Tuesday, January 16, 2018

TIMU YA USIMAMIZI WA HUDUMA YA AFYA WILAYA YA LINDI YAAGIZWA KUSIMAMIA UKARABATI WA VITUO VYA AFYA

Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (mbele), akishuka ngazi wakati wa ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa unaojengwa na Wakala wa Majengo (TBA), mkoa wa Ruvuma na kuridhishwa na kasi ya ujenzi huo.
Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA), mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Edwin Nunduma, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (hayupo pichani), kuhusu hatua na changamoto wanazozipata katika miradi ya ujenzi wa jengo la ofisi na nyumba ya makazi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa mkoani humo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kukagua miradi ya ujenzi wa jengo la ofisi na nyumba ya makazi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma. Miradi hiyo inajengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
Muonekano wa hatua ya awali ya ujenzi wa jengo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, mkoani Ruvuma. Mradi huo unajengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA). 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (katikati) akizungumza na Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Ruvuma, Eng. Lazeck Alinanuswe (kulia), wakati akikagua barabara ya Mbinga-Mbamba Bay yenye urefu wa KM 67 inayotarajiwa kujengwa hivi karibuni kwa kiwango cha lami na mkandarasi CHICO. 
 Muonekano wa barabara ya Mbinga-Mbamba Bay yenye urefu wa KM 67 inayotarajiwa kujengwa hivi karibuni kwa kiwango cha lami na mkandarasi CHICO. Mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo ulisainiwa tarehe 11 mwezi Disemba mwaka jana.





Wananchi wa Mbamba Bay wilayani Nyasa, mkoani Ruvuma wameiomba Serikali kuharakisha ujenzi wa barabara ya Mbinga-Mbamba Bay (km 67), kwa kiwango cha lami ili kutatua changamoto za usafirishaji wa abiria na mizigo wanazozipata hususan katika kipindi cha masika.

Wananchi hao wametoa kero hiyo mbele ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, alipofika wilayani hapo kukagua barabara hiyo ambapo wamefafanua kuwa licha ya wilaya hiyo kuwa na maliasili nyingi, wawekezaji na wafanyabiashara hushindwa kufika kutokana na changamoto ya barabara, hivyo kupelekea uchelewaji wa maendeleo katika wilaya yao.

"Uduni wa barabara hii unapelekea kutopata maendeleo ya haraka, pia usafiri kutoka hapa kwenda maeneo mengine ya jirani huwa mgumu hususan katika kipindi cha mvua kwani madereva wengi hupandisha nauli", amesema mmoja wa wakazi wa Mbamba Bay, Bw. Bahati Ndege.

Aidha, wananchi hao wameipongeza Serikali kwa hatua zinazofanya katika utatuzi wa kero mbalimbali zinazowakabili, hivyo wamefafanua kuwa Serikali kuamua kujenga barabara ya lami kutaboresha uchumi katika wilaya yao na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla. 

Kwa upande wake, Naibu Waziri Elias Kwandikwa, amesema kuwa mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo umesainiwa tangu Mwezi Desemba mwaka jana na kufafanua kuwa kinachosubiriwa sasa ni kwa mkandarasi kufika eneo la mradi na kuleta mitambo yake.

"Kila kitu kipo tayari, Wananchi wasubiri kwa hamu ujenzi wa barabara hii ambao unatarajiwa kujengwa kwa shilingi bilioni 129 na mkandarasi CHICO kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika", amesema Naibu Waziri Kwandikwa.

Amepongeza uongozi wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoani humo kwa kuweka changarawe katika barabara hiyo ambapo kwa namna moja inasaidia kurahisisha usafiri kwa kipindi hiki ambacho mkandarasi anasubiriwa kufika eneo la kazi.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo amekagua mradi wa ujenzi wa Ofisi na Nyumba ya Makazi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa zinazojengwa na Wakala wa Majengo (TBA), mkoani humo na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wake.

Naye, Meneja wa TBA mkoani humo, Mhandisi Edwin Nunduma, amesema kuwa TBA katika wilaya hiyo ina jumla ya miradi minne inayoendelea kwa sasa ikiwemo mradi wa ujenzi wa zahanati, nyumba na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ambapo amemhakikishia Waziri huyo kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.

Naibu Waziri Kwandikwa ameanza ziara ya kikazi mkoani Ruvuma ambapo leo amekagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara yake ili kujionea maendeleo yake.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

No comments: