Friday, January 19, 2018

WANANCHI NJOMBE WAKIRI KUKWAMA KATIKA BAADHI YA HUDUMA KWA KUKOSA VITAMBULISHO VYA TAIFA

Wananchi wa mkoa wa Njombe wameonyesha mwamko mkubwa kujitikoza kwa wingi kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa wakielezea namna wanavyotegemea kuvitumia katika kupata huduma mbalimbali za kijamii.

Wilaya ya Njombe Halmashauri ya Mji wa Makambako, ambako zoezi la usajili linaendelea hivi sasa, wananchi wengi wamekiri kupoteza muda wao mwingi kufuatilia kupata vitambulisho vya Taifa kutokana na Umuhimu mkubwa wa Vitambulisho hivyo katika huduma mbalimbali za kijamii.

Bwana Alphonce Mtengela mkazi wa Njombe akiwa anasubiri kupata huduma amesema “Sasa hivi kila mahali wanahitaji Kitambulisho cha Taifa ili waweze kukuhudumia, nimekwama kuchukua Mkopo baada ya kutokuwa na Kitambulisho cha Taifa hivyo kuna haja ya kuwa nacho ili iwe rahisi kutambulika katika huduma za Kijamii”

Wananchi wa Mkoa wa Njombe katika Wilaya za Njombe, Ludewa, Wanging’ombe, Makete na Makambako wanaendelea na zoezi la Usajili utakaomalizika mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu.


Ndugu Nicholaus Lugandu mkazi wa Kijiji cha Ikelu Kata ya Ikelu Wilaya Njombe akichukuliwa alama za Vidole wakati akipatiwa huduma ya usajili na Utambuzi uliohusisha uchukuaji wa alama za Kibaiologia, saini ya Kielektroniki pamoja na Picha, zoezi linaloendelea hivi sasa katika Wilaya ya Njombe Halmashauri ya Mji wa Makambako.




Wakazi wa Kijiji cha Lyamkena Halmashauri ya Mji Makambako wakiwa nje ya Moja ya kituo cha Usajili wilayani Njombe wakisubiri kupatiwa huduma ya Usajili na Utambuzi ili kupatiwa Vitambulisho vya Taifa.


  
Wanakijiji wa Kata ya Ikelu Kijiji cha Ikelu wakiwa kwenye foleni kusubiria huduma ya Usajili na Utambuzi katika moja ya vituo vya Usajili katika kata hiyo.
Bwana Alphonce Mtengela wa Kijiji cha Lyamkena Kata ya Lyamkena Wilaya Njombe akichukuliwa alama za Vidole wakati akipatiwa huduma ya usajili na Utambuzi uliohusisha uchukuaji wa alama za Kibaiologia, saini ya Kielektroniki pamoja na Picha, zoezi linaloendelea hivi sasa katika Wilaya ya Njombe Halmashauri ya Mji wa Makambako.
Bi. Anusiata Mwakalebela mwananchi mkazi wa wa Kijiji cha Lyamkena Kata ya Lyamkena Wilaya Njombe akichukuliwa alama za Vidole wakati akipatiwa huduma ya usajili na Utambuzi uliohusisha uchukuaji wa alama za Kibaiologia, saini ya Kielektroniki pamoja na Picha, zoezi linaloendelea hivi sasa katika Wilaya ya Njombe Halmashauri ya Mji wa Makambako.

No comments: