Saturday, March 30, 2013

DKT. SHEIN AHUDHULIA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YASIKU YA MTOTO YATIMA,ZANZIBAR LEO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea zawadi kutoka kwa Mtoto Hinaina Said Khalfan,wakati wa sherehe za siku ya Mtoto yatima zilizofanyika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel leo Mjini Zanzibar,shirika la misaada la I.H.H la Uturuki,kwa Ushirikiano na jumuiya ya Muzdalifa ya hapa Zanzibar kwa pamoja wamefanikisha kufanyika kwa sherehe hizo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti Muzdalifa,Sheikh Abdalla Hadhal,alipoangalia maonesho ya picha mbali mbali wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto Yatima katika Ukumbi wa Salama Bwawani leo, maadhimisho hayo yamefanywa na Shirika la I.H.H la nchini Uturuki kwa ushirikiano na Jumuiya ya Muzidalifa ya hapa Zanzibar inayoshuhulika kna Mayatima.
Baadhi ya Wazee na Wanajumuiya ya Muzdalifa wallipohudhuria katika sherehe ya Siku ya Mtoto wa Yatima,katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Zanzibar,wakisikiliza kwa makini Hotuba ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,aliyoitoa katika hafla hiyo leo.
Watoto Yatima waliohudhuria katika sherehe za maadhimisho ya siku ya Mtoto Yatima,wakiwa katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Zanzibar,zilipofanyika sherehe hizo,kwa ushirikiano wa jumuiya ya Muzdalifa na shirika la misaada la I.H.H la Nchini Uturuki leo na kuhudhuriwa na wananchi na Viongozi mbalimbali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea risala kutoka kwa Nasra Suleiman Abdalla,wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Mtoto yatima zilizofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini zanzibar.
Wanajumuiya wa Musdalifa inayoshuhulika na Watoto Mayatima,yemye makamo makuu yake Amani Mjini Zanzibar,wakiwa katika Sherehe za kuadhimisha siku ya Mtoto yatima,katika Ukumbi wa Salama Bwawani leo,na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa hutuba yake wakati wa Sherehe ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto Yatima katika ukumbi wa Salama bwawani Mjini Zanzibar leo,maadhimisho hayo yamesimamiwa na jumuiya ya Muzidalifa na Shikika la misaada la I.H.H la Nchini Uturuki,(kushoto) makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif,Balozi wa Uturuki Nchini Ali Daudi Gul,na Waziri wa Katiba na Sheria,Abubakar Khamis Bakary,(kulia).
Watoto Yatima waliohudhuria katika sherehe za maadhimisho ya siku ya Mtoto Yatima,wakiwa katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Zanzibar,zilipofanyika sherehe hizo,kwa ushirikiano wa jumuiya ya Muzdalifa na shirika la misaada la I.H.H la Nchini Uturuki leo na kuhudhuriwa na wananchi na Viongozi mbalimbali. [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Serikali itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inafikia hatua nzuri katika kutoa huduma kwa jamii hasa watoto mayatima huku akisisitiza haja ya kuwalea katika maisha bora na yenye furaha.

Dk. Shein aliyasema hayo leo katika sherehe ya siku ya motto yatima, zilizofanyika katika ukumbi wa Salama Bwawani mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Balozi wa Uturuki Mhe. Ali Daud Gul,wazee, wazazi pamoja na watoto yatima kutoka ndani na nje ya Zanzibar.

Dk. Shein alisema kuwa azma ya Serikali ni kujenga misingi imara kwa jamii ya watoto na watu wazima ili kuwajengea wananchi maisha bora zaidi.

Alisema kuwa hatua za kusaidia watoto yatima zinakwenda sambamba na juhudi za serikali ya Mapinduzi Zanzibar tokea kuasisiwa na Marehemu Mzee Abeid Amani Karume alipofungua nyumba ya watoto yatima Forodhani mara tu baada ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964.

Aliongeza kuwa katika kuendeleza huduma hiyo, Serikali ikishirikiana na Taasisi ya ZAYEDESA imewahamisha watoto yatima kwenda nyumba ya kisasa Mazizini na inatoa ushiriki mkubwa na Taasisi ya SOS katika kuendeleza kijiji cha watoto yatima Mombasa Unguja ambapo ipo skuli ya msingi na Sekondari pamoja na kupitisha Sheria Namba 6 ya mwaka 2011 yenye lengo la kuhakikisha haki za watoto, ulizni na ustawi wao.

Katika hotuba yake hiyo Dk. Shein alisema kuwa misaada na shughuli zao ni kuipunguzia mzigo Serikali ambayo hutumia kiasi kikubwa cha fedha katika uimarishaji wa sekta hizo hapa Zanzibar.

Dk. Shein aliwanasihi wazazi kuunga mkono juhudi za Jumuiya ya Muzdalifa kwa kuwekeza katika kuwalea vyema watoto yatima ambao mara nyingi wanakuwa nyuma.

Alieleza kuwa wazazi na walezi wanawajibu mkubwa kwa watoto yatima kwa kuwapa elimu, chakula kizuri, kuwapenda na kuwakinga na unyanyasaji, hasa wa kijinsia jambo ambalo litapelekea kuwa na vijana madhubuti walio na afya njema, elimu na uzalendo

“Suala la malezi mema kwa watoto yatima ni la lazima kwani wasemavyo wahenga’usipoziba ufa utajenga ukuta”,alisema Dk. Shein.

Aidha, Dk. Shein alieleza kuwa kuvunjika kwa amani ni miongoni mwa mazingira yanayosababishwa na binaadamu na kupelekea kuwepo kwa watoto yatima wengi.

Alisema kuwa dunia imekuwa ikishuhudia hali ilibvyokuwa mbaya katika baadhi ya nchi, Mashariki ya Kati, Asia na hata eneo la Afrika ambapo maelfu ya watoto wamebakia yatima kutokana na kukosa amani.

Alisisitiza kuwa hali hiyo inabainisha umhyimu wa kutunza amani na usalama kwani bila ya amani ni mtafaruku wa jamii na kuhatarisha maisha ya watoto.

Pamoja na hayo, Dk. Shein alitoa nasaha kwa jamii kujali na kudumisha amani miongoni mwa jamii pamoja na kujikinga na maradhi thakili na hatari ya ukimwi kwani ni maradhi yanayosababisha vifo vya wazazi na hatimae kuwaacha watoto yatima.

Dk. Shein alieleza haja ya kuzingatia hali iliyojitokeza nchini hivi sasa ya kuwepo watoto wanaoishi katika mazingira magumu ambapo wengine hukosa mahala pa kula, kulala, hawapati elimu na kwa jumla wanakuwa hawana mwelekeo mwema wa maisha yao.

“Ni wajibu wetu tushirikiane ili tuweze kuwaondoshea hali hii watoto wetu…naipongeza Wizara ya Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto kwa jitihada zao ni vyema taasisi nyengine zikashiriki katika kuliondoa tatizo hili ambalo lipo mijini”,aliongeza Dk. Shein.

Sambamba na hayo, Dk. Shein aliitaka Wizara ya Katiba na Sheria kuendelea kuwa karibu na Jumuiya ya Muzdalifah na kutoa shukurani kwa Jumuiya zote za ndani na nje ya Zanzibar zikiwemo I.H.H ya Uturuki, WEFA ya Ujerumani na Al-ANSAR FOUNDATION ya Uiengereza kwa kutoa michango yao mikubwa ya kuiunga mkono Jumuiya ya Muzdalifah ili iweze kufaya kazi zake vizuri.

Nae Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Abubakar Khamis, alieleza kuwa Serikali imekuwa ikishirikiana na taasisi mbali mbali katika kuhakikisha watoto yatima wanapata huduma zinazostahiki ili waweze kuishi vizuri.

Nae Mbunge Mstaafu wa Bunge la Uturuki Mhe. Husnu Tuna akitoa salamu zake kutoka kwa Jumuiya ya I.H.H alisema kuwa tatsisi hiyo imekuwa ikitoa misaada ya kibinadamu ambayo lengo lake ni kuondoa matatizo ya watoto mayatima ambapo imekuwa ikiiunga mkono Tanzania kwa mwaka wan ne hivi sasa na inalea mayatima 29,000 katika nchi 41.

Aidha, katika risala yao Jumuiya ya Muzdalifah ilieleza kuwa imekuwa ikitoa huduma mbali mbali zikiwemo huduma za kuwasaidia watoto yatima, huduma afya, maskulini, madrasat, zakka, sadaka, maafa, kuchimba visima na huduma nyenginezo.

Nao watoto yatima walieleza furaha zao kwa mgeni rasmi kwa kuungana nao katika siku yao hiyo adhimu na kutoa ombi lao la kuitaka siku hii iwe ya Kitaifa.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar.

Viongozi mbali mbali washiriki Mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Chambani Pemba, Marehemu Salim Hemed Khamis (CUF)

  Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Gando (CUF),Mh. Khalifa Suleiman Khalifa wakati wa kuwasili kwa Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Chambani Pemba, Marehemu Salim Hemed Khamis (CUF) aliyefariki dunia juzi katika Hosptilai ya Muhimbili,jijini Dar es Salaam.Kulia ni Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge,Mh. William Lukuvi.
Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda akisalimiana na Baadhi ya Viongozi waliofika uwanjani hapo kuupokea Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Chambani Pemba, Marehemu Salim Hemed Khamis (CUF) aliyefariki dunia juzi katika Hosptilai ya Muhimbili,jijini Dar es Salaam.
Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Chambani Pemba, Marehemu Salim Hemed Khamis (CUF) ukishushwa kutoka kwenye ndege mara baada ya kuwasili.
Mwili ukibebwa tayari kwa kuelekea kwenye Mazishi.

Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda akisaini kitabu cha Maombolezo huku akishuhudiwa na Mbunge wa Jimbo la Gando (CUF),Mh. Khalifa Suleiman Khalifa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisaini kitabu cha Maombolezo.
Mwili ukielekea Makaburini.
Viongozi mbali mbali wakiongozwa na Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda wakisoma dua mbele ya Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Mh. Maalim Seif Shariff Hamad akiongea jambo na viongozi wengine wakati wa Mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Chambani Pemba, Marehemu Salim Hemed Khamis (CUF),aliefariki katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam juzi.
Taratibu za Mazishi zikiendelea.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Mh. Maalim Seif Shariff Hamad akiweka udongo kaburini.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiweka udongo kaburini.Picha zote na Owen Mwandumbya,Bunge.

Friday, March 29, 2013

HIVI NDIVYO MAMBO YALIVYO ENEO LA JENGO LILILOPOEROMOKA LEO


Hivi ndivyo lionekanavyo jengo hilo mara baada ya kuporomoka na asubuhi ya leo na kupelekea watu kadhaa kufukiwa na kifusi hicho wakiwepo watoto waliokuwa wakicheza mpira jirani na jengo hilo.
Watu wengi wakiwemo ndugu wa watu waliokuwepo kwenye jengo hilo wakiangalia hata ya kuokolewa kwa ndugu zao.
Juhudi za uokoaji zikiendelea japo kuna uhaba mkubwa sana wa vifaa vya uokoaji.
Moja ya Magreda yaliopo eneo hilo la tukio likiendelea na kazi  ya kutoa kifusi ili kurahisisha kazi ya uokoaji.
Kikukweli hali bado ni tete katika uokoani,maaka pia kuna ufinyu wa nafasi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick akiwasili eneo la tukio ili kuungana na waokoaji wengine kwenye zoezi hilo.
Watu wanajitahidi kwenye uokoani,lakini kuna uhaba wa vifaa vya uokoaji.
Mkuu wa Mkoa akisogea eneo la tukio.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Mh. Said Meck Sadick akipatiwa maelezo ya namna ya uokoaji kutoka kwa maafisa wa kikosi cha Uokoaji.
Wanajitahidi lakini wanakwamishwa na vifaa.
Wadau wakionyesha nondo zilizokuwa zimejengewa kwenye jengo hilo wakimaanisha kuwa hazina ubora.
Magari yaliyokuwepo jirani na jengo hilo yakiwa yameangukiwa na kifusi.
Kazi ikiendelea huku wengine wakiwa hawaani kilichotokea.
Mawasiliano ya hapa na pale yakiendelea kuhakikisha utaratibu wa uokoaji unafanikiwa.


Kikosi ya Msalaba mwekundu kipo eneo la tukio.
Ulinzi mkali.
Mdau akiwahisha ngazi kwa ajili ya kuendeleza zoezi zima la uokoaji.

Mpiga picha wa Magazeti ya Serikali ya Daily & Sunday News na Habari leo,Mohamed Mambo akiwajibika kuhakikisha anapata picha bora.
Kumbukumbu ikichukuliwa.


Mh. James Mbatia akijadiliana jambo na mmoja wa wadau walipo eneo la tukio.