus International (CPI) warataibu wa mbio hizo Bw Erasto Kilawe (wa kwanza kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) wakati wa uzinduzi wa msimu wa saba wa mbio za Rock City Marathon zinazotarajiwa kufanyika Novemba 15 mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.  Wengine ni pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi  (wa pili kushoto), Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. Salim Kimaro (wa tatu kushoto).

 Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. Salim Kimaro (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) wakati wa uzinduzi wa msimu wa saba wa mbio za Rock City Marathon zinazotarajiwa kufanyika Novemba 15 mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Wengine ni pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi  (wa kwanza kushoto) na Bi Ummy Hassan kutoka idara ya Uhusiano NSSF ambao ni moja wa wadhamini wakuu wa mbio hizo.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi  (wa tatu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na waandaaji pamoja na wadhamini wa mbio za Rock City Marathon mara baada ya kuzindua rasmi msimu wa saba wa mbio hizo jijini Dar es Salaam jana. Mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Novemba 15 mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Wengine ni (kutoka kushoto) Katibu Mkuu wa BMT, Lihaya Henry,  Meneja Mkuu wa kampuni ya Capital Plus International (CPI) ambao ndio waratibu wa mbio hizo, Erasto Kilawe, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. Salim Kimaro , Bi Ummy Hassan kutoka idara ya Uhusiano NSSF ambao ni moja wa wadhamini wakuu wa mbio hizo pamona na Katibu Mkuu msaidizi chama cha riadha Tanzania (RT) Bi. Ombeni  Savala .

Na Mwandishi Wetu.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi, amezindua msimu wa saba wa mbio za Rock City Marathon zitakazofanyika Novemba 15 mwaka huu kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mbio za Rock City Marathon, zinazoandaliwa na Kampuni ya Capital Plus International (CPI), kwa ushirikiano na Chama cha Riadha Tanzania (RT), pamoja na Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MRAA) zinalenga kutambua na kuinua vipaji vya wanariadha nchini na pia kukuza utalii wa ndani kupitia sekta ya michezo.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam, Bw. Malinzi alisema baraza linafuraha kuona makampuni binafsi yakijiingiza katika kuinua mchezo wa riadha nchini.
“Mchezo wa riadha una changamoto kubwa na tunatambua jitihada zinazoendelea kufanywa na kampuni ya Capital Plus katika kurudisha hadhi ya mchezo  huu nchini kama ilivyokuwa miaka ya sabini na themanini,” alisema.
 Alisema kuwa Tanzania itarudi kileleni katika medani za michezo duniani kama wachezaji wataandaliwa katika viwango vinavyokubalika kimataifa.
“Inashangaza kuona taifa la watu milioni 45 linawakilishwa na wanariadha wachache sana, tena katika mbio ndefu huku tukikosa wanariadha wanaoliwakilisha vyema taifa katika mbio fupi,” alisema.
Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja Mkuu kutoka kampuni ya Capital Plus International, Bw. Erasto Kilawe alisema kuwa mbio hizo zimekuwa zikionyesha mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009.
 “Jiji la Mwanza limebarikiwa kuwa na vivutio mbalimbali vya utalii. Jambo hili limetusukuma kuendelea kumulika vivutio vya kipekee vinavyopatikana katika ukanda wa ziwa Victoria kupitia mbio hizi,” alisema Bw. Kilawe huku akiongeza kuwa mikakati kabambe imewekwa ili kuhakikisha mbio za mwaka huu zinakuwa za mafanikio makubwa kuliko misimu iliyopita.
Alisema baadhi ya makampuni yameanza kujitokeza kudhamini mbio hizo ikiwa ni pamoja na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Precision Air, New Africa Hotel na Bank M huku makampuni zaidi yakionyesha nia ya kudhamini mbio hizo.
“Tunawaalika wadhamini waendelee kujitokeza kwa wingi ili kuzifanya mbio za mwaka huu kuwa bora zaidi,” alisema.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wa michezo ikiwa ni pamoja na wanariadha, viongozi wa vyama vya riadha, viongozi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na wadau mbali mbali wa riadha nchini.
Kwa upande wake Afisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF , Salim Kimaro alisema kuwa shirika hilo limekuwa mstari wa mbele kudhamini mbio hizo kutokana ari yao katika kukuza hali ya michezo hapa nchini.
“Kwetu suala la michezo ni moja ya vipaumbele vyetu kutokana na ukweli kuwa michezo ni afya na pia ni sehemu ya ajira kwa vijana kwa sasa…tunaahidi kuwa mstari wa mbele katika kufaanikisha mbio hizi,’’ alisema.

MABONDIA THOMAS MASHALI NA FRANSIC CHEKA WASAINI KUZIDUNDA DESEMBA 25 JAMUHURI MOROGORO


Promota Kaike Silaju katikati akiwainuwa mikoni juu mabondia Thomas Mashali kushoto na Fransic Cheka baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Thomas Mashali kushoto na Fransic Cheka wakionesha mikataba yao baada ya kusaini kuzipiga desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Fransic Cheka kushoto na Thomas Mashali wakisoma mkataba kabla ya kutia saini kwa ajili ya kuzipiga desemba 25 katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS
Wakili Paul Kalomo kutoka Mega Attorneys akiwafafanulia kifungu kwa kifungu mabondia Thomas Mashali wa pili kushoto na Fransic Cheka kulia kabla awajasaini
Promota Kaike Silaju katikati akipitia mkataba kabla ajawasainisha mabondia Thomas Mashali kushoto na Fransic Cheka ambapo wamekubaliana kuzipiga desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS

Wakili Paul Kalomo akiwaelekeza mabondia Thomas Mashali kushoto na Fransic Cheka jinsi ya kusaini mkataba wa pili kushoto ni promota Kaike Silaju  mabondia hawo watapigana desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri morogoro .


 Na Mwandishi Wetu
Mabondia Thomasi Mashali na Fransic Chaka Jana wamesaini mkataba wa kuzipiga siku ya desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri Morogoro

akisimamia utiaji saini huo 
Wakili Paul Kalomo kutoka Kampuni ya  Mega Attorneys amesema mkataba huo ni rasmi kwa mabondia hawo watapambana siku hiyo kwenye mpambano wa raundi kumi kwa dakika tatu kila raundi na kupumzika kwa dakika moja mpambano utakuwa wa raundi kumi na mabondia watapimwa afya zao siku moja kabla ya mchezo ili kujiridhisha kuwa wako fiti

nae promota wa mpambano uho ambaye amekuwa akiandaa mapambano makubwa makubwa na yenye msisimko nchini amesema kuwa mpambano uho unasubiliwa na mashabiki lukuki na nimeamua kuweka katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro ili kuwapa fursa nyingine kwa wakazi wa morogoro kumwona Cheka ambaye kwa mda mrefu ajacheza

nae bondia Fransic Cheka amewaomba wapenzi na mashabiki wajitokezekwa wingi ili kuja kujionea kichapo atakachompa Mashali ambapo ndio kitamfanya ajutie kabisa kucheza mchezo wa ngumi

kwa upande wa Mashali amesema amefurai kupata nafasi nyingine ya kucheza na cheka kwani anataka kuonesha kiwango chake kilivyo kikubwa kwa sasa na yeye ni nambari wani katika ngumi nchini


katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na mapambano ya utangulizi ambapo bondia Vicent Mbilinyi atapambana na Deo Njiku wakati Mohamed Matumla atakabiliana na Cosmas Cheka

IGP MANGU AHIMIZA UCHAGUZI WA AMANI TARIME.

 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akisalimiana na Maofisa wa Polisi katika Kanda Maalumu ya Tarime na Rorya jana wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo wa Kipolisi.Kushoto ni Kamanda wa Polis Kanda Maalumu Tarime na Rorya, Lazaro Mambosasa.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Hosteli ya Polisi Kanda Maalumu ya Tarime na Rorya jana wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo wa Kipolisi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akizindua Hosteli ya Polisi katika mkoa wa Kipolis Kanda Maalumu ya Tarime na Rorya jana wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo wa Kipolisi
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akizungumza na wadau wa Polisi (hawapo pichani) wakati alipokuwa  katika ziara ya kikazi mkoa wa Kipolisi Tarime na Rorya ambapo alitumia kikao hicho kuwaasa kufanya uchaguzi kwa amani na utulivu.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)

Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Tarime.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu amewataka Viongozi wa Vyama vya Siasa katika Wilaya za Tarime na Rorya kufanya Kampeni za Kistaarabu ili kufanikisha Uchaguzi Mkuu pamoja na kuimarisha Amani na Usalama Wilayani humo.
IGP Mangu aliyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na Wadau wa Polisi wakiwemo Viongozi mbalimbali, Vyama vya Siasa pamoja na Wagombea wa Viti vya Ubunge na Udiwani, wakati alipokuwa katika Ziara ya Kikazi katika Kanda Maaalum ya Polisi Tarime na Rorya.

Alisema ili uchaguzi wa mwaka huu uweze kufanyika kwa amani, Viongozi wa Vyama vya Siasa na Wagombea hawana budi kuwashawishi wafuasi wao kufuata Maadili ya Uchaguzi ikiwemo kutotoleana lugha za Matusi.

IGP Mangu alisema baada ya Uchaguzi maisha yataendelea kama kawaida hilo ni jukumu la Wananchi wote wa Tarime kuondoa Uhasama wao katika mambo ya Siasa kwa kuwa Siasa siyo Uhasama.

Aidha, aliwashauri Wagombea Ubunge na Udiwani katika Majimbo ya Tarime Mjini, Vijijini, na Rorya kukutana mara kwa mara ili kujenga kuaminiana na kutatua changamoto zinazojitokeza katika kipindi hiki cha kampeni na hatimaye siku ya uchaguzi Mkuu.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Polisi Tarime na Rorya, kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Lazaro Mambosasa, aliwahakikishia Wadau wote kuwa Jeshi la Polisi limejipanga vyema kukabiliana na vitendo vyote vya vurugu vitakavyojitokeza, pamoja na kuhakikisha kila Mwananchi aliyejiandikisha anapata fursa ya kupiga kura bila vitisho vya aina yoyote.

Naye Mgombea Ubunge katika Jimbo la Rorya kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Lameck Airo alisema katika jimbo analogombea hakuna vurugu kwa kuwa wamekuwa wakiheshimiana katika Kampeni ili kuepusha vurugu kwa Wagombea na Wafuasi wao.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Dini,Vyama vya Siasa, Wafanyabiashara, Asasi zisizo za Kiserikali, Wazee wa Kimila pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Tarime.

RAIS KIKWETE AAGWA NA RAIS OBAMA NA MAMA OBAMA NA MABALOZI WA AFRIKA KATIKA SIKU YAKE YA MWISHO UMOJA WA MATAIFA












DAVIS MOSHA AANZA UTEKELEZAJI WA AHADI ZAKE MOSHI

Katika hali isiyotarajiwa  na wengi katika Jimbo la Moshi Mjini, Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Davis Mosha ameanza utekelezaji wa ahadi zake katika Jimbo hilo,  wiki chache baada ya kuzungumza na wanamuziki na wasanii kuhusu kazi zao na wasanii hao kuomba kupata kituo cha Redio cha kisasa na Studio ya kisasa ambavyo vitaweza kufanya kazi zao kwa ubora zaidi na pia kufika mbali.
Katika kutekeleza hilo Mh. Davis Mosha amekwishaanza ujenzi wa Studio ya Kisasa ya Kituo cha Redio chini ya Kampuni yake ya Africa Swahili Media na ujenzi huo unatarajiwa kukamilika mapema na vifaa vya Studio huyo vinatarajiwa kuwasili muda wowote kutoka Dar es Salaam baada ya kuwasili Bandarini vikitokea Nchini Italy. Mh. Davis Mosha aliwaahidi wasanii hao kufungua kituo cha Redio kitakachoweza kusikika Tanzania Nzima na Duniani kote kwa njia ya Satelite. Pia aliwahakikishia kufungua na kituo cha televisheni. Kituo hicho cha Redio na Studio ya kisasa kianatarajiwa kufunguliwa katika jingo la Kilimanjaro Commercial Complex Maarufu kama jingo jipya la NSSF lililopo Moshi Mjini.

Mh. Davis Elisa Mosha
  
Hati ya Kontena la Vifaa vya Studio lililotoka Italy Baada ya kuingia Bandari ya jiji la Dar es Salaam.

Mbali na utekelezaji huo wa Kero ya Wasanii, Mh. Davis Elisa Mosha wiki iliyopita aliweza kufanya Ziara ya kimya kimya katika Soko la Mitumba la King George Memorial na kutazama Changamoto za Soko hilo lakini pia alipata fursa ya kuzungumza na uongozi wa Soko hilo na wafanyabiashara wa Soko hilo. Kwa pamoja walieleza MAzingira magumu wanayofanyia Biashara huku ikiwa Miundombinu mibovu ikiwemo vyoo na Soko halina Paa inapelelea iwapo mvua itanyesha basi kunakua hakuna biashara kabisa maana Bidhaa hunyeshwa na Mvua na mbali na Mvua pia jua ni lao. Katika kutatua changamoto hizo Davis Mosha aliwaahidi kulifanyia kazi mapema tatizo lao na hatosubiri mpaka muda wa uchaguzi ufike maana adha hiyo wanayoipata ni wananchi wa Moshi wakiwemo mama zake na baba zake waliopo hapo Sokoni. 


Mh. Davis Mosha alipotembelea Soko la Mitumba la Memorial na kujionea changamoto mbalimbali.


Mh. Davis Mosha akisalimiana na wafanyabiashara wa soko la Memoria alipotembelea soko hilo.
Kutokana na Ahadi hiyo Jana Mh. Mosha aliwasili Sokoni hapo na Mainjinia kutoka Kampuni ya Group Six ltd ambao ni Raia wa China   kwa lengo la kufanya kufanya vipimo na Michoro ya uboreahwaji wa Soko hilo ili kuweza kuondoa changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wa Soko hilo. Mainjinia hao walizunguka katika Soko hilo na kutazama eneo la Soko ili kuweka mipango ya kuanza ujenzi wa Soko hilo ambapo ujenzi huo hautoathiri wafanyabashara hao kuendelea kufanya biashara zao.

Mainjinia Raia wa China kutoka Kampuni ya Group Six wakiwa soko la Mitumba la Memorial kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa Matengenezo ya soko hilo.





Mh. Mwigulu Nchemba akimkaribisha Mh. Davis Mosha azungumze na Wafanyabiashara wa Soko la Memorial 

Mh. Davis Mosha akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Mitumba la Memorial
Kutokana na utekelezaji huo wa ahadi wananchi mbalimbali wameonekana kufurahishwa na aina ya kiongozi waliompata ambaye anaomba Ridhaa ya kuchaguliwa kuongoza Jimbo la Moshi Mjini. Haata hivyo katika mkutano wa Hadhara uliofanyika jana katika Soko hili ulihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mh. Mwigulu Nchimbi ambaye alipata fursa ya kumzungumzia Davis Mosha. Mwigulu alisema kazi ngumu kuliko zote ni kutomchagua Davis Mosha kuwa Mbunge wa Moshi mjini na kazi Rais sana ni kumchagua Davis Mosha. Aliwaambia wakazi wa Moshi kuwa wana bahati ya kipekee kupata Mbunge ambaye ameanza utekelezaji wa ahadi zake kabla ya kusubiri bajeti ya serikali na viongozi kama hao ndi o Tanzania inawahitaji, Kwahiyo ikifika 25 mwezi wa Kumi wasifanye kosa wamchague Davis Elisa Mosha awe Mbunge wa Moshi Mjini pamoja na Madiwani wake wa ccm na bila kusahau kumpa kura za Kishindo Mgombea Urais wa ccm Ndugu John Pombe Magufuli.

IT BRIDGE YAWAFIKIA WANAFUNZI 60,000

IMG_3000
Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome kuzindua maonesho ya Tehama yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Na mwandishi wetu
JUMLA ya wanafunzi 60,000 katika shule 150 nchini wamepitiwa na mafunzo ya programu ya Bridge IT yenye lengo la kuongeza ubora wa elimu kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kidijiti (digital technology) katika ufundishaji na ujifunzaji wa Hisabati,Sayansi na Stadi za Maisha.
Hayo yamsemwa na Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa akimkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome kuzindua maonesho ya Tehama.

Alisema kutokana na mafanikio yaliyotokea sasa wanatanua wigo baada ya kuwezeshwa kifedha na Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya elimu (Global Partnership For Education) kwa ajili ya kuendeleza teknolojia hiyo katika kujifunza na kufundisha katika shule za msingi na hasa darasa la awali la kwanza hadi la nne.

Aidha maonesho hayo yanayofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere yana lengo la kuonesha ubunifu ambao upo tayari kutumika kufanikisha mafunzo hayo.

Pia maonesho hayo yanatarajia kujadili na kuangalia mbinu za kielektroniki zitakazoweza kuendana na mazingira ya Tanzania katika ufundishaji na kujifunza kwa gharama nafuu.

