Friday, August 18, 2017

UNESCO YAKABIDHI VIFAA VYA RADIO ZA KIJAMII VYA MAMILIONI

SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limekabidhi vifaa vya radio kwa radio za jamii nne vyenye thamani ya mamilioni ya shilingi. Unesco imesema kwamba utoaji wa vifaa hivyo umelenga kuongeza usikivu wa mawimbi ya radio katika maeneo ya vijijini. Shughuli ya kukabidhiana imefanyika Agosti 17 mwaka huu.

 Akizungumza wakati wakukabidhiana vifaa hivyo Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues alisema kwamba UNESCO inatambua kazi nzuri zinazofanywa na radio hizo za jamii za kuwafikia wananchi wengi zaidi. Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kushoto) akizungumza jambo wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya radio jamii iliyofanyika katika ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.[/caption] Aidha alisema ni muhimu sana kwa radio hizo za jamii kujiangalia na kujitunza zenyewe ili wasiingie katika matata na kuchapisha au kutangaza stori baada ya kukamilika kwake.

 Alisema ipo haja kwa vyombo vya habari kufanyakazi kwa mujibu wa taratibu zao na kuhakikisha kwamba hawachapishi habari ambazo zinahatarisha uwapo wa uandishi unaozingatia maadili. Meneja wa radio ya Jamii ya Baloha FM, Samada Maduhu aliishukuru UNESCO kwa kusaidia kituo chake na kwamba wanatarajia kufikia wilaya tano. Meneja wa radio ya Jamii ya Baloha FM ya Kahama, Samada Maduhu, akitoa neno la shukrani kwa ofisi za Unesco wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo yaliyofanyika katika ofisi za Shirika hilo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa mtaalamu wa Mawasiliano Unesco, Nancy Kaizilege Angulo.

Alishukuru UNESCO kwa kuwawezesha kufika katika wilaya tano na kwamba kwa msaada huo wataokoa shilingi laki saba kwa mwezi kuazima transmita. “Radio yetu inawafikia watu 500,000 lakini kwa kupatiwa hivi vifaa tutaweza kufikia watu milioni 1 katika wilaya zaidi ya tano za Kahama, Shinyanga Vijijini, Nyang’wale na Mbogwe mkoani Geita na pia Nzega na Uyui mkoani Tabora ,” alisema meneja huyo . Kwa mujibu wa Maduhu, kama wasingelipata transmita hiyo wangelikuwa wanatumia sh milioni 8.4 kwa mwaka. Ofisa Utawala na Rasilimali Watu wa Radio Jamii ya Pangani FM, Rehema Kilapilo akitoa shukrani kwa uongozi wa Unesco wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa vya redio iliyofanyika katika ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.[/caption] Kwa upande wake, Ayubu Kalufya wa radio ya jamii Uvinza alisema kwamba kituo chake kilikuwa kinakodisha transmita kwash laki tano na kufanya kwa mwaka mzima kutumia sh milioni 6.

 Alisema kwa kupata vifaa hivyo walikuwa wanaachama na ukodishaji huo. Kwa mujibu wa Kalufya, transmita hiyo mpya itawafikisha mbali zaidi katika pwani za Ziwa Tanganyika na hivyo kuleta mabadiliko yanayokusudiwa. Kalufya alisema wananchi wakisikia mambo mbalimbali ya kuwaelimisha na wao wakapata nafasi ya kutoa maneno yao haki za binadamu zitakuwa zimeheshimiwa sana nchini. Mkurugenzi wa Radio Jamii Uvinza FM, Ayubu Kalufya (kulia) akitoa neno la shukrani kwa hivyo Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kushoto) wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa vya radio hizo yaliyofanyika kwenye ofisi za shirika hilo jijini Dar es Salaam.

Aliishukuru Unesco kwa kuendelea kuwasaidia na kusema kama si kwa msaada wa UNESCO jamii zilizopo pembezoni zisingepata nafasi ya kutoa madukuduku yao. Radio nyingine zilizonufaika na msaada huo ni Pangani FM. Radio hiyo sasa inaweza kusikika Tanga nzima badala ya Pangani pekee. Katika orodha ya redio zilizopatiwa vifaa ipo pia Mkoani FM ya kutoka Zanzibar.  Picha juu na chini ni Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues na Ofisa Utawala na Rasilimali Watu wa Radio Jamii ya Pangani FM, Rehema Kilapilo wakisaini hati za makabidhiano ya vifaa katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za UNESCO jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Maofisa kutoka sekta ya mawasiliano UNESCO. Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akikabidhi hati ya makubaliano na moja kati ya vifaa hivyo kwa Ofisa Utawala na Rasilimali Watu wa Radio Jamii ya Pangani FM, Rehema Kilapilo wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za shirika hilo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Maofisa kutoka sekta ya mawasiliano Unesco Dar es Salaam. Picha juu na chini ni Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues na Meneja wa radio ya Jamii ya Baloha FM ya Kahama, Samada Maduhu kwa pamoja wakisaini hati za makabidhiano ya vifaa hivyo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za UNESCO jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Maofisa kutoka sekta ya mawasiliano UNESCO Dar es Salaam. Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akikabidhi hati ya makubaliano na moja kati ya vifaa hivyo kwa Meneja wa radio ya Jamii ya Baloha FM ya Kahama, Samada Maduhu wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za shirika hilo jijini Dar es Salaam. Picha juu na chini ni Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues na Mkurugenzi wa Radio Jamii Uvinza FM, Ayubu Kalufya kwa pamoja wakisaini hati za makabidhiano ya vifaa hivyo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za UNESCO jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Maofisa kutoka sekta ya mawasiliano UNESCO. Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akikabidhi hati ya makubaliano na moja kati ya vifaa hivyo kwa Mkurugenzi wa Radio Jamii Uvinza FM, Ayubu Kalufya wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za shirika hilo jijini Dar es Salaam. Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akigonga 'cheers' na wawakilishi wa redio jamii zilizopokea vifaa hivyo kwenye hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za shirika hilo Unesco jijini Dar es Salaam.

No comments: