Tuesday, August 1, 2017

SERIKALI YAONGEZA MUDA WA KUNYONYESHA KWA WATUMISHI WA UMMA NA MASHIRIKA NA SEKTA BINAFSI

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii .

SERIKALI imeongeza masaa ya unyonyeshaji kwa watoto kwa watumishi wa serikali, mashirika pamoja sekta binafsi ili kuwezesha watoto kuwa na afya bora inayotokana na maziwa ya mama.

Hayo ameyasema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akifungua Wiki ya Unyonyeshaji, amesema kuwa mama mzazi baada ya kumaliza miezi mitatu ataingia kazini 3:30 na kuondoka saa 7:30 katika kumuwezesha mama kunyonyesha mtoto bila kuingiliwa na majukumu ya kikazi.

Ummy amesema kuwa watendaji wa Umma na mashirika pamoja na taasisi lazima wafanye hivyo katika kutambua umuhimu wa mama mzazi kunyosha kwa muda uliowekwa kwa kipindi cha miezi sita.

Amesema kuwa ni gharama kubwa katika kuhudumia watoto walio na utapiamlo ambao unatokana moja ni kukosa maziwa ya mama kwa muda mrefu hivyo kuepuka ni nyia rahisi ikiwemo kutengwa kwa masaa hayo.

Waziri Ummy amesema kuwa suala la lishe lazima liangaliwe kwa ukaribu na wadau wote katika kuweza kuwaondoa watoto katika utapiamlo ambao unafanya kudumaa kwa akili.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Chakula na Lishe Nchini(TFNC), Joyceline Kaganda amesema jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanyika juu ya masuala ya lishe na wadau kwa mifumo mbalimbali.

Amesema kuwa wiki ya unyonyeshaji wa kina mama ni muhimu katika katika ukuaji wa mtoto wa kumjenga katika afya bora.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Lishe nchini (Panita), Tumaini Mkindo amesema serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. Pombe Magufuli imwemeka kipaumbele katika ubaoreshaji wa lishe nchini.

Amesema kuwa sera zimeweza kuongezeka katika masuala ya lishe ikiwa eneo la kipaumbele katika mpango wa taifa wa miaka mitano pamoja mikoa na halmashauri kuwa na bajeti ya lishe.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akipata maelezo juu masuala ya lishe kutoka kwa mtaalam wa lishe wa Taasisi ya Chakula lishe nchini (TFNC),Neema Joshua wakati maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji leo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya unyonyeshaji na uzinduzi usambazaji taarifa kwa njia ya simu leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chakula na Lishe Nchini(TFNC), Joyceline Kaganda akizungumza juu ya mikakati ya lishe na umuhimu wa unonyeshaji leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Lishe nchini (Panita), Tumaini Mkindo akitoa salamu za mashirika yasio ya kiserikali yanavyofanya kazi katika sehemu ya lishe kwa kuwa miradi mbalimbali.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akibonyesha kitufe kuashiria uzinduzi wa taarifa kupitia simu za mikoni katika ufunguzi wa wiki ya unyonyeshaji leo.
Sehemu ya wadau katika ufunguzi wa wiki ya unonyeshaji leo jijini Dar es Salaam.

No comments: