Wednesday, July 26, 2017

BALOZI WA KUWAIT NCHINI JASEM AL-NAJEM AUNGA MKONO SERA MAGUFULI YA ELIMU BURE

Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani imezindua visima vitano virefu vyenye thamani ya zaidi ya milioni hamsini vilivyotolewa msaada na ubalozi wa Kuwait nchini.
Visima hivyo vitano vilivyozinduliwa vimejengwa katika kijiji cha Kisayani, Kerekese, Mpafu, Sotele na Sangasanga  vya Mkuranga.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo wilayani mkuranga mkoani pwani balozi wa Kuwait  Mhe. Jasem Al-Najem alisema serikali ya Kuwait kupitia ubalozi uliyopo nchini inafanya jitihada kubwa kusaidia Tanzania katika nyanja mbalimbali zinazohusu Jamii ikiwemo afya pamoja na maji.
Aidha balozi Jasem alisema katika kuunga mkono sera ya Rais wa awamu ya tano Dkt John Pombe Magufuli ya elimu bure wameamua kuanzisha mradi ujulilanao wa kisima kila shule ili kupinguza changamoto ya maji pamoja na kuakikisha wanafunzi wanapata maji safi na salama kwa wakati lengo nikuboresha elimu nchini."maji no muhimu sana uchimbaji wa maji mashuleni sio utasaidia wanafunzi na wanachi wanaoishi karibu na kusaidia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kupata huduma kamili ya masomo"alisema.
Pia ubalozi huo umetoa mabeseni hamsini pamoja na vifaa vya akina mama wakati wa kujifungua katika hospital ya wilaya ya mkuranga ili kuboresha huduma ya afya.
Aidha Mbunge wa viti maalum mkoa wa pwani Zainabu Vulu alisema afya ya Mama na mtoto  ni muhimu sana na kukikosekana vifaa afya ya mama itakuwa hatarishi."tunashukuru sana kwa msaada wenu huu utasaidia sana mama kujifungua mtoto mwenye afya na mwenyewe kubaki mwenye afya "alisema.
Hata hivyo Mbunge wa jimbo la mkuranga mh. Abdalah Hamis Ulega amewashuru kuwait kwa msaada huo na kusema mpaka sasa wameshachimba visima ishirini visima nane kati ya hivyo ni vya serikali.
Aidha aliongeza kama Mbunge wa mkuranga aliguswa na kuamua kutafuta wafadhili baada ya kupata barua kutoka kwa Mwalimu mkuu wa shule ya msingi kisayani kutaka kuifunga shule hiyo kutokana na changamoto ya maji,ndipo akawatafuta wafadhili hao ambao wamechima visima virefu vitano vya maji wilayani humo.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya mkuranga Filiberto Sanga alitoa wito kwa wanachi kuhakikisha wanakitunza kisima hicho kisiharibike.
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filberto Sanga akizunguma  na wanacnhi wa kijiji cha Mpafu katika hafala ya uzidunzi wa visima vitano vyenye thamani ya zaidi ya milioni hamsini vilivyotolewa msaada na ubalozi wa Kuwait nchini Visima hivyo vitano vilivyozinduliwa vimejengwa katika vijiji vya Kisayani, Kerekese, Mpafu, Sotele na Sangasanga 

 Balozi wa Kuwait nchini, Mhe Jaseem Al Najem akizungumza na wanchi wa kijiji cha Mpafu kataika uzinduzi wa visima virefu vitano vilivyo fadhiliwa na Ubalozo wa Kuwet nchini leo mkoani Pwani.
 Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdalah ulega akimshukuru Balozi wa Kuwait nchini, Mhe. Jaseem Al Najem kwakuchimba visima hivyo.
 Mganga  Mkuu Wilaya ya Mkuranga Dkt.Steven Mwandambo wa (kwanza kushoto) akitoa maelekezo mbele ya Balozi wa Kuwait nchini, Mhe Jaseem Al Najem,watendaji wakuu wa wilaya katika hafla ya uzidunzi wa visima virefu vitano vilivyo vyenye thamani ya zaidi ya milioni hamsini.
 Balozi wa Kuwait nchini, Mhe Jaseem Al Najem wa (pili kushoto) akikabidhi watendaji wa wilaya ya mkuranga mabeseni hamsini pamoja na vifaa vya akina mama wakati wa kujifungua katika hospital ya wilaya hiyo.Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii
 Balozi wa Kuwait nchini, Mhe Jaseem Al Najem akizindua kisima  katika kijiji cha Mpafu kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filberto Sanga, Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdalah ulega.
 Picha ya pamoja
Balozi wa Kuwait nchini, Mhe Jaseem Al Najem wakionja maji baada ya kuzindua kisima  katika kijiji cha Mpafu kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filberto Sanga, Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah ulega.
Picha na habari na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii

3 comments:

shuja said...

IMC provides Digital Solutions to clients spread across the globe. Our services provide ethical Digital Marketing Services which offer innovative solutions From the past 6 years. We are providing different types of Digital Marketing Services like Search Engine Optimization (SEO), Social Media Marketing (SMM), Pay Per Click (PPC), Content Marketing (CM), Email Marketing (EM), Web Designing. The team of IMC is informing that, Every kind of Digital Marketing Service will be available with a good commitment for all types of business holders in Dubai, UAE.
Internet Marketing Company

Spider Business Center said...

virtual office in dubai- Establish Your Company's presence in the Most Prestigious Business Address and Get a new height to your business.

Idx Website For Realtors said...

Nice article I'm impressed to see this blog, very interesting and thanks for sharing all the information with all of us. Very useful for me. Good information. Thank you for sharing with us.
Best Idx Websites For Realtors
Best Real Estate Agent Websites With Idx
Idx Website For Realtors