Sunday, May 31, 2015

VIJANA WA KAWE WASHIRIKI JOGGING

 Vijana wa Kawe wakishiriki Jogging.
 Gabriel Munasa (mwenye kaptura ya pink) akishiriki jogging pamoja na vijana wa Kawe,kushoto kwake ni Elias Nawera.





 Bendera ya Taifa ikiwa juu kuashiria kuhitimisha kwa mchakamchaka huo ambao mgeni rasmi alikuwa Gabriel Munasa.
 Gabriel Munasa akishiriki mazoezi ya viungo kwenye viwanja vya michezo vya Kawe.



 Gabriel Munasa akiongea na vyombo vya habari ambapo alielezea lengo na madhumuni ya kuwasaidia vijana kupitia vikundi vya jogging na pia alitumia fursa hiyo kuwaeleza nia yake ya kugombea ubunge kwa jimbo la Kawe na kama litagawanywa atagombea jimbo la Bunju.


Burudani baada ya mazoezi.

Rais Kikwete aongoza Mkutano wa Pili wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa EAC kuhusu Burundi


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa kwanza kulia) kwa pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museven (wa pili kulia), Rais wa Afrika Kusini, Mhe Jacob Zuma (wa tatu kutoka kulia), Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Mhe. Alain Nyamitwe (wa tatu kushoto) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Richard Sezibera (wa pili kushoto), wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kabla ya kuanza rasmi kwa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadili hali ya siasa na usalama nchini Burundi. Mkutano huo ulifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 31 Mei, 2015. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (wa pili kutoka kulia) akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Joyce Mapunjo na  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje (kulia)  nao wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Dkt. Richard Sezibera akisoma maazimio yaliyofikiwa mara baada ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kumalizika.
Kundi la Watu Maalum la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalofuatilia hali ya siasa na usalama nchini Burundi chini ya uongozi wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Jaji Joseph Sinde Warioba  wakifuatilia mkutano wa Wakuu wa Nchi wa EAC. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini.
Juu na Chini ni Wajumbe mbalimbali wakifuatilia mkutano wa wakuu wa nchi wa EAC
Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Mhe. Radhia Msuya (katikati) akiwa pamoja na Mkurugenzi Msaidizi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Burundi, Bibi Victoria Mwakasege nao wakifuatilia mkutano
Maafisa Mambo ya Nje nao wakifuatilia kwa makini mkutano 
Sehemu ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini nao wakifuatilia mkutano 
Mkurugenzi wa Idara ya Habari,  Bw. Assah Mwambene (katikati) kwa pamoja na Afisa Habari wa Sekretarieti ya Maziwa Makuu Bw. Macdonald Mwakasendile (kushoto) wakirekodi matukio 
Rais Kikwete akifuraia jambo na Rais wa Afrika Kusini Mhe. Zuma pamoja na Rais wa Uganda Mhe. Museveni mara baada ya kumaliza mkutano.
Rais Kikwete akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Bi.Nkoosazana Dlamini-Zuma kabla ya kuanza mkutano. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akiongozana na Rais wa Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta tayari kwenda kuanza mkutano wa kujadili hali ya usalama nchini Burundi .
Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula akizungumza jambo na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya,, Bw. Vervaeke.

....Kuwasili kwa viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Mulamula akisalimiana na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyetta akipita kwenye Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili nchini
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Harrison Mwakyembe akimtambulisha Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula kwa Rais wa Uganda mara baada ya kumpokea Rais huyo alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Rais Museven akipita katikati ya  Gwaride la heshima. 
Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini Balozi Radhia Msuya akisalimiana na Rais wa Afrika ya Kusini alipowasili nchini
Picha ya Pamoja baada ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.Picha na Reginald Philip

UHAMIAJI YASHIRIKI KATIKA MAONYESHO YA KARIBU TRAVEL MARKET FAIR, JIJINI ARUSHA

Waziri wa Utalii na Mali Asili, Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb.) akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Afisa Uhamiaji, Rosemarry Mkandala wakati alipotembelea Banda la Idara ya Uhamiaji mara baada ya kufungua rasmi Maonesho ya Utalii “Karibu Travel Market Fair” mnamo tarehe 29.05.2015 yaliyofanyika katika viwanja vya Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha.
Waziri wa Utalii na Mali Asili, Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb.) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la Idara ya Uhamiaji tarehe 29.05-2015 na kuipongeza Idara ya Uhamiaji kwa juhudi zake za kuendelea kushiriki kwenye Maonesho ya Utalii “Karibu Travel Market Fair” yaliyofanyika katika viwanja vya Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha ambapo pia alisisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya Taasisi hizo mbili katika kukuza sekta ya Utalii nchini.
Waziri wa Utalii na Mali Asili, Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb.) akipokea machapisho mbali mbali yanayolenga kuelimisha jamii taratibu za Utoaji wa Huduma za Uhamiaji nchini, mapambano dhidi ya Uhamiaji Haramu na makosa mengineyo ya Kiuhamiaji, wakati alipotembelea Banda la Idara ya Uhamiaji kwenye Maonesho ya Utalii “Karibu Travel Market Fair” yaliyofanyika katika viwanja vya Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha.
Maafisa wa Uhamiaji wakitoa Elimu juu ya masuala mbali mbali ya Kiuhamiaji nchini kwa wananchi na wadau mbali mbali walipotembelea Banda la Idara ya Uhamiaji wakati wa Maonesho ya Utalii “Karibu Travel Market Fair” yaliyofanyika katika viwanja vya Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha jana.
Afisa Uhusiano wa Idara ya Uhamiaji, Tatu Burhan akizungumza na mgeni alietaka kujua taratibu za kupata vibali vya ukaazi nchini, wakati alipotembelea Banda la Idara ya Uhamiaji jana (30.05.2015) kwenye Maonesho ya Utalii “Karibu Travel Market Fair” yaliyofanyika katika viwanja vya Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha.
Kamishna wa Uhamiaji (Utawala na Fedha), Piniel O. Mgonja, akisaini kitabu cha wageni na kupokea taarifa ya Ushiriki wa Idara kutoka kwa Afisa Uhusiano wa Idara ya Uhamiaji, Tatu Burhan alipotembelea Maonesho ya Utalii “Karibu Travel Market Fair” jana (30.05.2015) yaliyofanyika katika viwanja vya Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha.
Kamishna wa Uhamiaji (Utawala na Fedha), Piniel O. Mgonja, akiwa pamoja na Maafisa Walioshiriki kwenye Maonesho ya Utalii “Karibu Travel Market Fair” yaliyofanyika katika viwanja vya Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha. Kulia kwake ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Arusha, Naibu Kamishna Danson Mwakipesile, akifuatiwa na Naibu Kamishna wa Uhamiaji Vitalis Mlay, kushoto kwake ni Afisa Uhusiano wa Idara ya Uhamiaji Tatu Burhan.

Kamishna wa Uhamiaji (Utawala na Fedha), Piniel O. Mgonja, akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya Uhamiaji wakati akizungumza na vyombo vya habari jana (30.05.2015) walipotembelea Banda la Idara ya Uhamiaji kwenye Maonesho ya Utalii “Karibu Travel Market Fair” yaliyofanyika katika viwanja vya Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha.
Baadhi ya wageni wakichukua machapisho mbali mbali ili kuelewa vyema masuala mbali mbali ya Kiuhamiaji nchini, wakati walipotembelea Banda la Idara ya Uhamiaji kwenye Maonesho ya Utalii “Karibu Travel Market Fair” yaliyofanyika katika viwanja vya Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha jana.

Wananchi waishukuru serikali kuwajengea uwezo wa kupunguza athari za maafa ya ukame

Na. Mwandishi Maalum

Wananchi wa Wilayani  Same katika  kata ya Hedaru, Makanya na Vunta wameishukuru serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya uratibu maafa, kwa kuwajengea uwezo wa kuzuia, kupunguza na kukabiliana na maafa yanayotokana na ukame ambao umekuwa ukizisumbua kata hizo Kutokana na mabadiliko ya Tabia Nchi.

Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Mradi wa kujengea jamii uwezo wa kukabili maafa ya ukame imefanikiwa kujenga uwezo huo kupitia vikundi vya maendeleo vya wilayani humo, ikiwa vikundi kumi (10) kutoka kata tatu za wilaya hiyo vimepatiwa  Mbuzi 40, kuku 50, mbegu za mihogo, viazi, mtama, mboga mboga pamoja na kutoa miche ya miti kwa shule moja kila kata na vifaa vya kutunza bustani.  
Akiongea wakati Idara hiyo ilipokuwa ikifuatilia utekelezaji wa mradi huo hivi karibuni,  wilayani humo katika kata ya Makanya,  kijijini  Mgwasi, Mwenyekiti wa kikundi cha Kavangere, Stephano Hamisi, alieleza kuwa wananchi wa kata hiyo kupitia ufadhili wa mradi huo wameweza  kulima na kufuga hali inayowajengea uwezo wa  kupunguza na kukabiliana na maafa yanayotokana na ukame. 

“Tunaishukuru serikali kwa mradi huu,  kwani tunao uwezo wa kuzuia, kupunguza na kukabiliana na maafa yanayotokana na ukame kwa kuwa tulipewa mbegu za mazao yanayo himili ukame na yanayo stawi haraka kwa kipindi kifupi cha mvua, kwa mantiki hiyo tunao uhakika wa chakula lakini pia uhakika wa kipato kwa  kilimo cha bustani, ufugaji wa mbuzi na kuku ambazo tumewezeshwa na mradi huu ” alisema Hamisi.

Aliongeza kuwa katika vikundi ambavyo vimewezeshwa na mradi huo wanao utaratibu wa kila mwana kikundi kupata mbuzi (5) na wengine ambao hawapati mbuzi hupewa kuku (5) ambapo wanakikundi hubadilishana mifugo hiyo kwa kadri wanavyo endelea kuzaliana lengo likiwa ni kila mwanakikundi kufuga mbuzi pamoja na kuku.
Mratibu maafa wilayani Same, Ally mngwaya anaeleza kuwa mradi huo umeweza pia kuzijengea jamii uwezo wa kuzuia maafa ya ukame kwa kuhamasisha upandaji miti, ambapo shule za wilayani humo zimeshirikishwa ili kujenga kizazi chenye uwezo wa kukabiliana na kupunguza vihatarishi vinavyoweza kusababisha maafa ya ukame katika kata zao.

“ Kwa kata tatu zinazofadhiliwa na mradi huu tumechagua shule moja kila kata na tayari viriba vya miche 2500 vimegawiwa katika shule za wilaya hii ikiwa lengo ni kufikia miche 5000. Tukipanda miti ya kutosha katika kata hizi na tukaachana na  shughuli za kibinadamu zinazochangia sana kutokea kwa ukame kama ukataji na uchomaji wa miti ovyo na uharibifu wa vyanzo vya maji, ninaamini tutakuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia, kukabili na kupunguza athari zitokanazo na ukame” alisisitiza Mngwaya.

Awali akiongea katika kata hizo, Mratibu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wa Mradi huo, Harrison Chinyuka alifafanua kuwa mradi huo umefanikiwa kuwajengea uwezo wananchi  wilayani Same kwa kuwa umewatumia  wataalam waliopo katika ngazi ya Kata za wilaya hiyo katika   kuijengea uwezo jamii hiyo  wa kuzuia, kupunguza na kukabiliana na maafa yanayotokana na ukame.
“katika kutekeleza mradi huu tumewatumia  wataalam wa Sekta ya Kilimo, Mifugo, Afya, Elimu na Utawala wa kata za wilaya hii kwani wataalamu hawa wapo karibu na jamii inayopata athari za ukame, kupitia wataalamu hawa jamii hii imeweza  kuelewa vihatarishi vinavyoweza kusababisha maafa ya ukame na  matumizi ya mbegu na pembejeo za kilimo, mifugo na misitu pamoja na upatikanaji wa maji safi na salama kwa matumizi ya binadamu na mifugo”  alisema Chinyuka.

Mradi Wa Kuijengea Jamii Uwezo Wa Kupunguza Athari Za Maafa Kwa Mikoa Iliyoathirika Zaidi Na Ukame umefadhiliwa na Benki ya Dunia na kusimamiwa na UNICEF chini ya Uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu Maafa, na Halmashauri husika wakiwa Watendaji Wakuu wa Mradi huo. Mradi huo unatekelezwa kwa kipindi cha miezi 18 uliozinduliwa Wilayani  Same, mkoani Kilimanjaro tarehe 11 Desemba 2013.