Monday, August 21, 2017

DKT. KALEMANI AFANYA MKUTANO NA WATENDAJI WA NISHATI NA MADINI

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani amefanya kikao cha kazi na wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Taasisi ikiwa ni pamoja na Shirika la Umeme la Tanzania (TANESCO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Chuo cha Madini Dodoma (MRI), Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO). Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kujadili mafanikio na changamoto katika utendaji kazi wa Wizara.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akizungumza na watendaji pamoja na wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake (hawapo pichani) katika kikao hicho. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo na kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. James Mdoe.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. James Mdoe (kushoto) akielezea mafanikio ya sekta za nishati na madini nchini katika kikao hicho.
Sehemu ya watendaji na wafanyakazi kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) katika kikao hicho.

Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Haji Janabi akitoa mchango wake kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi kutoka Idara ya Manunuzi Wizara ya Nishati na Madini, Amon MacAchayo akifafanua jambo katika kikao hicho.
Mtaalam kutoka Idara ya Madini, Wizara ya Nishati na Madini, Philip Mathayo akifafanua jambo katika kikao hicho.
Mjiolojia kutoka Idara ya Madini, Wizara ya Nishati na Madini, Ezekiel Seni akitoa maoni yake katika kikao hicho.
Mkufunzi kutoka Chuo cha Madini Dodoma (MRI), Joseph Mtui akielezea mikakati ya uboreshaji wa chuo hicho katika kikao hicho.

No comments: