Sunday, May 28, 2017

Biko kutoa Milioni 20 jumatano hii, mwingine aibuka na 10M Arusha

BAHATI Nasibu ya Biko Ijue Nguvu ya Buku, sasa imezidi kuchanja mbuga baada ya kuongeza donge nono la washindi wa droo zao kubwa, ambapo sasa mshindi wa droo ya Jumatano hii anatarajiwa kunyakua jumla ya Sh Milioni 20.

Mbali na kutoa kiasi hicho cha pesa, tayari imempata mshindi wake wa droo ya tisa ya Jumapili ambaye ni Leopard Mpande wa jijini Arusha, aliyenyakua Sh Milioni 10 huku pia Biko ikiwa imeshapata washindi zaidi ya 35,000 wa papo kwa hapo. 

Balozi wa Biko Tanzania Kajala Masanja kulia akizungumza jambo wakati wa kuchezesha droo ya tisa ambapo mkazi wa Arusha, Leopard Mpande aliibuka kidedea kwa kutangazwa mshindi hivyo atajinyakulia Sh Milioni 10 kutoka Biko. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo.

Kajala Masanja akizungumza na Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo.
Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo kushoto akiandika dondoo za mshindi wa Sh Milioni 10 wa Biko aliyetangazwa leo jijini Dar es Salaam, ambapo mkazi wa Arusha, Leopard Mpande aliibuka kidedea katika droo hiyo.

Akizungumza leo katika droo iliyompata Mpande, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage, alisema kwamba wameamua kuongeza zawadi ya droo kubwa ya jumatano hii kutoka Sh Milioni 10 hadi 20 ili kuwawesha washiriki nafasi ya kujikwamua kimaisha kwa zawadi za BIKO, "Changamkieni fursa hii" alisema.

Alisema droo ya kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 20 itafanyika Jumatano, huku akiwataka watu wacheze mara nyingi zaidi kwa kufanya miamala kwenye simu zao za MPESA, TIGOPESA na AIRTEL Money kwa kuingia kwenye kipengele cha lipa bili au lipa kwa MPESA ambapo watatakiwa waingize namba ya kampuni ambayo ni 505050 na kuweka pia namba ya kumbukumbu ambayo ni 2456.

“Ukifanya hivyo utaweka kiasi cha kununua tiketi kuanzia Sh 1000 au zaidi ambapo Sh 1000 itakuwa na nafasi mbili za ushindi kwenye droo kubwa ya Jumatano pamoja na kushinda zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na sh 1,000,000, huku donge kubwa likipanda kutoka Sh Milioni 10 hadi 20 Jumatano hii.


“Biko ni kutoa pesa kwa washindi wetu ili wafanikiwe katika maisha yao, hivyo wanachotakiwa kufanya ni kucheza mara nyingi, huku pia nikimpongeza mkazi wa Arusha, ndugu Mpande kufanikiwa kuibuka na Sh Milioni 10 katika droo iliyochezeshwa Jumapili,” Alisema.

Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Jehud Ngolo, aliwapongeza Biko kwa kufikia hatua ya kutoa Sh Milioni 20 kwa washindi wa droo kubwa ya Jumatano akisema ni hatua nzuri, hivyo Watanzania wanapaswa kuchangamkia fursa hiyo ili waibuke na mamilioni ya Biko.

“Sisi tunafuatilia kwa karibu mchezo wa Biko na tunaridhishwa na utaratibu wao wa upatikanaji wa washindi wa droo zao kubwa na ni mchezo wenye uaminifu mkubwa hapa nchini ambapo wanatarajia droo ya Jumatano hii kutoa Sh Milioni 20, jambo ambalo ni zuri kwa mustakabali wa kukuza uchumi kwa washiriki wote wa bahati nasibu ya Biko,” Alisema Ngolo na kumpongeza pia mshindi wa Arusha aliyeibuka na jumla ya Sh Milioni 10,” Alisema.

Kwa mujibu wa Biko, droo ya Jumatano hii itatoa Sh Milioni 20, huku mshindi wao wa Arusha wa Sh Milioni 10 akitarajiwa kukabidhiwa fedha zake haraka iwezekanavyo kama walivyopewa washindi wengine walioshinda katika droo nane za Jumatano na Jumapili zilizopita.

No comments: