Spika wa Bunge la Jumuiya ya
AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Margareth Zziwa akipanda mti katika eneo la Taasisi ya Sanaa na Utamaduni
Bagamoyo (TaSuBa) jana wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki. Upandaji wa mti huo ni katika kutekeleza azimio la Jumuiya ya Afrika
Mashariki katika jitihada za kutunza mazingira
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara
(MB) akipanda mti katika eneo la Taasisi
ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) jana wakati wa ziara ya Wabunge wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki. Upandaji wa mti huo ni katika kutekeleza azimio la
Jumuiya ya Afrika Mashariki katika jitihada za kutunza mazingira.
Spika wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki
(EALA) Mhe. Margareth Zziwa (Kulia) akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa
wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo
(TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao wakati wa ziara ya Wabunge wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana mjini Bagamoyo.
Mmoja wa wabunge wa Bunge la Jumuiya ya
AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Susan Nakawuki (mwenye blauzi ya pinki) akinunua bidhaa
kutoka kwa mmoja wa wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi
wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni
Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao wakati wa ziara ya
Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akiweka saini katika daftari la wageni katika
moja ya kikundi cha wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi
wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni
Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao kwa wakati wa ziara
ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana.
Baadhi ya Wabunge wa Afrika Mashariki
akiwemo Mhe. Shyrose Bhanji anayewakilisha
Tanzania katika bunge hilo wakiangali kazi za sanaa ya uchingaji kutoka
kwa mmoja wa wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo
(TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao kwa wakati wa ziara ya
Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana.
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Shyrose
Bhanji wa Tanzania akimkabidhi zawadi ya sinia lililotokana na kazi za
uchongaji Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Margareth Zziwa mara baada ya
kupenda bidhaa hiyo na kuamua kumnunulia spika huyo jana wilayani Bagamoyo
wakati wa ziara ya Wabunge wa Afrika Mashariki katika Taasisi ya Sanaa na
Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa).
Katikati ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki
ambaye pia ni mtoto wa Baba wa Taifa Mhe. Makongoro Nyerere (katikati)
akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afika Mashariki wa Serikali ya Tanzania Bibi. Joyce Mapunjo na
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabriel walipokuta katika viwanja vya Taasisi ya Sanaa na
Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) wakati wa ziara ya wabunge wa Afrika Mashariki
katika Taasisi hiyo.
Spika wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki
(EALA) Mhe. Margareth Zziwa (Kulia) akikabidhi kitabu cha mpango mkakati wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo
(TaSuBa) Bw. Michael Kadinde wakati wa ziara ya Wabunge wa Afrika Mashariki.
TaSuBa ni taasisi pekee katika ukanda wa Afrika Mashariki uliopewa dhamana ya
kuwa Kituo cha Maarifa katika Nyanja za Sanaa na Utamaduni
Spika wa Bunge la Jumuiya ya
AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Margareth Zziwa (Kulia) akikabidhi kitabu cha
mpango mkakati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe Ahmed Chipozi jana wilayani Bagamoyo wakati wa ziara ya Wabunge wa Afrika
Mashariki katika taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSuBa). Anayeshuhudia katikati
ni Waziriwa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara
(MB).
Spika wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA)
Mhe. Margareth Zziwa (Kushoto) na Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB).wakiwa
na baadhi ya Wabunge wa Afrika Mashariki wakipata maelezo kuhusu muelekeo na
malengo ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) kutoka Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi
hiyo Bw. Michael Kadinde jana wakati wa ziara ya wabunge hao.
Kikundi cha Sanaa kutoka Taasisi ya Sanaa na
Utamaduni (TaSuBa)wakifanaya sanaa za maonyesho kwa mchezo aina ya Akrobati mbele ya wageni ambao ni wabunge wa
Afrika Mashariki wakiongozwa na Spika wa Bunge hilo Mhe. Margareth Zziwa
(Hawapo picha) walipotembelea taasisi hiyo jana mjini Bagamoyo.
Kikundi cha Sanaa kutoka Taasisi ya
Sanaa na Utamaduni (TaSuBa)wakichezo ngoma yenye asili ya kabila la Kisukuma
ijulikanayo kama Gobogobo mbele ya wageni ambao ni wabunge wa Afrika Mashariki
wakiongozwa na Spika wa Bunge hilo Mhe. Margareth Zziwa (Hawapo picha)
walipotembelea taasisi hiyo jana mjini Bagamoyo.
Baadhi ya wageni wakifurahia ngoma wakati wa
ziara ya wabunge wa Afrika Mashariki jana mjini Bagamoyo walipotembelea Tasisi
ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa).
Kutoka kulia mwenye skafu niNaibu Waziri
wa Afrika Mashariki wa Tanzania Dkt.Abdulla Juma Abdulla, Spika wa Bunge la
Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Margareth Zziwa (mwenye miwani), Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB), Mbunge
wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere, Mwenyeki ti wa Bodi wa
TaSuBa Bw. Abraham Bafadhili na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TaSuBa Bw. Michael
Kadind wakiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa kikundi cha sanaa kutoka
taasisi hiyo wakti wa ziara ya wabiunge wa Afrika Mashariki katika taasisi hiyo
jana.