Pia wanatarajia kuangalia utayari wa walimu na namna ya kuwabadilisha mtazamo ili waweze kufundisha na kufundishika.
“Lengo la serikali kupitia Wizara ya Elimu ni kupanua wigo wa elimu hasa elimu ya awali kwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano ambayo itabadilisha ufundishaji kutoka kutumia vitabu vilivyopo katika mfumo wa ‘hard copy’ na kuwa katika mfumo wa sauti na picha au ‘soft copy’,” alisema Profesa Bhalalusesa.
IMG_3089
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akifuatilia kwa makini risala Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa (hayupo pichani).

Alisema hadi kufikia wakati huu serikali imeshapiga hatua kubwa katika matumizi ya Tehama ambayo katika majaribio yake yameonesha kufanikiwa na wadau mbalimbali wa elimu wameyapongeza na kuyaunga mkono.

Profesa Bhalalusesa alisema kwa sasa wagunduzi mbalimbali wa mifumo ya Kompyuta inayoweza kutumika kufundishia ndio watakoonesha kazi zao na kutoa ufafanuzi wa kina kwa majaji wataochagua kazi chache na kuzifanyia majaribio kabla ya kuanza kutumika kufundishia.

Kwa Upande wake Mratibu wa Mpango wa Kukuza stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu kutoka Wizara ya Elimu, Agripina Habichi alisema mpango huo wa matumizi ya Tehama utasaidia wanafunzi kufahamu kusoma na kuandika kabla ya kuendelea na masomo ya darasa la tatu.

“Maonesho haya yanafanyika katika wakati muafaka ukizingatia tunataka kupiga hatua kubwa katika kuboresha elimu yetu. Washiriki wa maonesho haya wamekuja kutuonesha utawaalamu wao unaoweza kutumika kufundishia.

Lengo letu ni kuwafikia wanafunzi wengi zaidi ambapo tumeazimia kuzifikia shule zaidi ya 2000 katika mwaka wa fedha wa 2016/2017 na hivyo tutakuwa katika kiwango bora zaidi cha utoaji wa elimu inayojitosheleza,” alisema Habichi.
IMG_3142
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akizungumza kabla ya kuzindua rasmi maonesho ya Tehama yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katika maonesho hayo serikali imesema inatarajia kuanza kutumia rasmi Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) katika kufundishia wanafunzi kuanzia ngazi ya chini kabisa ya elimu ambayo ni chekechea.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome alisema matumizi ya Tehama katika ufundishaji wa wanafunzi wa chekechea yataimarisha kiwango cha elimu.
“Dunia imebadilika sana hasa katika sekta ya elimu na mawasiliano, hatuna budi kuendana nayo kwa kasi ileile ya ukuaji wake kwa kuimarisha mifumo yetu ya ufundishaji,” alisema Profesa Mchome.
Alisema wizara yake imeanzisha mpango maalum utakaosaidia wanafunzi kujifunza kwa njia ya kisasa ya kutumia mbinu za kielektroniki katika kujifunza na hivyo kuimarisha uelewa na kuongeza hamasa ya ufundishaji kwa wanafunzi.
Profesa Mchome alisema maonesho hayo yana lengo la kupata wadau mbalimbali waliobuni programu zinazoweza kutumika katika kufundishia kwa kutumia mifumo ya kielektroniki na hivyo watachaguliwa wachache wenye sifa na watakowezesha mafunzo hayo katika shule za Msingi na baadae katika ngazi ya sekondari.
IMG_3160
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akijianda kuzindua rasmi maonesho ya Tehama yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
IMG_3161
Sasa yamezinduliwa rasmi.
IMG_3214
Ofisa Miradi ya Elimu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika lake katika kuendeleza sekta ya elimu nchini kwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome (kushoto) mara baada ya kuzindua maonesho hayo ambapo pia UNESCO inashiriki. Katikati ni Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa.
IMG_3217
Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari (katikati) akimsikiliza mmoja wa wadau wa elimu aliyetembelea banda la UNESCO kwenye maonesho ya TEHAMA yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Miradi ya Elimu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo.
IMG_2982
Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari (kulia) akiwa na wadau wengine wa elimu wakipitia makbrasha mbalimbali katika mkutano huo.
IMG_3006
Pichani juu na chini ni baadhi wadau wa elimu waliohudhuria uzinduzi wa maonyesho hayo.
IMG_3004
IMG_3028
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi jijini Dar walioshiriki hafla hiyo.
IMG_3105
Mkurugenzi Mkuu wa Shule Direct, Faraja Nyalandu akipozi na wadau kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam yanakoendelea maonesho ya TEHAMA.