Friday, August 18, 2017

CHUO CHA UFUNDI ARUSHA CHAZINDUA MTAALA MPYA WA GESI NA MAFUTA


Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Hagnery Chitukulo amekipongeza Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) kwa uamuzi wake wa kushirikiana na Chuo cha Camosun cha nchini Canada kuandaa mtaala wa ufundi bomba,gesi na mafuta katika ngazi ya Diploma.

Akizindua mtaala huo ambao ni kwanza na aina yake nchini alisema utaisadia serikali kuwapata vijana wengi wenye utaalamu wa sekta ya mafuta na gesi nchini katika ngazi hiyo ambayo imenekana kuna pengo kubwa nchini.

“Mafunzo haya yatasaidia sana kuwapata wataalamu wetu na itaipunguzia serikali mzigo wa kuwaajili wataalamu wa kigeni ambao ulipwa fedha nyingi za kigeni,”alisema

Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha,Dk Richard Masika amesema baada ya kutambua mahitaji makubwa ya wataalamu wa fani hiyo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita walikua wakiaanda mtaala kwa ushirikiano na Chuo cha Camosun na mafanikio yamepatikana.

Alisema kozi hiyo ni nyumbufu itakayowawezesha wanafunzi kufanya kazi baada ya kumaliza mwaka wa kwanza na baadaye kuendelea na masomo jambo ambalo litakua likiwapa maarifa kwa vitendo zaidi badala ya nadharia pekee.

Mmoja wa wanafunzi wanaosoma kozi hiyo ambayo imegharamiwa na serikali ya Tanzania,Latifa Mkombo amesema wanaishukuru serikali kwa kutoa ufadhili huo na kuahidi kusoma kwa bidii kwaajili kuingia katika ajira za gesi na mafuta.
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Hagnery Chitukulo akizungumza wakati wa ufunguzi wa kozi ya ufundi bomba,mafuta na gesi katika chuo
cha Ufundi Arusha(ATC) jijini Arusha,kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Camosun nchini Canada,Sherri Bell na kulia ni Mkuu wa Chuo cha ATC,Dk Richard Masika. 
Afisa wa kitengo cha biashara katika ubalozi wa Canada nchini,Anita
Kundy akisoma hotuba yake,kushoto ni Mshauri wa ufundi kutoka nchini Canada,Dk Alan Copeland. 
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Hagnery Chitukulo akionesha nakala ya mtaala mpya wa kozi ya ufundi bomba,mafuta na gesi uliozinduliwa
katika chuo cha Ufundi Arusha(ATC) 
Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi nchini(TVET)Wizara ya Elimu,Sayansi na
Teknolojia,Mhandisi Thomas Katebalirwe akizungumza jambo katika hafla ya uzinduzi huo. 
Baadhi ya wanafunzi wa mwanzo wa kozi ya ufundi bomba na utaalamu wa gesi na mafuta katika Chuo cha ufundi Arusha 

Mgeni rasmi Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Hagnery Chitukulo(wa tatu kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na wageni kutoka Chuo cha
Camosun,Victoria nchini Canada na Chuo cha ATC. 

No comments: